Inhalt

Cover

KUHUSU UNABII HUU

Susan ana kipaji cha unabii. 1 Wakorintho 14:1 yasema “Ufuateni upendo na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu.” Tunaishi na tunahitajika kutii maagizo ya Mungu katika Agano Jipya. Ijapo kuna baadhi wanao amini kuwa vipaji vya kiroho kama unabii havipo tena. La sivyo. Hizi ni fikra za ubinadamu wala sio za Mungu. Mungu hajabadili agano lake. Tungali katika enzi za Agano Jipya. Tafadhali nawaomba muelewe ya kwamba sharti lako la kwanza ni kwa Bwana Yesu Kristo na neno lake kama ilivyoandikwa kwenye Bibilia. Hasa Agano Jipya. Kama ipasavyo, unabii wote wafaa kupimwa kulingana na Bibilia. Ikiwa unabii unalingana na Bibilia, basi tunatarajiwa kutii. Kwa sasa, Mungu hatumii unabii ili kutuletea imani au kanuni mpya, bali anautumia ili kuimarisha maneno yake ambayo tayari ametupa katika Bibilia. Mungu pia anatumia unabii kutuonya binafsi kuhusu matukio yajayo ambayo yatatuathiri.

Jinsi ilivyo katika Agano la Kale, Mungu hutumia manabii katika nyakati hizi za Agano Jipya. Katika kitabu cha Matendo ya Mitume ambacho kimo kwenye Agano Jipya kinataja manabii kama Yuda na Sila (Matendo ya Mitume 15:32) na Agabo (Matendo ya Mitume 21:10) na wengine wengi. Huduma ya wanabii inazungumziwa pia katika 1 Wakorintho 12:28; 14:1, 29, 32, 37 na hali kadhalika katika Waefeso 2:20; 3:5; 4:11. Yesu huwachagua manabii wamtendee kazi duniani. Pia Yesu anatumia unabii na manabii kutueleza matakwa yake kwetu wanawe. Bibilia iliandikwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Kuna baadhi ya watu wanaosema kuwa unabii unaweza kuongezea ua kupunguza maandiko ya Bibilia. Bibilia yenyewe inasema kuwa unabii ni moja ya karama za Roho Mtakatifu. Bibilia inaongezewa au kupunguzwa wakati watu wanaongezea maneno yao wenyewe kupitia fafanuzi mbali mbali na hata kuongezea dhana zao wenyewe ambazo hazitoki kwa Mungu na zinatokana na mawazo ya kipagani. Kazi ya kimsingi ya wanabii katika Bibilia imekuwa na itaendelea kuwa ya kuwarejesha watu kwa neno la Mungu na kwa Bibilia kama inavyosema katika 1 Wathesalonika 5:19-21“Msimzimishe Roho; msitweze unabii; jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema.” Jinsi ya kujaribu ujumbe huu ni kwa kulinganisha yaliyomo na yale Bibilia isemayo. Katika unabii wote ulioko hapa, mimi binafsi (Mike Peralta) nimeujaribu ujumbe wote ulioko hapa na unakubaliana na Bibilia. Ningependa wewe msomaji pia ujaribu ujumbe huu mwenyewe na kuulinganisha na Bibilia. Ikiwa unalingana na Bibilia, basi ni dhahiri kuwa Mungu anakutaka uutwae kwenye moyo wako na kuyatii maagizo yake.

 

YALIYOMO

Utambulisho kutoka kwa Bwana Yesu

Sura ya 1. Unyenyekevu

Sura ya 2. Msiweke imani yenu kwenu wenyewe au kwa wengine

Sura ya 3. Jifunzeni unyenyekevu

Sura ya 4. Kumuamini Mungu

Sura ya 5. Msamaha

Sura ya 6. Ishini duniani ila msiwe mmoja wa “wale wa dunia”

Sura ya 7. Unyakuo na Karamu ya Arusi ya Mwana Kondoo

Sura ya 8. Jitayarisheni kwa unyakuo

Sura ya 9. Kuhusu Kanisa lililopotea

Sura ya 10. Tamaa ya ulimwengu

Sura ya 11. Ulimwengu unaelekea kwenye dhiki

Sura ya 12. Naja hivi karibuni

Sura ya 13. Muda unayoyoma wanangu

Sura ya 14. Ulimwengu umenigeuka

Sura ya 15. Wachungaji hawanifuati

Sura ya 16. Wakati wa kurudi kwangu umewadia

Sura ya 17. Kuhusu Mpinga Kristo

Sura ya 18. Wakati unakaribia wa kurudi kwangu

Sura ya 19. Jitayarisheni

Sura ya 20. Wakati wenu u karibu kwisha 

Sura ya 21. Mbali na mapenzi yangu mwanipinga

Sura ya 22. Uovu waja kuuteketeza ulimwengu

Sura ya 23. Saa sita ya usiku inakaribia

Sura ya 24. Acheni kupigana wenyewe kwa wenyewe

Sura ya 25. Sitawachukua ikiwa mngali na dhambi ambayo hamjatubu

Sura ya 26. Nitazameni mimi

Sura ya 27. Hamna budi kujitayarisha ikiwa mwataka kuja nami

Sura ya 28. Uzima wenu wa milele u mashakani

Sura ya 29. Lazima munikimbilie sasa sio kutembea

Sura ya 30. Bi arusi wangu apendeza kwa njia zake zote

Sura ya 31. Ni wachache sana wanaoniabudu na kutubu kwangu

Sura ya 32. Ni karibu kumuondoa bi arusi wangu na kumpelekea mahali palipo salama

Sura ya 33. Aidha mnipe nafasi ya kwanza ama msinipe nafasi yoyote ile

Sura ya 34. Kuna dhiki yaja – dhiki kuu

Sura ya Sura ya 35. Hakuna manufaa yoyote kuiikimbiza dunia inayokufa

Sura ya 36. Wengi wadhaniao wa tayari wajidanganya

Sura ya 37. Muda uliosalia ni mfupi sana

Sura ya 38. Wafuasi wangu kamili wanakesha wakiningojea - wanajiadhari

Sura ya 39. Ushuhuda

 

 

UTAMBULISHO KUTOKA KWA BWANA

 

Wanangu, huyu ni Bwana wenu anayenena nanyi. Naja kwa upesi. Kurudi kwangu kumewadia, Ni mlangoni. Naja! Jitayarisheni.

 

Ujumbe huu uliandikwa na binti yangu Susan akiwa kwa mfungo wa siku arobaini, kwa ombi langu. Nilimleta mahali faragha ili aweze kujinyima. Nilimpa maneno mengi niliyotaka yawajie ninyi wanangu. Kwa hivyo aliyaandika jinsi nilivyo mwelekeza. Barua hizi zote zina ujumbe maalum ambao mnahitajika kuusoma na kutafakari kwa maana kurudi kwangu kumekaribia.

 

Ni Mimi Bwana na Mwokozi wenu,

 

YAHUSHUA (Yesu Kristo) 

 

 

 

 

 

 

USHUHUDA

Maneno haya yote aliyasema Mungu Baba, na mwanawe YAHUSHUA HA MASHIACH (Yesu Kristo au Yesu Mwenye upako au Yesu Masiya) kwa Susan akiwa kwa mfungo wa siku arobaini. Maneno haya yalirekodia kati ya Januari 27, 2012 na Machi 6, 2012.

 

USHUHUDA

Nakushukuru sana kwa barua zako pepe unazotutumia ukituelezea maneno ya Mungu. Niliomba na kumuuliza Roho Mtakatifu aniongoze niweze kuelewa mambo mengi na kutembea kwa njia za Bwana. Niombee. Mungu aibariki huduma yako. – Msomaji wa 1

 

Dada Susan, asante sana YAHUSHUA kwa barua hizi na yote yale uliompitishia binti yako ili aziandike. Nilianza kuzisoma na ninasoma kurasa kumi kila siku. Nimebarikiwa. – Msomaji wa 2

Susan, asante sana kwa barua hizi. Zimenibariki sana na ninahisi moyo wangu ukiona njaa ya kumjua Bwana YAHUSHUA. –msomaji wa 3

 

Dadangu Susan, naelekea kumaliza kusoma barua hizi za Mungu. Kweli ni maneno ya ajabu. Nashindwa kuweka kitabu chini. Ukweli wake, hekima yake na jinsi anatusihi tumfuate ni ajabu. Ni mnyenyekevu na mwenye upendo anavyotuhimiza, na kuonya mataifa. Namshukuru kwa yote. Ubarikiwe sana. – Msomaji wa 4

 

Susan, asante sana dada kwa kunitumia barua hizi. Zimenifanya nimuabudu Mungu. Naomba mamilioni ya watu watafanya vivi hivi. Mungu akubariki sana kwa utiifu wako na uaminifu wako kwake. Upendo wa milele ndani ya Masiya. – Msomaji wa 5

 

Susan, huu ni unabii ulio na upako mkuu kutoka kwa Bwana. Nimesoma unabii mwingi tangu nilipokuwa mkristo mchanga mwaka wa 1979. Nimesikia na kusoma unabii mwingi kwa miaka 33 lakini maneno yaliyoko katika kitabu hiki ndiyo maneno yaliyo na upako mkuu niliyo yasikia maishani mwangu mwote.- Mike Peralta (aliyekiandika kitabu hiki)

 

SURA YA 1: UNYENYEKEVU

Unyenyekevu ni utufu. Ni kukubali kuwatumikia wengine bila manung’uniko, kuwasamehe wenzako wanapokukosea. Ni kuwa na hamu ya kuwatumikia wengine na kumpendeza Mungu. Ni kutaka kumtumikia Bwana kila wakati kwa matumaini. Ni kuwa na moyo ulio tayari kumtumikia Bwana na watu wengine. Unyenyekevu pia ni kukubali kuwa wa mwisho, usiyeonekana hadharani.

Luka Mtakatifu 14:7-11. Akawaambia mfano wale walioalikwa alipoona jinsi walivyochagua viti vya mbele, akasema, Ukialikwa na mtu harusini, usiketi katika kiti cha mbele isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahiwa kukuliko wewe, akaja Yule aliyewaalika wewe na yeye na kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa haya kushika mahali pa nyuma. Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma, ili ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele zaidi; ndipo utakapokuwa na utukufu mbele ya watu wote walioketi pamoja nawe. Kwa maana kila ajikwezaye atadhaliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.

Mathayo Mtakatifu 19:30. Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.

Ni yule mtu ambaye anasahaulika kwa maana yeye ni mtu duni, anachanganyika na mandhari. Hawataki kuwa katikati ya mambo. Wanataka wafichike mbali, polepole, wakimtii Mungu. Huu ndio unyenyekevu, binti yangu na huyu ndiye bi arusi wangu.

Yeye ni hivi vitu vyote nilivyotaja. Sasa wayaona makosa yako binti yangu? Tuendelee…

Kuwa mnyenyekevu maana yake ni nini? Ni kufanya kazi bila kuonekana na bila kutamani umaarufu. Ni kumtii Mungu kikamilifu. Ni kutafuta kumtii Mungu katika mambo yote. Unyenyekevu ni kutojali yale watu wengine wanafikiria juu yako. Ni kuwatendea wengine bila kusifiwa. Ni kutamani fadhili kutoka kwa Mungu wala sio kwa binadamu. Ni kukuwa katika fadhili za Mungu na kumpendeza Mungu.

Ni enye upole na kusadiki.

Ni enye kukuwa katika Mungu.

Ni kuwa kama Yesu.

Unyenyekevu wapendeza mbele za Mungu. Mtu mnyenyekevu na anayemwogopa Mungu hung’aa machoni pa Mungu. Unyenyekevu ni kutaka kumfurahisha Mungu na kutaka kutembea katika njia zake. Kujishusha na kutojifikiria kuwa bora kuliko wengine, kujiona chini ya wengine na kutowahukumu walio karibu nawe. Mimi pekee ndiye nafaa kuhukumu. Simaanishi ujifadhaishe ila uziheshimu hisia za wenzako. Na wanapoanguka, usiwadharau kimoyomoyo bali uwahurumie maanake hata wewe pia waweza kuanguka kwenye dhambi mbele ya Mungu aliye Mtakatifu.

Hivi ndivyo inavyokuwa mtu aki nyenyekea. Wanakuwa na ushuhuda wa kupendeza. Wanang’aa katika ufalme wangu, machoni mwangu. Nawapa sikio langu. Wanaponililia nawasikiza. Naweza kuwatendea lolote hata liwe gumu kiasi gani. Nitafanya lote liwezekanalo kwa ajili ya watumishi wangu wanyenyekeao. Je binti yangu, unayaelewa haya? Watumishi wangu wanyenyekevu wanajitolea kwangu.

Wanaelewa kuwa hawawezi kutenda lolote bila mimi. Kila mara wananitafuta kwa kila jambo jinsi mtoto amtafutavyo mzazi. Huyu ndiye mtumishi wangu mnyenyekevu. Hawana hiari yao. Wananiamini mimi katika mienendo yao ya kila siku. Wananitafuta ili wapate majibu yao kutoka kwangu. Huniamini kwa moyo wote nami huwajibu. Nawapa yaliyo mema maana wananitegemea kwa mambo yao yote. Ni wanyenyekevu na watukufu machoni mwangu. Wana uzuri mpole. Sio kama watu wa dunia.

Wanajitokeza kutoka kwa umati wa watu. Uzuri wao ni wa Kimungu na wa mbinguni. Hivi ndivyo mbinguni kulivyo – kumejaa watu waliosalama kwa Mungu wao kwa sababu nakutana na mahitaji yao yote.

Hawana haja ya kuwa wafidhuli na wenye kiburi. Mahitaji yao yote yatimizika kupitia kwangu. Wanaridhika, wananitumikia kwa hiari yao, na wanafurahia kuwatumikia wengine kuwa maana natosheleza mahitaji yao kila wakati. Hakuna yule anayepigania kuonekana kuliko wengine mbinguni. Kila mtu ameridhika. Mbinguni ni mahali pasafi, patakatifu, patulivu, penye pendo, furaha na kicheko.

Imani kama ya mtoto ndiyo yenye maana, kwa sababu mtoto hakimbii mbele. Mtoto humfuata mzazi nyuma na kwa karibu kwa sababu ana imani na mzazi wake. Anamkwamilia mzazi akimngoja amuongoze na kumfunza. Mtoto haichukui nafasi ya mzazi. Anafahamu vyema kuwa hawezi kuongoza. Ana imani kuwa mzazi wake atakutana na mahitaji yake yote. Mtoto anapoenda mbali na mzazi wake, anakuwa na wasiwasi na mahangiko maanake anafahamu kuwa yule mzazi wake ambaye anamwamini na kumpenda ndiye tu anayeweza kukutana mahitaji yake yote. Hivi ndivyo uhusiano ulivyo kati ya Mungu na yule mtumishi wake myenyekevu. Watu wanyenyekevu humfuata Mungu kama vipofu maanake wamwamini, naye Mungu huwakomboa.

Hamna majibu kwingine. Mungu ndiye Mkuu na ndiye Tumaini la pekee. Tumaini la kutegemewa. Watoto huwatafuata wazazi ili wawatimizie mahitaji yao yote. Wanawalilia maanake wazazi wao watawakomboa kama vile Mungu awakomboao wanyenyekevu wake wamfuatao kwa moyo mnyenyekevu na safi.

Je, unayaelewa haya binti yangu? Je, mtu aliye na kiburi anaweza kubadilika na kuwa mnyenyekevu? Binti yangu jibu ni “ndiyo” kwa kuongozwa na kunitii mimi, Mungu wenu.

Kwa hivyo, yote yanawezekana kwa Mungu. Ndiyo, yote yawezekana kwangu.

Mithali 15:33. Kumcha Bwana ni maonyo ya hekima. Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.

Haya tuanza. Unyenyekevu ni upendo. Upendo unatokana kwa moyo mnyenyekevu. Upendo hautoki kwa kiburi. Kiburi huharibu upendo. Kiburi husema:

“Mimi ni bora kukuliko”.

“Najua mengi kukuliko”

“Haustahili mengi kuniliko”

“Hauna thamani kuniliko”

“Mimi naweza kujisimamia na “sikuhitaji”.

Kiburi kinasimamia haya yote, mwanangu.

Kiburi ni kibaya kwa njia zote. Ni kujifikiria mwenyewe tu, ni kujipendekeza, ubinafsi na mizizi yake iko kwenye uovu. Utukufu usio na maana unajipandisha juu ya Mungu na kujidai “Simuhitaji Mungu” Mimi ni Mungu. Najitawala. Kiburi huchukiza mno. Hamna uzuri wowote kwenye kiburi. Hakuna wokuvu kwa kiburi. Kiburi kina wazuia wengine. Kinawafanya wengine wajione duni wasiopendwa, wanakataliwa, wanaumizwa na kukwazwa. Kiburi ni tofauti sana na tabia za Kristo. Hakuna ukristo wowote katika kiburi. Hakuna kitu cho chote kizuri kitokacho kwenye kiburi – ni uovu mtupu. Unanielewa mwanangu? Je, twawezaje kutoroka kiburi Bwana? Binti yangu, kimbia mbali na kiburi, toroka kabisa uende mbali na kiburi. Tafuta unyenyekevu wakati wote.

Binti yangu, hauna haja ya kujipendekeza kwa watu ikiwa una mapenzi yangu.

Tafuta pendo langu na utosheke nalo na tamaa yo yote ile ya kutaka mapenzi kutoka kwa walio kuzunguka itafunikwa na hili pendo langu kuu. Waliokuzunguka, hawawezi kutosheleza mahitaji yako ya ndani. Mimi tu pekee. Mimi ndiye niwezaye kutosheleza moyo ulio na njaa, tupu na unao tamania.

Nina majibu yote ya moyo kama huu. Mimi ndiye pekee naweza kuujaza. wanadamu hawawezi. Hawana huo uwezo ingawa huwa wanaonekana kama kwamba wanao. Kukubaliwa na watu ni kwa muda mfupi tu. Mimi ndicho kisima kijazacho kote. Najaza na kutosheleka hamu ya moyo wa binadamu. Njooni kwangu ili mtosheleze haja zenu za mapenzi. Wekeni kiburi chini. Ni nguvu zinazoharibu upendo. Zinatenda nje ya upendo na kuharibu kila mtu. Kiburi ndio uovu wa kwanza. Bado kinatawala na kuishi katika mioyo ya binadamu. Kiburi kinawafanya wanadamu watafute njia zilizo tofauti na mapenzi ya Mungu.

Binadamu hujijenga kwa kutumia ngazi zao kazini, mali, talanta, walivyonavyo, na uhusiano na wengine. Hii ni miungu na inawafanya wasimtazamie Bwana Mungu kwa majibu kuhusu maisha yao. Wajijenga wa kutumia njia ambazo sijabariki ndio waonekane kuwa wamefaulu kuliko wengine. Wale walio wanyenyekevu pekee yao ndio wamtafutao Bwana kuwapa majibu kuhusu maisha yao na kukutana na mahitaji yao. Wanaziacha tamaa za kutaka kufuata ulimwengu ili wajionyeshe kwa wenzao.

Wakati unapojikusanyia mali au kujitengenezea jina duniani, hata kupitia kwenye huduma ya Bwana, ni wewe unayetaka kukubaliwa na wengine walio karibu nawe. Hayo siyo mapenzi ya Bwana. Hayawezi kuwa mapenzi ya Bwana. Wanangu wanyenyekevu hunitafuta katika mahitaji yao ya kila siku nami huwakomboa. Hivi ndivyo niwafunzavyo imani. Wakati wanangu wanapambana wakitumia nguvu zao wenyewe ili wafaulu maishani, wanafeli maanake sitawatunukia wale walio nje ya mapenzi yangu. Ingawa wataonekana sawa na kila kitu laini lakini huo ni usalama wa uongo.

Pia, huwa nawaacha wafeli ndipo watambue kuwa wananihitaji. Nahitaji kuwa tamaa ya mioyo yao. Mimi ndiye jibu kwa yote. Vingine vyote ni matumaini ya uongo, yanayowaongoza wanangu nje ya mapenzi yangu.

Ndio, hawa ni wana wenye kiburi wanaopambana kwa njia zao wenyewe bila ushauri wangu, bila kunijua na bila kuniamini. Hii inawafanya wawe na utoshelezaji duni. Endeleeni kupambana. Ndio wanangu, pambaneni na mtatoka mkiwa tupu, mkitamani mengine zaidi bila kutosheka. Mtaendelea kuwa na tamaa, msielewe mnachokitamani. Mimi ndiye “hicho msichokielewa”. Mimi ndiye njia ya pekee ya kutosheka. Kutosheka kiroho, kimwili, na kimoyo.

Natosheleza, nakamilisha na ninamaliza. Najaza mapengo yaliyomo mioyoni mwa binadamu. Hakuna kitu kinachoweza kufanya hivyo, hata binadamu hawezi. Huu ndio msingi wa kiburi na dhambi inayotokana na kiburi. Moyo unaotafuta pahali pote ila kwa Mungu. Tupu, pweke na kutotosheka ndiyo matokeo ya moyo kama huu ulio na kiburi. Maisha ya huzuni ambayo Mimi Mungu sikutaka viumbe vyangu nilivyoviumba viishi.

Kiburi. Dhambi mbovu isiyo na upendo kwa njia yoyote ile. Hakina upendo na yeyote. Unyenyekevu kwa upande mwingine hupenda. Haujipendekezi. Hautawali wengine. Hungoja wengine watumikiwe kwanza. Huenzi wengine kujiliko. Hautumii wengine kwa manufaa yake. Haujigambi na sio fidhuli. Hauna maringo wala majivuno. Unyenyekevu wapendeza, ni mkarimu, ni wenye umbo zuri, wenye upendo, wenye kujali, kama Mungu, kama Kristu na humtafuta Mungu.

Unyenyekevu hautawali wengine wala kujilazimisha kwa cheo. Hungojea wakati wake. Una upendo wakati wote. Hautafuti kuwanyanyasa wengine ili uwe juu. Huwatafutia wema waliomzunguka.

Mbona unyenyekevu ni kitu bora kwangu mimi Mungu? Nafurahia wakati wanangu wananyenyekea mbele zangu. Hiyo inaonyesha heshima na imani kwangu mimi Mungu wao. Wananitumainia mimi ili niwatimizie mahitaji yao yote. Wanaondoa tamaa ya kutaka kujitafutia majibu kwa maisha yao hao wenyewe kupitia nguvu zao, ufanikishaji wao na kujipendekeza kwao. Hawafuati nia zao na kuniacha mimi Mungu wao. Hawajitegemei na kuniacha mimi ambaye ni njia ya kweli. Mimi Mungu wao. Mimi ndimi njia yao ya pekee. Njia ya kweli. Njia.

Wengi wamedanganyika wanaofuata njia zao bila kunisongea na kutafuta mapenzi yangu, ukweli wangu na mwelekeo wangu maishani mwao. Wanafuatilia vile ambavyo dunia inasema vi sawa: pesa, vyeo, kujulikana na kutafuta kujitosheleza kwa njia nyingi zisizofaa. Njia zilizo kando nami Mungu wao. Huo ni udanganyifu wa kiwango cha juu sana.

Sisemi eti msifanye kazi au kuishi maisha. Ninachosema ni kuwa mnitafute kwanza nami nitawaongoza na kuwaelekeza kwa njia zilizo sawa muishipo duniani. Mkifuatilia mipango na ndoto zenu bila mimi kuingilia kati basi mtakuwa mnaenda kando na mapenzi yangu. Hivyo mtakuwa mmejiweka wazi kwa adui wangu na mtakuwa mnaishi kwa dhambi kwa maana hamtakuwa kwenye mapenzi yangu. Hiki ni kiburi na ni uasi. Wengi wanatembea hivi.

Mithali 18:12. Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.

Mithali 29:23 Kiburi cha mtu kitamshusha; bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa.

Mathayo Mtakatifu 23:12. Na ye yote atakaye jikweza atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili atakwezwa.

Waraka wa Yakobo 4:6. Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hivyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.

Mithali 8:13. Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; kiburi na majivuno, ni njia mbovu na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.

Mtu anaketije katika mapenzi yako BWANA? Hivi ndivyo unavyokaa katika mapenzi yangu: Unitii kikamilifu. Kisha nitaziongoza hatua zako kila siku. Uje kwangu kila siku na kuniuliza nikuelekeze, nikuongoze, kama mtoto. Hii ndiyo imani kama ya mtoto. Ulimwengu wawadanganya watu kuwa kujitegemea ndiyo njia ya pekee ya kukuletea ushindi. Huu ni mpango wa adui wangu. Ameudanganya ulimwengu na uongo huu. Wanangu wanafukuza na kukimbiza maisha wakitumia nguvu zao na mipango yao bila kunishauri mimi muumba wao, na kuamini kuwa yote ni salama. Ikiwa inaonekana vyema, basi ni lazima iwe vyema. Lakini huu ni uovu ambao una nia ya kuwaondoa wanangu kutoka kwa njia nyembamba. Mimi pekee ndiye niliye na mwelekeo mwema. Njia iliyo sawa ya wanangu kutembelea nami nawapa mwelekeo huu kila siku.

Yohana Mtakatifu 5:30. Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi bali mapenzi yake aliyenipeleka.

Ikiwa watu wataendelea kuishi duniani watafanya mipango ya siku za baadaye. Itakuwaje sasa? Ndiyo mwanangu. Wanangu wanaishi duniani, lakini naweza kuwapa mwelekeo kuhusu mipango yao ya siku za baadaye ikiwa watanitafuta. Wakati mwingine jibu huwa: “Tulia na ungoje.” Wale wanangu walio karibu sana nami, watembeao nami kila siku ndio pekee watakaopewa utambuzi. Wanangu walio mbali nami na wananijia tu mara moja moja, sitawabariki. Mimi si Mungu unayemjia mara moja moja kama vile wengine wanaamini. Wengi hunijia wakati wa matatizo kisha wanarudi nyuma na kunisahau. Hawa wana hawanijui.

Mimi ni Mungu anayetamani urafiki wa karibu sana na wanangu. Wanaponikujia mara moja moja ni uovu mkuu. Vuguvu. Ninawatema.

Mathayo Mtakatifu 7:21-23. Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. 

 

 

SURA YA 2: MSIWEKE IMANI YENU KWENU WENYEWE AU KWA WENGINE

Sasa binti, tuanza. Leo nataka kujadiliana nawe kuhusu shida ya ‘ubinafsi’. Kujitosheleza, kujitegemea na kujipendekeza ni dhambi. Inakuzwa na mfumo wa kidunia na adui wangu.

Kujitegemea ni kuiweka nafsi yako mbele badala ya Mungu. Nikutembea kwa mapenzi yako badala ya mapenzi ya Mungu. Ni kama mfungo huu wa siku arobaini ni mapenzi yangu. Watu wanapofanya wapendalo bila kunitafuta kupitia uhusiano wa karibu nami, huwa nje ya mapenzi yangu na hivyo wanaishi kwenye dhambi. Hiyo ni kuniasi. Nataka wanangu wawe katika mapenzi yangu. Wakati mwingine mapenzi yangu hayaonekani yakiwa sawa kulingana na matarajio ya dunia. Dunia inasema fuata pesa, mali, ulinzi na mapenzi ya binadamu. Mapenzi yangu hayalingani na yale dunia huyaona kuwa sawa. Ni tofauti. Lakini mapenzi yangu ni sahihi.

Niliwaumba wanadamu ili waniamini na kutembea kwenye mapenzi yangu. Ili waweze kutembea kwa mapenzi yangu, yafaa wajitolee mhanga mbele yangu na kunitii kwa unyenyekevu na kunitafuta kila siku. Wale wanaonitafuta kwa ukweli kwa kutenga muda wa kuhusiana nami mahali pa siri na kusoma neno langu, watanipata na pia kupata mapenzi yangu. Hii inahitaji uchaguzi. Lazima uchague maanake mambo ya dunia yanaweza kukutoa kwenye njia yangu iliyonyoofu na nyembamba. O! Kuna njia zingine zakuendea lakini zote zitakuteketeza. Njia ya jehanamu ni pana na wengi huifuata. Wachache huipata njia hii iliyo nyembamba na muhimu inayokuja kwangu na kwa uzima wa milele. Wengi hudhani wako kwenye njia nyembamba lakini wamedanganyika. Wanawasikiza wengine waliopotea pia.

Viongozi wangu wengi wamedanganyika na wanawadanganya wengine kwa sababu wanaamini kuwa kufanya kazi nyingi na kukaa kanisani ukijishugulisha ndiko kutakupeleka Mbinguni. Huu ni udanganyifu. Uhusiano wa karibu nami, kunijua na kutumia wakati wako kunijua na kutenga muda kwangu. Huu ndio ufunguo wa usalama wa milele.

Zaburi 91:1. Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.

Mwili unalishwa kanisani lakini mwili huu hauwezi kufanya kazi vyema bila chakula ninachowapa kwenye mahali pa siri na kwa kutenga wakati wakunijua kwa undani. Hapa ndipo mwili unajengwa kikamilifu. Hapa ndipo nawasilisha mapenzi yangu na maneno yangu kwa kondoo wangu na kuwastahamilisha ndio waweze kupona adui anapowaletea shida.

Ni katika kuwa na uhusiano wa karibu sana nami ndio utakaokuwezesha kustahamili mitego na majaribio ya maisha. Ukijaribu kukabiliana na mambo haya peke yako utapambana na hatimaye ushindwe maanake haujui ninayohitaji ukiwa mbali nami na ilhali mwishowe mimi ndiye hakimu wa wote.

Utaweza je kukabiliana nami wakati wa hukumu ikiwa hujawahi kunikaribia na kujifunza matakwa yangu? Utakaponikabili bila husiano wa karibu nami utakuwa mikono mitupu maanake uliitegemea imani yako, fikira zako, mapenzi yako na utapungukiwa sana. Utakosea.

Warumi 14:12. Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.

Usidanganywe. Wengi wa hawa wanaojiita viongozi wangu hawana wakati nami, na hao pia hawatendi mapenzi yangu, na nikama kipofu akimwongoza kipofu kwa vichochorofunge vya uteketezi. Wengi watastaajabu jinsi walivyodanganywa kwa sababu waliwategemea watu wasionijua na wakadanganyika sana.

Huwezi kuweka imani yako kwa mambo ya dunia yanayoonekana kana kwamba ni ya ukweli. Lazima unitii.  

Niachie yote na unitafute kwa moyo wote. Hili ndilo jambo ninalohitaji.

Neno langu linanena juu ya ukweli huu. Lisome vyema na ujionee. Viongozi wangu wengi wanaupenda ulimwengu na mambo yake, kwa hivyo hao hulibadili neno langu ili wajihisi vyema wanapo changanyika na dunia. Dunia ni adui wangu. Lisome neno langu. Ukweli huu haujafichika. Huwezi kunipenda na pia upende dunia. Hatutangamani. Nimewaeleza kinaganaga kuhusu haya. Ni kweli, umo kwenye dunia lakini lazima unifuate na uzifuate njia zangu wakati ungalipo duniani.

Yakubu 4:4. Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.

Kuna vivuta mawazo kila uendapo ambavyo vinawaongoza watu na kuwafanya wasiwe na uhusiano wa ndani nami. Ni lazima muwe na tamaa ya kutaka kukaa nami kuliko vivuta mawazo vya dunia. Utakuwa unakubali kitu duni ikiwa utakimbilia mambo ya dunia kuliko kuwa na uhusiano na Muumba wa uhai wote – Muumba wako, Muumba wa nyota na mbingu.

Waebrania 10:38-39. Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; naye akisitasita, roho yangu haina furaha naye. Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.

Usibadilishane utukufu wa milele nami Muumba na Mwenye kupa riziki kwa uhai mwingine wo wote na raha duni upewazo na dunia. Unavyovifuata duniani ni vitu visivyo na maana ambavyo hatima yavyo ni kifo. Mnachagua hatima zenu, mnaziamini njia zenu, na kuamini kuwa ninabariki uamuzi wenu. Hamjanijua kwa karibu na undani. Mngalifanya hivyo, mngalijifunza tofauti. Mnadanganywa na njia za dunia na huyo adui wangu mjanja. Anawafanya mtende mambo mnayoamini ni mema bila mimi. Siwezi kubariki njia kama hizi. Kisha mnashangaa kwa nini mnapatwa na mateso mengi. Undanganyifu mkuu kutoka kwa adui wangu ni kule kuamini kuwa mambo yote ni shwari wakati unafuata ulimwengu bila uhusiano wa karibu na mimi. Huu ni udanganyifu mkuu kushinda zote. Yote yanaonekana sawa lakini wakati wa hukumu nitawaambia; siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.

Mathayo Mtakatifu 7:21. Si kila mtu aniambiaye Bwana, Bwana atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye Mbinguni. Wengi wataniambia siku ile Bwana, Bwana, hatakufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

Ndiyo, hili ni neno langu. Sikuwaumba ili mwende mbali nami na kujitafuatia njia zenu wenyewe bila kunishauri. Ndiyo, mnaweza kutenda haya yote maanake mna hiari, ila hamko kwenye hiari yangu na kwa hivyo mnatenda dhambi dhiidi yangu.

Nawapa wanangu hiari na wanaweza kuchagua kunitafuta kwa ndani na kuamini uongozi wangu au waweza kwenda mbali nami. Wanangu wanapoenda mbali name, nje ya mapenzi yangu, wakitafuta mipango yao wenyewe, wanatenda kazi dhidi ya mipango ya ufalme wangu, na huu ni uovu. Wana sababisha uharibifu wasiojua hata kidogo, kwa sababu wamejiamini kuwa wanaweza kuishi maisha yao nje ya mapenzi yangu mema na mipango yangu. Wanajiletea shida na kuwaletea wengine pia. Wanajiweka wazi kwa mitego na mipango ya adui. Wanangu, bila mimi, hamuwezi kushindana na ujanja na hila za adui wangu. Msijifikirie wenye busara sana. Ninyi ni bure bila mimi.

Mbona ninasema kuwa walio na imani kama ya mtoto ndio watakaourithi ufalme wangu? Ni kwa sababu wanatambua kuwa wananihitaji wakati wote jinsi mtoto anavyo mtazamia mzazi wakati wote. Mtoto anajua bila mzazi yumo hatarini. Hivyo ndivyo wanaangu wana tambua kuwa bila mimi watakuwa kwenye hatari kuu na kuamini kila neno ninenalo. Hii ndiyo maana nawasihi wanaangu wawe na muda kwa neno langu ambalo litawaelimisha.

Majibu kuhusu jinsi ya kuishi maisha haya yamo kitabuni mwangu. Niliwapa kitabu hiki kama kielekezi kwa wanadamu.

Roho wangu anaufichua ukweli katika kurasa hizi. Ni kwa kupitia kutii na kumpokea Roho wangu kwa kipimo kikamilifu ndipo utapokea utaalamu unaohitaji ili kuyaelewa maneno yangu kikweli. Sio kuwa kupitia mafunzo ya binadamu, bali kwa Roho wangu ndio maneno yanakua katika moyo wako. Ni kwa kupitia kwa Roho wangu tu ndipo utapokea uzima wenye nuru upatikanao kwenye kitabu changu.

Mathayo Mtakatifu 18:4. Basi yeyote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.

1 Wakorintho 2:11-14. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajwa tuliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu, maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.

Ulimwengu wa sasa umejaa udanganyifu. Msidanganywe na uovu unaokuzwa na adui wangu. Anataka muamini kupitia ujumbe mnaoupata kila siku kwamba mnaweza kuviamini vitu vya dunia. Mnaweka imani yenu kwa vitu vingine vyote isipokuwa Mimi, niwapaye uhai. Mnaweka imani yenu kwa pesa, elimu, usalama wa dunia, serikali. Huu ni msaada wa uongo. Huu ni udanganyifu wa hali ya juu na unawapeleka wanangu mbali nami. Wanangu wanaanza kuniamini kijuujuu. Wanakuja kwangu kidogo kisha wanategemea vitu vingine kuliko kunitegemea mimi. Huu sio uhusiano wa ndani.

Ndiyo, mna uhusiano wa ndani na dunia na matamanio yenu wenyewe. Lakini hamna uhusiano wa ndani nami. Mnatakiwa mnirudie na kuweka kila kitu mbele yangu. Hamuwezi kunijua kikweli hadi mtakapoweka kando usalama wa kidunia na kuja kwangu mkifuta uhusiano wa ndani. Chochote kile mbali na uhusiano wa aina hii ni uhusiano vuguvugu nami sitaheshimu uhusiano vuguvugu. Wengi watashangaa watakapokuja mbele yangu na kugundua kuwa kucheza dansi na dunia na kuwa na wakati mchache nami utawaweka nje ya ufalme wangu. Kutakuwa na wengi sana watakaoshikwa na mshangao.

Ufunuo wa Yohana 3:16. Basi, kwa sababu una uvuguvugu wala hu baridi wala si moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

Ni nini ninachotaka na kutarajia kutoka kwa wanangu? Nataka maisha yao. Nayataka yote kwa utiifu kamili. Ku dansi nami kisha unaenda na kudansi na ulimwengu ni uovu. Lisomeni neno langu. O! Wengi hulisoma neno langu na kuchukua maneno watakayo ili wajitulize ndio waendelee na raha za dunia huku wakijiona kuwa wataingia katika ufalme wangu maisha yao yaishapo. Utakuwa mshtuko ulioje kwa wale watakaogundua kuwa nawapokea wale tu waliojitolea kikamilifu kwa yote – waliojitolea mhanga. Ole wao watakapogundwa kuwa kumbe kule kufuata mali na umaarufu, ilikuwa kazi bure na iliwaweka nje ya ufalme wangu. Hiari yao na mipango yao ya siku zijazo iliwaongoza kwa njia iliyo mbali na mapenzi yangu na mipango yangu kamili kwa maisha yao – maisha niliyo wapa.

Ndio. Hakuna yeyote apumuaye siku kwa siku bila idhini yangu. Hii ndio maana wanangu wasiwe na uhakika sana juu ya mipango yao ya kibanafsi iliyo mbali na mapenzi yangu, na makusdio yangu ya kweli kwa maisha yao. Naweza kuuchukue uhai wo wote ule nitakao kwa hiari yangu. Hakuna aishiye kando na maamuzi yangu kwa maisha yao. Nawapa, nachukua kulingana na vile nionavyo bora. Ndio maana ni ujinga wakati wanadamu wanajiundia mipango yao nje ya mapenzi yangu kwa maisha yao. Ni kiburi na ujinga na ni uovu. Hii ndiyo njia adui wangu anayoitumia kuwaongoza kondoo wangu kwa njia potovu akitumia mambo yanayoonekana sawa na kawaida. Ni mpango wa adui wa kuwadanganya wengi.

Kitabu Cha Ayub 12:10. Ambaye nafsi ya kila kilicho hai i mkononi mwake, na pumzi zao wanadamu wote.

Zaburi 104:29. Wewe wauficha uso wako, wao wanafadhaika; waiondoa pumzi yao, wanakufa, na kuyarudia mavumbi yao. 

 

SURA YA 3: KUJIFUNZA UNYENYEKEVU

Binti, ni tayari kukupa maneno. Usikilize kwa makini ninapozungumza. Nataka kukupa taarifa mpya. Nataka kuzungumzia kuhusu kujifunza njia ya kuwa mnyenyekevu.

Hii ndiyo njia ya wanyenyekevu. Wenye moyo mpole na mtulivu ndio wanangu wanyenyekevu. Wanaenda kwa upole bila kutafuta cheo au marupurupu. Wananitafuta kwa njia zote. Kila kukicha wanamtafuta Mungu wao. Hawataki umaarufu.

Wanatamani tu kupendwa na kutunzwa nami, Mungu wao. Wananiamini nami nawatunza. Nakutana na matarajiyo yao. Nawatimizia haja zao. Nawaletea vyote wanavyohitaji maishani mwao. Mimi ni Mwamba wao.

Ni mwaminifu wakati wote kwa watumishi wangu wanyenyekevu. Nawaletea amani na utulivu kwenye dhoruba zote. Ni upande wao kila wakati; nakaa nao kila wakati, nawatumikia kila wakati. Nawapenda watumishi wangu wanyenyekevu. Hao ni harufu nzuri kwangu. Nawapenda nao wanipenda. Hatutenganishwi. Mimi ni hewa yao. Wanameremeta kama nyota. Hawatafuti njia za dunia. Nawatosheleza. Hawayumbiyumbi na mambo ya dunia. Wananitafuta ili niwatosheleze nami nawaletea vyote watamanivyo.

Hawaudhiki. Ni wachache sana wanao tembea kwenye njia hii. Niwachache sana wanaoipata njia hii. Wale waipatao, wanapata barabara ya kwenda kwa ufalme wangu wa milele.

1 Petero 5:6. Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake.

Watumishi wangu wanyenyekevu huisikiza sauti yangu. Wanasonga ninapowambia wasonge na wananitumikia wakati ninapowahitaji kwa mioyo yenye furaha: wanapenda kutumika katika ufalme wangu. Wanatosheka kumtumikia Mfalme wao nami nawaletea furaha na amani. 

Upendo wangu unabubujika juu yao. Hawakosi cho chote.

Ili uwe mnyenyekevu, huna budi kujiweka katika nafasi ya mwisho. Usiye hitaji nafasi ya kwanza.

Ni busara kuwa wa mwisho sio wa kwanza. Wajinga hutafuta nafasi ya kwanza. Watumishi wangu wanyenyekevu wana busara na wajua kinacho nipendeza mimi, Mungu wao.

Wanangu ni wale wanyenyekevu. Wale wasio fahamika duniani na wasioonekana, wamefichika mbali na wao wapendao dunia.

Hawana maana hapa duniani, lakini kwa ufalme wangu hao ndio watawalao na watamalakio. Wameinuliwa katika umiliki wangu mbinguni. Nawaheshima wanyenyekevu wangu. Wanaketi nami kwenye kiti changu cha enzi na kufurahia kuwepo kwangu. Wanyenyekevu wanaojiweka kwenye nafasi ya mwisho kwenye maisha haya, watafurahia cheo kwenye ufalme wangu. Wanainuliwa na kuwekwa kwenye utukufu kwa ajili ya kuishi maisha ya utiifu ulimwenguni. Hawa huniletea raha na niwapa amani, amani ya milele.

Marko Mtakatifu 10:31. Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na wa mwisho watakuwa wa kwanza.

Natembea na walio wanyenyekevu na kujitambulisha kwao. Hii ndiyo zawadi yangu kwa kujitolea mhanga kwao. Upendo wao kwangu ni harufu iliyonzuri na nitawaheshimu.

Unyenyekevu ndiyo njia ya ufalme wa Mungu. Kila aliye kwa ufalme wangu amejazwa na unyenyekevu. Kiburi hakiwezi kuinga kwenye ufalme wangu. Hakina nafasi kwenye ufalme wangu. Utiifu wa amani ndio ulio na nafasi katika ufalme wangu. Huu ndio ufalme, mwingi wa unyenyekevu na upole. Mahali ambapo kila mmoja anatosheka na upendo na uzuri unaofurika. Hakuna asiye tosheka na maisha yake mbinguni. Matumaini na amani ni tele. Ufalme wa mbinguni umefurika kwa upendo.

1 Yohana 2:16. Maana kila kilichomo duniani, yaani tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.

 

SURA YA 4: KUMWAMINI MUNGU

Natuanze binti yangu (Februari 7, 2012). Mwanangu, leo tutashughulikia jambo geni: Nataka kuzungumzia juu ya kumwamini Mungu. Wanangu hawaamini, wanasema wanaamini lakini mioyo yao i mbali nami, wanajiamini wenyewe. Huu ni uovu.

Wanaiamini dunia na vitu vya duniani. Hawatembei kwa njia yangu kwa maana hawaniamini. Wangaliniamini, wangalitembea kwenye njia yangu, kwa mapenzi yangu, na kwa njia zangu, kikamilifu. Wanatafuta pande zingine za kwenda. Wanaelekea kwa pande zingine. Wanatafuta majibu kutoka kwa dunia kupitia pesa, umaarufu, usalama, mapenzi na burudani… kila kitu isipokuwa Mimi, Mungu wao! Wajidanganya wasemapo wananiamini, ilhali wanatafuta majibu yao kutoka kwa ulimwengu. Uongo, yote ni uongo. “Mwamini Mungu” wanasema, lakini hawaniachii maisha yao na wanaendelea kukwamilia dunia wakitafuta majibu. Wanaishi kwenye uongo, wajidanganya na hawaoni.

Ndiyo, nawabariki wanangu kwa wingi. Nawanyeshea mvua na kuwaangazia jua kwa wema na waovu pamoja. Lakini wanangu hawaniamini na wanaendelea kufanya usherati na ulimwengu. Huku ni kukirihi. Natamani wana wanaoweka maisha yao chini yangu na kutii na kuniachia maisha yao nakuamini. Wana wanaoiweka mipango yao ya siku zijaazo kwangu na kuyaamini mapenzi yangu kwa ajili ya maisha yao. Wakiwa kwenye mapenzi yangu, hawataabiki wakijishughulisha na kuwa na wasiwasi juu ya kesho. Ninamjali shorewanda, sembuse wanangu wanaoniachia yote na kunitii kikamilifu kwa moyo wote?

Mathayo Mtakatifu 5:44-45. Lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombee wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni. Maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema; huwanyeshea mvua wenye haki na wasio na haki.

Zaburi 4:5. Toeni dhabihu za haki na kumtumaini Bwana.  

Mimi ni Mungu wa kuaminika. Hakuna mwamba mwingine. Mengine yote ni mchanga uzamao. Mimi Mungu adumuye milele. Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Naweza kuaminika. Mbona mnapoteza wakati mkisumbukia mipango yenu wenyewe? Hakuna ajuaye yajayo mbele hata kwenye saa moja ijayo. Mipango yenu yaweza kuharibika kwa kufumba na kufumbua macho. Mbona mnaikwamilia ni kana kwamba inaweza kuwaokoa? Kana kwamba ni ya kutegemewa? Hivyo ni kuabudu miungu wengine kweli!

Mathayo Mtakatifu 7:26. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga.

Acheni kuikwamilia hiyo mpango yenu dhaifu. Nipeeni maisha yenu yote. Mimi ndiye nijuaye yajayo. Mimi ndiye nijuaye mtakayofanya kesho.

Matumaini yenu na ndoto zenu nje ya mapenzi yangu yatawaelekeza kwa uteketezi kwa sababu wale walio kwenye mapenzi yangu, wanaonitegemea kwa kila kitu ndio walio salama, salama kweli. Wengine wote wanatembea mbali na mapenzi yangu wakiniasi kwa hivyo hawawezi kwenda mbele na kuwa salama. Hili ni jambo la kusikitisha sana wanangu.

Amkeni na muache kuziamini njia zenu za uasi na muniamini mimi Mungu wenu. Mimi ndiye nijuaye kwenye njia ile nyembamba. Msihadaike mkidhani mwaweza kuipata njia hii bila mimi… huo ni ujinga. Wachache wanaipata njia hii kwa sababu ni wachache sana wanaoacha kuzishikilia njia zao wenyewe. Wale wengine wanadhani njia zao ni mwafaka kwa sababu kila mtu anazifuata, lakini njia ya jehanamu ni pana! Msiwaamini hao wengi wanaowazunguka na hali wamepotea pia. Hamuoni? Ni nini msichokielewa kuhusu haya wanangu?

Mathayo Mtakatifu 7:13-14. Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni pana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi wauingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.

Kwa hivyo, niaminini mimi. Naaminika. Maneno yangu hayakosi kutimia. Kisomeni kitabu changu. Nawakomboa wale ambao wanataka ukombozi. Mimi ni Mungu awakomboao wajitoleao kwangu kikamilifu kwa mioyo iliyovunjika. Kwa hivyo, njooni mkombolewe na mjifunze kuniamini mimi Mungu wenu.

 

SURA YA 5: MSAMAHA

Natuanze tena (Februari 7, 2012). Sasa nataka kuzungumzia kuhusu “Msamaha.” Wanangu, nataka kuzungumzia juu ya jambo hili la msamaha. Wanangu hawana msamaha mioyoni mwao. Wanaweka malalamishi juu ya wengine mioyoni mwao. Siwezi kuwasamehe wasiosamehe. Mnanielewa? Nitawezaje kukusamehe ikiwa hutowasamehe waliokukosea? Je, neno langu halizungumzii haya? Msamaha ni upendo. Kutosamehe kunaleta dhambi zingine nyingi: Uchungu, kulipiza kisasi, hukumu zisizo za kweli na kadhalika. Inampa adui njia ya kuingia ndani na kuwaangamiza. Hii inafanya msiwe na uhusiano wa ndani nami Mungu wenu, na kuwafanya msimpokee Roho wangu. Hili ni kosa kubwa.

Mathayo Mtakatifu 6:14-15. Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba wenu wa mbinguni atawasamehe nyinyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawa samehe nyinyi makosa yenu.

Ikiwa hauna msamaha kwa wengine, hautakuwa tayari nirudipo. Itatutenganisha. Hautakwenda nami. Achaneni na mambo ya kutosameheana nyuma. Sameheana. Achaneni na hasira mlizo nazo kwa wenzenu. Unafaidika na nini unapomkasirikia mwenzako? Unateseka zaidi kuliko yule uliyemkasirikia. Hauoni haya? Wokovu wenu wa milele una thamani sana kuliko hasira.

Marko Mtakatifu 11:25. Nanyi kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na baba yenu aliye mbinguni awasamehe na nyinyi makosa yenu.

Ichunguzeni mioyo yenu na mjiulize swali hili: Ni lipi la maana sana kukupotezea uzima wako wa milele… kosa ndogo tu? Samehe na uende na uone wingu jeusi likiondoka. Hata kama yule ambaye umemsamehe hatakusamehe, mwombee. Ndiyo, waombeeni maadui zenu. Waombeeni na mioyo mikunjufu na nitaifanya mioyo yenu iwapende wote wanaotaka kuwaumiza. Nitawapa mioyo ya nyama. Itakuwaje mnatarajia watu wasiotembea kwa mapenzi yangu na wasio na Roho Mtakatifu wangu wawe wema kwenu? Lazima muwe watulivu, wakarimu, na wenye huruma kwa watu wasionijua mimi. Ni vigumu sana kwa watu wasionijua, wale wasionijua kwa kweli wawatendee kama wale wanijuao. Hamuoni? Msiwatarajie watu wasio na uhusiano wa ndani nami kuwatendea mema.

Mathayo Mtakatifu 5:44-45. Lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa baba yenu aliye mbinguni. Maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

Dunia inadhani inaweza kuendelea bila mimi Mungu wake. Inajidanganya. Mimi pekee ndiye ninayeshikilia kila kitu pamoja. Mimi ndiye niletaye njia ya ukweli ya kuishi kwa wanadamu. Dunia hii, inayonitenga, inaishi kwenye mwelekeo wa uongo. Imekuwa na uovu tele.

Hakuna ukweli. Ni maafikiano na ulaghai. Mbali na mienendo yangu minyoofu, binadamu huishi kwenye ulaghai na upotovu. Hakuna yeyote anayeaminika au chochote kinachoaminika. Bi arusi wangu pekee, anayebaki ardhini, na kutembea kwa mapenzi yangu, ndiye aliye kwenye njia nyoofu. Yeye tu ndiye dhabiti na wa kweli. Wengine wote wanatembea kwenye njia isiyoaminika na ya uovu, kwa kila jambo.

Msamaha: Huu ndio ufunguo wa kukufungulia njia ya kurudi kwangu. Msamehe kila mtu. Hakuna kutosamehe ko kote kunaolingana na kupoteza nafasi yako milele.

Luka Mtakatifu 6:37. Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni nanyi mtaachiliwa.

Binti yangu, huyu ni Bwana Mungu wako, anayenena nawe. Natuanze, sasa nataka kuwafundisha jinsi ya kuishi na wengine. Wengi wanadharauliana. Hawana utulivu, na heshima. Yote haya yanasababisha ugomvi. Inawafanya wasitosheke na kuleta kuumizana mioyo. Wanangu wana ubinafsi. Wanataka wawe wa kwanza kwa kila jambo. Hawayatilii maanani matakwa ya wengine.

Hawawajali wenzao. Hii inasababisha hasira na mabishano. Wanangu, nina huzunishwa sana na haya. Chanzo cha shida hii ni ubinafsi. Na hii ni kwa sababu ya ukosefu wa unyenyekevu.

Mithali 15:33. Kumcha BWANA ni maonyo ya hekima. Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.

Mwenye moyo mnyenyekevu ndiye atakaye weza kuishi na wengine vyema. Lazima mziache tamaa zenu na kuwajali walio karibu nanyi ndio watosheke. Mtahitaji kuchukwa nafasi ya nyuma. Hii ndio njia ya unyenyekevu. Na hii huzaa matunda ya amani, kutosheka na hali nzuri.Wachache sana hujifunza kuishi hivi. Wachache sana huupata ukweli huu. Lakini hii ndiyo njia ya amani, njia yangu. Nawapa sheria hizi za maisha ili ninyi waanangu mwishi kwa amani na kutosheka. Wengi wenu mnakataa kuzifuata kisha mnakuwa na ugomvi na kutotosheka. Mtajifunza lini kuwa njia yangu ndiyo njia njema ya kusafiria? Ninajua kila kitu. Ninajua jinsi wanangu wanaweza kuishi pamoja. Nawapa sheria na kanuni za kuwaongoza kwa nyumba zilizo na amani. Mnahitajika kunifuata na kuziacha njia zenu ili mzifuate sheria zangu.

Zaburi 34:14. Uache mabaya ukatende mema, utafute amani ukaifuatie.

Tukichagua ubinafsi nyumba zetu zitakosa raha. Niacheni nitawale juu ya nyumba zenu. Niacheni nitawale ndani ya mioyo yenu. Njia yangu ni tulivu, yenye amani, upendo. Nitazifanya nyumba zenu ziwe makao yenye raha kama nilivyowatakia tangu mwanzo. Nipeni mioyo yenu kwa hiari yenu nami nitawanyeshea utulivu. Kaya zenu zitakuwa na uhakika, upendo na amani. Tembeeni kwenye njia za kutosheka, unyenyekevu, na kuwajali wengine ili mzae matunda ya kutosheka. Niacheni nitawale juu ya kaya zenu, na nitawapa maskani yenye raha na furaha.

Zaburi 37:11. Bali wenye upole watairidhi nchi, watajifurahisha kwa wingi wa amani.

 

 

SURA YA 6: ISHINI DUNIANI, BALI MSIWE “WA DUNIA”

Natuanze. Leo ninataka kuzungumzia juu ya kuishi duniani. Waanangu wanaishi duniani, bali si lazima wawe “wa dunia”! Dunia ni adui wangu. Nimechukizwa na uovu wake mkuu.

Wanangu, mnaweza kutembea kati ya watu wa dunia bila kushiriki kwenye vitu vya dunia. Dunia itawaongoza kwa njia za upotevu na kuumwa moyo.

Yakobo 4:4. Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.

Mimi ndicho chanzo cha ukamilifu, amani, na utulivu. Msigeukie dunia ili iwape mwelekeo wa maisha yenu. Mtapotoshwa. Ni sharti mnijie mimi niwape mwelekeo. Nishikilieni wakati huu ambao ni muhimu. Nina majibu ya maswali yenu yote.

Ninataka kuwaondolea dhiki na mashaka ila ni lazima mnipe maisha yenu yote. Mkifanya hivyo nitayachukua maisha yenu na kuwakomboa.

Mnaweza kutembea duniani kwa usalama bila ya kuathiriwa na tamaa za duniani, ila mnanihitaji nitembee nanyi. Naweza kuwaongoza mpite kwenye mivuto ya dunia inayoweza kuwa potosha na kuwavuta mbali nami.

Nataka mnitazamie mimi. Myaweke macho yenu kwangu, Mwokozi wenu. Mimi ndiye mlango utakao wapeleka mahali salama. Milango nyingine yote itawepeleka kwa maangamio. Msidanganywe na kuyatoa macho yenu kwangu. Nawapa tumaini kwa dunia hii isiyo na matumaini.

Ooh! Inaonekana kuwa na matumaini, bali kinachoonekana kama kawaida ni udanganyifu.  

Zaburi 25:15. Macho yangu humwelekea BWANA daima. Naye atanitoa miguu yangu katika wavu.

Hizi ni saa za mwisho. Dunia i katika enzi za mwisho. Dunia inakaa kawaida lakini sivyo. Inaelekea kuteketea. Wengi watagundua haya lakini watakuwa wamechelewa. Fungueni macho yenu. Dunia inawapa matumani ya uongo.

Niacheni niwaongoze. Nipeni maisha yenu. Nitayafungua macho yenu kupitia kwa Roho Mtakatifu wangu na mtafanywa upya na kuyaona mambo jinsi yalivyo ndipo mtakapo uona ukweli. Roho Mtakatifu pekee ndiye anayeweza kuyafungua macho yenu ya kiroho ili muone dunia inavyowadanganya. Ni tayari kuwapa marhamu ya roho ili iwasaidie kubadilika. Mnaweza kuniuliza nami nitawapa. Nipeni mioyo, roho na nafsi na maisha yenu nami niwape macho mnayohitaji ili kutembea salama duniani.

Ufunuo wa Yohana 3:18. Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako upate kuona.

 

SURA YA 7: UNYAKUO NA KARAMU YA ARUSI YA MWANA KONDOO

Natuanze. Haya maneno ni kwa yeyote yule atakaye yapokea. Leo nitazungumzia kuhusu unyakuo ujao na kuondoka kwa bi arusi wangu, Kanisa langu.

Huu wakati unakaribia kwa upesi. Wanangu wengi hawako tayari. Wananipinga na kukwamilia kwa dunia. Wanataka kutembea kwenye njia za dunia. Wanakimbia hapa na pale na hawasikii maonyo niwapayo. Hivi karibuni nitaacha kuwaonya kisha nije na bi arusi ataondolewa. Atatolewa kabisa hapa duniani.

Danieli 12:4. Lakini wewe, ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huku na huko, na maarifa yataongezeka.

Hatambuliki duniani. Amefichwa. Nimemweka utawani kwa usalama. Nuru yangu inaangaza kupitia kwake – Nuru ya mwisho ambayo imebaki duniani. Muda ni mfupi na hivi karibuni nuru hii itazimika. Watumwa wangu wataondoka kwenda kwa makao yao ya usalama mbinguni wauache huu ulimwengu wa udhalimu.

Unyakuo huu utakuwa tukio kubwa. Kuondolewa kwa wanangu walio tayari. Hakutakuwa na tukio lingine kubwa kama hili kwenye historia ya binadanu. Hakutakuwa na jambo jingine kama hili, kabla na badaye. Huku ndiko “Kutoka” kukuu.

Wanangu wataondoka mara moja na kupokea miili mitukufu. Miili hii itakuwa thabiti na ya milele. Itakuwa kama mwili wangu mtukufu. Mimi ndiye limbuko kwa wengine wengi. Hawa wana watakuwa na maisha ambayo hawajawahi kuwa nayo mbeleni. Maisha matukufu, uzima wa milele.

1 Wakorintho 15:51-54. Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tatabadilika kwa dakika moja. Kufumbua na kufumbua wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia na wafu watafufuliwa wasiwe na uharibifu nasi tutabadilika. Maana sharti huu uharibikao uvae kutoharibika nao huu wa kufa uvae kutokufa. Basi huu uharibikao utakapovaa kutoharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, mauti imemezwa kwa kushindwa.

Kutakuwa na vitu vingi vyema sana mbele kwa wanangu watakaonyakuliwa. Acheni niwaonyeshe kidogo tu vile itavyokuwa: Wanangu watakapofika, watalakiwa na wapendwa wao: familia na marafiki wale tayari wako mbinguni. Nitakuwa nikiwatazama. Huu utakuwa wakati wa utukufu mkuu. Ni tunu ilioje kuungana na familia ulioikosa muda mrefu! Kisha wanangu watapelekwa hadi kwenye karamu ya arusi ya Mwana Kondoo. Nitawaongoza kwenye karamu hii.

Ufunuo wa Yohana 19:9. Naye akaniambia, Andika Heri walioalikwa kwa karamu ya arusi ya Mwana Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.

Meza itaandaliwa kwa vitu tele. Vikorokoro vyote vitakuwako. Kila jambo kuhusu karamu hii litakuwa la kuwastaajabisha. Wanangu watakaa katika sehemu iliyoandaliwa kila mmoja wao na majina yao yatakuwa yameandikwa kwenye sehemu hiyo kwa dhahabu. Vyombo vyote vitakuwa vya dhahabu vilivyopambwa na vito. Kitambaa cha mezani kutakuwa cha hariri, na nyuzi za dhahabu. Nuru itang’aa na vikombe vyote vitakuwa vya dhahabu vilivyolainishwa na vito ukingoni.

Kutakuwa na zawadi kwa kila mmoja pahali watakapoketi. Zawadi hii itakuwa ni kumbusho la uhusiano wangu na huyo mwanangu. Kila zawadi itatofautiana na nyingine. Kila zawadi itakuwa na maana yake kwa kila mwana kuonyesa uhusiano wangu naye. Kutakuwa na vitu vingi vya kustaajabisha siku hiyo – siku ya karamu ya arusi yangu.

Mathayo Mtakatifu 22:2. Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi.

Kila mwana atakuwa na malaika wa kumshughulikia. Chakula kinatengenezwa kwenye jikoni zangu za mbinguni. Hakuna kitakachokosekana. Vyakula vyote vitakuwa vya kipimo cha mbinguni. Kutakuwa na vyakula muvijuavyo kutoka kwenye ardhi na pia vya mbinguni ambavyo hamjawahi kuviona. Kutakuwa na uzuri usio kifani.

Meza yangu itajaa mwangaza: Mishuma na Menorah (kinara cha taa saba). Wanangu watavaa kanzu za mianga. Watatoa mianga na hakutakuwa na vivuli.

Waraka wa Yakobo 1:17. Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Bwana wa mianga; kwake hakuna kubadilika wala kivuli cha kugeukageuka.

Nitaongoza kwa kumpongeza bi arusi wangu. Nitaimba sifa zake kwa maana yeye ni mrembo kwangu. Kutakuwa na muziki na dansi na furaha kila mahali.

Bi arusi ataniona kwenye utukufu wangu wote. Kwa maana nitakuwa ninang’ara ajabu. Uzuri wangu utang’aa kila mahali na upendo wangu utatiririka kwa wote ambao watashiriki kwenye karamu hii. Babangu atakuwa akitutazama kwa furaha na raha kuu kwa maana kutakuwa na kucheza na furaha tele.

Nitacheza dansi na bi arusi wangu na tutakuwa kama kitu kimoja. Wanangu watacheza na kufurahia. Mioyo yote itakuwa yenye furaha. Hakuna atakayekuwa na huzuni. Huu utakuwa wakati mukuu wa utukufu na upendo.

Njiwa watajaa hewani. Watapaa kwenye mapambo na kuumba mipangilio iliyo na ujumbe kwa bi arusi wangu hewani. Bi arusi atashikwa na bumbwazi. Nitampa bi arusi wangu pete. Majina yetu yatakuwa yameandikwa kwenye pete hizi. Maua ya kila aina na rangi yatakuwa kila pahali. Rangi mpya na rangi nzee. Harufu nzuri itajaa hewani. Wanangu watafurahia mno.

Luka 15:22. Lakini baba aliwaambia watumwa wake, lileteni upesi vazi lililo bora mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni.  

Malaika wangu watajaza mbinguni na nyimbo, kucheza na muziki. Vifaa vya muziki vya mbinguni vitacheza muziki mzuri. Hata nyota zitaimba zikisherekea Mwana Kondoo na bi arusi wake.

Ayubu 38:6-7. Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni, Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?

Majeshi yote ya mbinguni yatakusanyika na kuimba sifa kwa bi arusi wa Mwana-Kondoo. Kila mmoja ataimba sifa kwa Mfalme, bi arusi wake yuaja. Amejiweka tayari. Furaha na ianze!

Ufunuo wa Yohana 19:7. Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana Kondoo imekuja na mkewe amejiweka tayari. Mwana Kondoo aichukuaye dhambi ya dunia ameungana na mpendwa wake kwa ndoa takatifu. Jina lake ni kuu! Lisifuni jina lake takatifu kati ya mbinguni zote kwa maana amemchumbia mpendwa wake naye amempa moyo wake!

Yohana 1:29. Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!

Wanangu pia wataonyeshwa makao yao. O! binti, ni uzuri, ni fahari. Hakuna jicho ambalo limeona wala sikio ambalo limesikia aliyoandaliwa bi arusi wangu mtukufu anipendaye.

1 Wakorintho 2:9. Lakini kama ilivyoandikwa mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.

Binti, makao haya yatakuwa yakupendeza sana kuliko chochote kile ulimwengu unaweza kuwapa. Hakuna cha kulinganisha na yote yale nimemwandalia bi arusi wangu. Makao hayo yatamfaa kila mwana. Hakuna makao yatakayofanana. Kila nyumba itakuwa tofauti na nyingine.

Yohana Mtakatifu 14:2-3. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia, maana naendea kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.

Wanangu wataduwazwa na kile watakachokipata kwa kila nyumba. Kila nyumba ina vitu vitakavyompendeza na kumfurahisha mwenyewe. Hakuna kitu ardhini kinachoweza kueleza mapambo na uzuri wa kila moja ya nyumba hizi. Tutashiriki pamoja. Tutacheka na kutalii pamoja. Msisimuko hautakwisha.

Kutakuwa na bustani na starehe kokote. Muziki utajaa hewani na harufu nzuri. Kila nyumba itajaa vicheko na mapenzi. Hakutakuwa na ukiwa mbinguni. Ni pamoja na wanangu kila mara tukifurahia na kukaa pamoja.

Zaburi 36:8. Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako, Nawe utawanywesha mto wa furaha zako.

Upendo wangu utawazunguka kote. Kicheko, upendo na furaha ndio tuzo ya hizi nyumba za kudumu milele. Furaha isiyo kifani, raha idumuyo milele.

Hiki ni kionjo tu cha yale yajayo. Wanangu hawana ufahamu kuhusu yale niliyowaandalia. Hakuna vile niwezavyo kuwaelezea yaliyo juu mbiguni kikamilifu. Kuweko na kushuhudia pekee ndiko kutaweza kuwapa picha kamili.

Kwa hivyo wanangu, njooni mfurahie uzuri wa mbinguni kwenye ufalme udumuo milele na nyumba zilizotenganezwa kwa upendo za bi arusi wangu.

Zaburi 16:11. Utanijulisha njia ya uzima; mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume, mna mema ya milele.

 

 

SURA YA 8: JITAYARISHENI KWA UNYAKUO

Natuanze. Sasa binti, siku zijazo kabla ya unyakuo, kuna mengi yakutayarisha. Wanangu wanafaa wawe na muda nami katika mahali pa siri. Muda wa utulivu, ili waweze kunijua. Nawahitaji kwa pamoja nami. Ningependa kuwaelezea yaliyo moyoni mwangu. Nataka wanipe mioyo yao kikamilifu, maisha yao na vyote vile wamevishikilia hapa duniani.

Zaburi 91:1. Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu, atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.

Wanangu wameushikilia ulimwengu. Wanaamini kuwa ulimwengu utawapa kila kitu. Ulimwengu ni mtupu na wenye moyo baridi. Kila mtu kibinafsi. Hakuna amjaliye mwenziwe. Imekuwa hali ya unyang’au. Kila mmjoa anamfuata mwenziwe kusudi apate kile anachotaka kwake na kujitosheleza binafsi. Ni ulimwengu usio na matumaini na wa taabu nyingi. Na wanangu wangali wanaushikilia wakiamini utawapa watakayo. Wanapumbazwa na waliopotea ambao wanaeneza njia zao potovu. Wanangu wanafaa wajiondoe kwenye upuuzi huu na wanirudie mimi Mungu Aishiye, Muumba wao, aliye na majibu yote ya maisha ya sasa na yajayo.

Mimi ndiye Mungu Mkuu wa vyote viishivyo na roho zote zinazopumua. Nina funguo za uzima wa milele. Jisalimisheni, kwangu nijapo kuja duniani, nimchukue bi arusi wangu na kuwaondokea ili ulimwengu upokee hukumu yake.

Ayubu 12:10. Ambaye nafsi ya kila kilicho hai i mkononi mwake, na pumzi zao wanadamu wote.

Haya yote yatatendeka hivi karibuni. Kusalimu amri ndiko kunakohitajika ili muwe kati ya bi arusi wangu; wanangu nitakaowaokoa. Hakuna lingine. Mnitii kwa kila jambo na mwache nitawale kila sehemu ya maisha yenu ndipo roho wangu atakuja kwa roho zenu na kuwafanya upya na kuisafisha mioyo yenu kwa kuifunika kwa damu yangu iliyotoa fidia na uongofu kupitia kwa neno langu. Hii ni muhimu ili kuzikomboa nafsi zenu ili ziwe bila doa, ziwe safi na tayari kwa unyakuo, kupelekwa mahali salama. Ikiwa mna mashaka au tashwishi yoyote, lisomeni neno langu!

Waefeso 5:25-27. Enyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akijitoa kwa ajili yake; ili maksudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.

Ombeni ili mjazwe na Roho Mtakatifu. Tubuni dhambi zenu. Anzeni kufunga ili kuonyesha majuto kwa dhambi zenu ambazo mumezileta mbele yangu, mimi Mungu aliye Mtakatifu. Nitawajaza tena. Nitawaongoza kwa ukweli wa milele katika njia zangu na mapenzi yangu.

Hiari zenu wenyewe zitawapeleka kwenye upotovu. Hii ndiyo njia pana ambayo neno langu linazungumzia. Njooni kwenye mapenzi yangu. Hii ndiyo njia nyembamba, njia iliyo salama na nitawapeleka kwa hiyo njia.

Mathayo Mtakatifu 7:13-14. Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, nayo njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.

Neno langu litawaongoza kwa njia yenye nuru. Njia zingine zote zinaelekea kwenye upotovu wa milele. Njooni kwenye nuru yangu na kwa mapenzi yangu. Nipeni uzima wenu. Niacheni niziondoe dhambi zenu mlizotenda na niwaonyeshe njia itakayowaongoza kwa uhuru ikiwatoa kwa utumwa wa dhambi.

Zaburi 119:105. Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu.

Hata liweje, dhambi hukuweka utumwani, na kukufanya mtumwa wa dhambi. Naweza kuwaweka huru, bali ni lazima mjisalimishe kwangu, mtubu, na kukubali kuwa ninyi ni wenye dhambi na mnataka kuwekwa huru na mfanye hivyo kwa moyo uliojuta na ulio mnyofu. Nitafurahia kuwaweka huru kutoka kwa dhambi ambazo zinawafunga na kuwafanya watumwa. Mimi ninaweza kuwaweka huru kutoka kwa cho chote kile kinacho wafanya kuwa wafungwa.

Hamna jambo nisiloliweza. Hamna! Nilikuja kwa ajili ya wafungwa waliofungwa! Mnachohitaji kufanya ni kuniuliza tu, nami nitawaweka huru!

Luka Mtakatifu 1:37. Kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.

Niacheni niwaondolee mzigo huu. Niacheni niwaondolee huzuni na simanzi. Niacheni niwaliwaze na kuichukwa mizigo yenu. Niacheni niwatayarishe kwa kurudi kwangu kutukufu! Yote haya ni yenu -- jitoleeni, wekani kando matamanio yenu yote ya kilimwengu na mje kwangu kwa kujitolea kikamilifu. Nitawapa amani ipitayo akili zote na mtakuwa sawa mbele zangu. Mtakuwa bila hukumu mbele yangu, mbele ya Baba na mbele ya Roho Mtakatifu.

Wafilipi 4:7. Na amani ya Mungu,ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

Upendo huu hawezi kununuliwa --- ni wa bure --- bure kwenu kuupokea – bure kwenu mkiuliza. Harakisheni kwa maana ni wa muda mfupi. Nakaribia kurudi, msichelewe. Wakati wa kuoshwa na damu yangu ni huu. Jitayarishe.

1 Yohana 1:7. Bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisisha dhambi yote.

Natuanze, binti. Leo nataka kuzungumzia juu ya wale watakaoachua wakati wa unyakuo.

Baada ya unyakuo, dunia haitakuwa sawa tena. Kutakuwa na mageuzi makubwa mahali pote. Dunia haitakuwa sawa tena. Hofu kuu itakuwa duniani. Wanangu walio vuguvugu wataelewa kile ambacho kimetendeka na hofu, hofu kuu, itawaingia moyoni.

Dunia haitatenda mambo kama kawaida. Hata ya nchi itageuka. Kutakuwa na mioto na majanga makuu mahali pote. Watu watakuwa bila ulinzi kwa sababu vikundi vya watu wenye ghasia watakuwa wakitembea pote wakitafuta watu wakuvamia na kuwanyang’anya walivyo navyo. Hakutakuwa na askari au polisi wa kuwasaidia kwa maana kutakuwa na vurugu.

Wengi watayapoteza maisha yao kwa sababu uharibifu wa ghafula utaikumba dunia. Mahali pote duniani hapatakuwa sawa tena kwa maana watu wengi wataangamia mara moja.

1 Wathesalonike 5:3. Wakati wasemapo, kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.

Hofu kubwa itawangia watu kote duniani. Hakutakuwa na pahali pa usalama pakwenda. Hakutakuwa na chakula. Watu watakata tamaa. Haya yataendelea kwa muda fulani ndipo mpinga Kristo ataingia na kuiweka dunia nzima chini ya mamlaka yake.

Mwanzoni, watu wataona kama ni jambo njema kwa sababu dunia itatulia, ila utulivu anaouleta utakuwa ni kifo kwa wengi. Watakaokataa mfumo wake wata uawa, na wengi watateswa na kusumbuliwa. Kuukata mfumo huu hakutakuwa kwema kwa maana hatamvumilia yeyote. Yeye ni muovu kabisa. Atauweka ulimwengu wote chini ya utawala wake wa udhalimu. Nchi zote zitamfuata kwa kutaka kuweko kwa mpangilio baada ya machafuko yaliyoachwa na unyakuo.

Huu utakuwa wakati wa huzuni kwa ulimwengu wote. Wengi watajiua wakitafuta kuepuka. Huu hautakuwa utatuzi kwa hivyo mtu ye yote asifikirie hata kuyachukua maisha yake.

Mpinga Kristo ataweka chapa ya mnyama kama njia ya kuwatawala -- kuikataa chapa au alama kutakuhukumia kifo. Hakuna atakayeachwa.

Ufunuo wa Yohana 13:16-17. Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kiume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.

Ufunuo wa Yohana 14:11. Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.

Wafuasi wangu wengi walio vugurugu sasa wataelewa gharama ambayo ni sharti walipe ili waingie kwenye ufalme wangu. Wengi hawatamtii mpinga Kristo na kwa hivyo wengi watakufa kwa ajili ya imani yao. Watakuwa wengi.

Haijalishi ni wangapi watakaokufa kwa Mpinga Kristo. Tamaa yake ya kutaka kutawala itakuwa moyoni mwake. Hatajalii kuhusu wale watakaopoteza maisha yao. Utakuwa ni wakati mgumu kwa wale wanaolikiri jina langu. Ni wakati mgumu sana unaokaribia wanangu! Kumekuweko na nyakati ngumu ulimwenguni hapo nyuma bali huu wakati utakuwa mgumu zaidi. Hapa hapatakuwa pahali pema kwa aliye na watoto. Giza litatawala. Haya ndiyo yatakayolikumba kanisa langu vuguvugu.

Makanisa vuguvugu yatanirudia kwa wingi -- watu watanitafuta sana. Nitakuwepo bali lazima wapitie wakati mgumu. Familia zitatenganishwa na huzuni utatanda. Haya yote yatatokea kwa maana wanangu wamekuwa na mioyo migumu na kukataa kusikiliza maonyo ambayo nawapa kila siku. Haya yote yanaweza kuepukwa ikiwa wanangu watakuja kwangu, wanililie kwa mioyo minyenyekevu, watubu dhambi zao na kuutafuta uso wangu. Wajifunze kunijia kwa uhusiano wa karibu. Kimbieni mje kwa mikono yangu iliyo wazi kuwapokea. Nitawaonyesha ukweli kuhusu kurudi kwangu hivi karibuni na jinsi ya kujitayarisha kama bi arusi.

Njooni wanangu. Kimbieni. Nawasubiri ili niwaokoe kutoka kwa haya yote. Mimi ndiye muokoaji mkuu. Tamaa yangu ni kuwaokoa. Hakuna haja muachwe nyuma. Kuna nafasi kwa ye yote yule atakayekuja na kunitolea maisha yake. Nahitaji kujitolewa kwako kikamilifu na kutubu dhambi zako. Msidanganywe. Hakuna haja muachwe nyuma. Kuna nafasi kwa ye yote yule atakayekuja na kunitolea maisha yake. Nahitaji kujitolea kwenu kikamilifu na kutubu dhambi zenu. Msidanganywe. Hakuna njia nyingine. Niacheni niwaletee utulivu wakati wa unyakuo.

Natuanze tena. Wanangu wanadhani wana miaka mingi sana huko mbele. Hawaelewi kuwa nimechoshwa na huu ulimwengu.

Wanangu wameshikwa na dunia sana hata hawaoni jinsi dunia ilivyo mbali na ukweli ambao mimi Mungu nasimamia. Hata makanisa yao ya mbali na neno langu, ukweli wangu, kitabu changu. Viongozi wa makundi yangu wanajishughulisha na mambo ya dunia na wanaifanya kazi yangu kujifurahisha wenyewe. Hawana upendo kwangu. Wanafuata mali, umaarufu na kukubaliwa na walio wazunguka kisha wanaamini nita wabariki.

Wanaamini kuwa wingi wa watu makanisani mwao ndio kuonyesha kuwa wamefaulu na kwamba napendezwa na hayo. Ninapendezwa tu ikiwa viongozi wangu wanawaelekeza wafuasi wao kunitafuta mimi kwanza katika njia zao na kutembea nami katika uhusiano mtulivu. Ni wachache sana wanohuburi haya kwa sababu hawataki kuwaudhi wengi wanaowataka waje kwa makanisa yao. Wengi wanaleta pesa na pesa zinafanya kila mmoja afurahi bali ufalme wangu siowa utajiri katika maisha ya sasa.

Luka Mtakatifu 16:13. Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili, kwa maana ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.

Viongozi wangu wa mbali nami. Na mbona wasiwe? Ikiwa wanataka kuwafurahisha, muda wao nami utatoka wapi? Wanaishi kwa sababu yangu! Mimi ndiye niletaye jua na mvua.

Huu ni wakati wa giza na giza linaendelea kuwa kubwa kila siku, ilhali viongozi wangu wanaendelea kuuficha ukweli huu kutoka kwa makundi yangu. Wanaficha ukweli nakuwaletea maneno ya furaha na raha. Makundi yangu yanadanganywa na hayatayarishwi. Wanadhani mambo yote ni sawa na wanaendelea kuishi maisha yao kama kawaida.

Ni maonyo yapi nitakayowapa ili niwaamshe? Ni lipi wanalotaka kusika ndipo wakiamini kitabu changu ambacho kimewapa ukweli? Hakuna asikiaye wala aminiye. Ni yapi yatakayosemwa kwa kanisa ili wayasikie maonyo na kuziweka kando tamaa zao za vitu vya dunia ili wakeshe na kujitayarisha?

Hosea 4:6. Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi, kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.

Wamekuwa wapole na wanapotoshwa. Muda unayoyoma nalo kanisa linabaki limeridhika tu kana kwamba kila kitu ki sawasawa. Kanisa vuguvugu limedanganywa -- linanifuata bila uhai. Kanisa lingalinifuata na kuwa na uhusiano wa ndani nami, basi maonyo niwapayo hayangalikuwa mageni kwao na wangaliyafuata kwa moyo wote.

Huu ni wakati wa giza kuu kwa makanisa. Machache sana yanaelewa. Ni machache sana yanayotembea kwa njia zangu na maadili yangu. Neema haitapewa wale wanao asi kwa hiari, na wanao kataa kutubu. Mnamuhuzunisha Roho Mtakatifu wangu kisha mtafanya nini kanisa?

Waefeso 4:30. Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.

Mnapomfukuza Roho Mtakatifu wangu kutoka kwa hayo majumba yenu ya fahari eti kwa sababu amezidi kupita kiasi kumbukeni mimi na Roho wangu tu kitu kimoja. Mnamuabudu nani ikiwa mumemfukuza Roho Mtakatifu wangu kutoka mahali mlipo? Niambieni ni nani mnaye muabudu? Mnaabudu miungu wengine!

Matendo ya Mitume 7:51. Enyi wenye shingo ngumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, siku zote mnampinga Roho Mtakatifu; baba zenu walivyofanya, na nanyi ni vivyo hivyo.

Mumejiumbia Mungu wenu wenyewe. Mungu anayefaa tamaa zenu za kilimwengu, bali siyo Mungu mmoja aishiye milele. Ni kijimungu. Mwadhani kuwa wale watu wa zamani walioabudu sanamu za dhahabu walinikashifu sana. Nanyi vile vile hamna tofauti nao! Njooni kwangu mkinyenyekea kwa toba makanisa nami nitaziosha nafsi zenu. Nitawasamehe dhambi zenu za kuniacha na kukimbilia mali. Natamani kuwarudisheni, kwangu. Niacheni niwaamshe na kuwaletea amani na kuwaweka sawa na Mungu wenu.

Marko Mtakatifu 8:36. Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?

Mambo yaliyo sasa, mu mbali nami na njia zangu. Siwezi kuwabariki. Naomba mnirudie O’ kanisa potevu! Ningali nasubiri muda kidogo. Kuchelewa sio chaguo. Simameni imara na kutii onyo hili. Tendeni! Maisha ya wengi yamo hatarini.

2 Timotheo 4:3-4. Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watijipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti, nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.

 

SURA YA 9: KUHUSU KANISA LILILOPOTEA

Natuanze. Katika neno hili, nataka kuzungumzia juu ya kanisa langu lilopotea; wale wanaoamini wa salama kwangu ilhali wa mbali nami. Nawazungumzia nyie sasa: wengi wamo katika makanisa wanayoamini yanawapa ukweli wote kunihusu na yale nisimamiayo -- lakini ukweli ni kwamba wamefanya neno langu kuwa hafifu. Hawawambii ukweli wote kikamilifu kwa sababu wengi hawataki ukweli. Hawawezi kustahamili ukweli. Hawataki kuijua injili yangu yote. Wanataka tu yale yanayopendeza masikio yao, ili waendelee kuishi kidunia na kuingilia anasa za dunia. Wakati wa kurudi kwangu umewadia na siwezi kuwachukua waumini wangu vuguvugu. Wataachwa nyuma. Ndipo watakapojuta kile imani yao hafifu imewatendea.

Ufunuo wa Yohana 3:15-16. Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una vuguvugu wala hu baridi wala moto, nitakutapika katika kinywa changu.

Sasa wanangu, hamwezi kutegemea viongozi wenu wa kanisa kuwapa ukweli. Ni lazima mnitafute ninyi wenyewe ndipo mpate ukweli wote. Lazima mkisome kitabu changu, mjitolee kwangu kwa moyo wote na mniulize niwajaze na roho wangu mkiwa na mioyo minyenyekevu na yenye kutubu. Hakuna njia nyingine. Nataka kujitolea kwote. Nitayabadilisha maisha yenu na maisha yaliyojaa wingi wangu na macho yenu yatafunguka kuona ukweli. Ukweli wangu. Ndipo mtaelewa ninachohitaji kutoka kwenu ili muweze kupokelewa ufalmeni mwangu.

Kanisa langu limepotea na wala halielewi maana ya kuwa mfuasi wangu. Hawafuati kanuni na njia zangu. Wanatafuta upenyo utakaowapa njia ya kutenda yale watakayo huku wakijisikia vema na kudhani kuwa wao ni wangu. Haya yamekuwa yakiendelea kwa muda mrefu sana na sasa yamezidi kiwango na ni wachache sana wanaotaka kuujua ukweli wote kikamilifu. Ni wachache sana wanaotamani kuelewa yale ambayo neno langu linasema.Wanataka hadithi ndogo ndogo zinazowafanya wajihisi vyema. Wanakuja na kwenda bila kunijali wala kutaka kujua mimi ni nani. Wanadhani wananijua. Wafuasi wangu wengi hawanijui. Wengi wanatapatapa kwa uhusiano wetu. Hawaelewi kikamilifu maana ya hao kunifanya Mungu wao. Mimi ni kama tu mtazamaji anayetazama maisha yao bila ya kushiriki kwa hayo maisha, bila kushiriki uhusiano wa ndani nao.

Mathayo Mtakatifu 7:21-23. Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

Jambo hili linanihuzunisha sana kwa maana hii ndiyo sababu yangu mimi kuwaumba wanangu, wawe na uhusuani wa ndani nami, ili tutembee katika njia hii ya maisha pamoja. Ila dunia inawavutia hadi wanachagua njia iliyo duni badala ya kuja kwangu na kunijua mimi muumba wao. Huzuni kuu sana hii kukimbilia viumbe na kumkataa muumba; muumba wa vyote wanavyo kimbilia. Ni huzuni kuu kweli! Wanangu, hamuoni kuwa ninahitaji utakatifu na uaminifu? Nataka kuwa wazo lenu la kwanza, mpenzi wenu wa kwanza, nataka kuwa wa kwanza—kwa jumla. Hii ndio maana mliumbwa—muwe wenzi wangu milele. Ikiwa hamwezi kutembea nami kwenye njia hii sasa, mtawezaje kuwa wenzi wangu milele? Mtaunganishwa na nani milele? Mimi au adui wangu? Yafaa mjiulize swali hili wenyewe. Upendo wangu ni wa ndani sana kuliko upendo wo wote ambao mwanadamu anaujua. Msijiuze kwa kutafuta utoshelezaji duni. Hamtawahi kuujua upendo mkuu kuliko wangu. Wana, ipelelezeni mioyo yenu na kuzichunguza nafsi zenu. Tumesimamia wapi, Mimi nanyi? Tunapatana wapi maishani mwenu? Ni nje nikichungulia ndani au tu kwenye uhusiano? Ni mimi kiini cha maisha yenu? Mwanitaka niwe wapi? Jiulizeni. Nawasubiri. Mikono yangu i wazi kuwaleta kwenye uhusiano kamili na muumba wenu, Mungu wenu.

Muda unakaribia wa maamuzi muhimu. Je, ungependa kuwa kati ya bi arusi? Yeye ni wangu kwa jumla. Ananisubiri na kunitazamia. Mimi sio tu ndoto inayopita na ya muda mfupi tu kwake. Mimi sio mtu anayamkujia tu mara moja moja au wakati anahitaji kitu kutoka kwangu. Tumeshikamana. Nikisonga, anasonga. Tunachanganyika. Tu kitu kimoja. Yu kwenye mapenzi yangu na anatembea kwenye njia yangu nyembamba. Mwendo wake na wangu unawiana.

Kwa hivyo wanangu, nawaachia uchaguzi. Ingawa ningependa mnichague, mngali mna hiari. Kwa hivyo ninawaalika mje kwenye uhusiano mkamilifu na kusudi nililowaumbia. Uchaguzi ni wenu. Msingojee sana kuchagua. Toleo hili ni la muda mfupi, halitakuweko milele.

 

SURA YA 10: TAMAA YA ULIMWENGU

Ndiyo binti. Natuanze. Susan, hili ndilo jambo ninalotaka kuzungumzia leo: Dhambi itokayo mioyoni mwa wanadamu – na dhambi ya tamaa ya ulimwengu. Njia zote za dunia ni mbovu, waja waovu wanaoendeleza vitendo vya uovu. Yote dunia itendayo ni mbali na Mungu. Dunia haiko kwenye mapenzi yangu. Dunia hukiri kunijua, bali i mbali sana nami, na ukweli wangu. Inakimbia kwa kasi kuelekea inakotaka kwenda bila ushauri wangu, niliyeiumba. Huu ni uovu. Kukimbilia nje ya mapenzi yangu ni uovu. Mapenzi yangu tu ndiyo mema. Hamuyaoni haya wanangu? Dunia hii itawezaje kuelekea kwa Mungu ikiwa imeniacha mimi Mungu na mambo yote ninayosimamia? Nasimamia utakatifu, usafi wa moyo, sheria na taratibu, ukweli na uadilifu. Dunia hii inapinga njia zangu na hata haikaribiani na yale kitabu changu kinaweka kama ukweli na njia zangu za milele. Dunia inanikashifu na kuzikashifu njia zangu ipatapo njia ya kufanya hivyo. Inawakashifu wanifuatao. Njia zangu haziheshimiwi wala kutukuzwa. Zingalikuwa zinaheshimiwa, dunia haingalikumbwa na huzuni, mateso, magonjwa na masikitiko. Njia zangu zaleta baraka. Njia za ulimwengu zinaleta laana tele. Ni wale tu ambao wanatembea karibu nami na neno langu ndio wapatao amani na utulivu niwapao hata wakiwa taabani.

Huyu ndiye bi arusi wangu anifuataye bila kusita. Anijua. Anipenda. Haendi mbali nami. Anajua ya kwamba mimi ndiye chanzo cha maisha yake, nguvu zake, upendo wake, na uwezo wake. Ni wapi kwingine atakakokwenda ili apate faraja kama hii? Anajua ni vyema kukaa nami kuliko kuwaendea wapenzi wengine. Amenijaribu, akanionja na anajua mimi ni mwaminifu kwake. Ni wake kwa jumla. Hakuna awezaye kupachukua pahala pangu machoni mwake. Dunia haijui upendo wangu. Imekubali mapenzi duni. Ole wao wafuatao dunia na njia zake wakiamini kuwa mfumo wa dunia una majibu yote! Hivi karibuni, dunia itaipoteza nuru yake ya mwisho nitakapomuondoa bi arusi kati yao. Atakapo ondoka, dunia itabaki gizani. Hakutakuwa na chochote cha kutazamia kinachoweza kuwaelekeza kwa ukweli na uzuri. Ubaya na uovu ndio utakuwa duniani. Hii ndiyo dunia itakayokuja hivi karibuni. Haya yatafanyika hivi karibuni.

2 Wathesalonike 3:3-4. Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kitu kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.

2 Wathesalonike 2:6-7. Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake. Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.

Dunia ambayo haishi kwa kufuata sheria na maadili yangu ni kama meli bila usukani. Hii ni meli ambayo imekufa, meli ambayo inazama. Wanangu, hivi karibuni, mtaona kifo na maangamizi ambayo hamjawahi kuona maishani mwenu. Maanake dunia hii imechagua kumgeuka Mungu wake. Muumba wake. Msipumbazwe. Ulimwengu hauwezi kuendelea bila maadili na ukweli wangu. Ni meli inayozama. Ni wakati wa kuondoka kwenye meli hii inayozama. Mtakuja nitakapowaita waumini wangu? Mtanifuata ama mtabaki nyuma mkikwamilia kwa matumaini yasiyo ya kweli kuwa dunia ina majibu yote? Mngali mnawasikiza mbwa mwitu waliovalia ngozi ya kondoo wanaowahadaa na kuwambia kuwa kila kitu ki sawa? Hawa mbwa mwitu wasionijua, wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake. Mtaendelea kupotoshwa na kupofuka kwa sababu mnaufurahia ulimwengu sana?

2 Timotheo 3:5. Wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake.

Njooni mshiriki na Mungu na mgundue kuwa kuna ukweli mkuu, kuna amani kuu, kuna upendo mkuu. Ni miye! Nifuateni wana! Nijueni. Ninastahili kufuatwa. Ninastahili kujulikana. Nipeni muda wenu. Mimi ndiye niliyewaumba. Hamtaki kukaa nami milele? Kuna njia nyingine. Ni mahali ambapo wema wote utokao kwangu unakosekana. Ndiyo. Yote yaliyo mema duniani hutoka kwangu.

Niliumba vyote. Bila mimi, hamtapata tena wema huo wote, vitu vyote vilivyo vizuri mnavyovifurahia vitokavyo moyoni mwa Mungu. Kwa hivyo, yatafakari haya sana. Amueni: milele nami au bila mimi. Amueni. Chagueni. Je, nitawachukua nitakapokuja kumchukua bi arusi wangu? Ni uamuzi wenu. Bali kuna malipo. Ni sharti muachane na ulimwengu na anasa zote za ulimwengu kwa maana njia za ulimwengu sio njia zangu. Nitawaachia ninyi wenyewe muamue mtakako kwenda. Ni wachache sana wanaochagua njia yangu. Wachache sana ...

1 Yohana 2:15. Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

 

 

SURA YA 11: DUNIA INAELEKEA KWENYE DHIKI

Natuanze binti yangu. Sasa nataka kuzungumzia juu ya mambo ambayo yatatendeka hivi karibuni. Dunia inaelekea kwa matatizo. Kuna mawingu makuu meusi kila upande. Karibuni, hivi karibuni, dunia hii itabadilika. Yote yatabadilika kwa ghafla bi arusi atakapoondolewa. Dunia itakuwa na giza na bila matumaini ya kurudia ilivyokuwa hapo awali. Hivi karibuni, wanangu, jambo hili litatendeka. Anzeni kujitayarisha. Mimi sio wa kutia chumvi kwa ukweli. Maneno yangu niyakuaminika. Wakati wa mabadiliko haya waja upesi sana. Mwendo umeshapangwa na hauwezi kubadilishwa. Dunia imekuwa mbovu na hakuna mtu, serikali, wala nguvu zo zote zile zitaweza kusimamisha yajayo. Huu ni wakati wa ufunuo na siku za mwisho. Wakati wa kurudi kwa mwanangu. Hivi karibuni, dunia itajua yaliyotendeka kama mwizi usiku. Hakuna lolote linaloweza kupinga tukio hili. Ilishatabiriwa na sasa yaja kutimia, jinsi maneno yangu yalivyosema kuwa itatendeka.

1 Wathesalonike 5:2. Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.

Wana, mnahitaji kufanya matayarisho. Jitayarisheni. Jitayarisheni kwa kurudi kwangu hivi karibuni, na kurudi kwa mwanangu. Yuaja na jeshi la malaika wake mawinguni ili kumtwaa mpendwa wake. Wakati huu umekaribia. Amkeni enyi waumini. Jitayarisheni. Jitayarisheni kwa tukio kuu kwenye historia, Bwana arusi akimjia bi arusi. Njooni mjitayarishe. Nyote mjitayarishe. Njooni mtayarishwe na damu ya Mwana Kondoo. Jifunikeni kwa damu yake. Damu inapatikana bure. Jitoleeni katika upendo wake mkuu. Mfanyeni mwanzo na mwisho wenu. Tu kitu kimoja: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Sasa wanangu, adui ana mipango yake. Anajitayarisha kuzindua mashambulizi yake dhidi ya wanadamu. Ustaarabu wote u karibu kubadilika. Sitaki mpatwe kwa kutokujua. Bali mageuzi haya makubwa yatatendeka hivi karibuni. Mnahitaji kujitayarisha. Binadamu watashuka wawe na kichaa na maovu yasiyoweza kutibiwa. Hadi mwanangu atakaporudi duniani ndipo maovu yatamalizika.

2 Wathesalonike 2:8. Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake.

Hivi karibuni wanangu, mtahitajika kufikia mapatano: Mtaamini nini? Mtashikilia nini? Ulimwengu ambao unaisha au njia zangu na mapenzi yangu? Nawapa ufalme wa milele. Msidhani ulimwengu una mema ya kuwapa. Ulimwengu u karibu kwisha. Mandhari yake yatabadilika. Msiwe na tamaa mkishikilia ulimwengu usio na mategemeo. Mnapoteza wakati wenu. Ukubali ukweli huu na mwamke. Nawapa ukweli. Someni kitabu changu mkilinganisha na yatendekayo sasa hivi. Ni sawia kabisa maanake yaliyotabiriwa kale lazima yatimizwe. Sio ulinganifu wa kibahati. Hili ni lile neno kuu la Mungu ambalo linatimia. Neno langu halikosi kutimizika. Maneno yangu ni stadi. Mimi ni Mungu mwenye nguvu zote, mwenye ukweli, nisiyepunguza hasira, mwenye uwezo wote, mfalme wa wafalme asiyebadilika, Bwana wa mabwana. Maneno yangu hayabadiliki.

1 Petero 1:24-25. Maana, mwili wote ni kama majani, na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka. Bali neno la Mungu hudumu hata milele. Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.

Aliyelala naamke! Huu ndio wakati wa kuamka. Muwe macho. Wakati ni sasa. Ondoeni vyote vinvyowapofusha. Wekeni chini mambo ya dunia na kunisikiza kwa makini. Saa sita ya usiku yakaribia. Wanangu, nawasihi, msipatikane mkiwa hamjajitayarisha. Jitayarisheni. Wakati wa Mwana kurudi u karibu ....

 

SURA YA 12: KURUDI KWANGU HIVI KARIBUNI

Natuanze. Binti yangu, leo ninataka kuzungumzia juu ya yale yanayohusu dunia kwa ajili ya kurudi kwangu hivi karibuni. Dunia i karibu kushuhudia mlipuko wa mabadiliko. Mabadiliko yaja kutoka pande zote. Kuondolewa kwa bi arusi wangu – wale ambao wamejitayarisha. Wamejitakasa na damu yangu pia kupitia kuoshwa na neno langu. Kutolewa kwa bi arusi kutafuatiwa na uteketezi wa ghafla na kupanda kwa mfumo wa mpinga Kristo.

Waefeso 5:25-27. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili maksudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.

Haya yatakuwa mabadiliko ya ghafla. Hakuna cho chote kitakachokuwa kikuu kuliko mabadiliko haya katika historia. Watakaoachwa watahisi mabadiliko haya na watakaochukuliwa watajua. Wengi watafariki katika mabadiliko haya maana uharibifu waja ulimwenguni. Uharibifu hautakoma kwa maana nitamwaga ghadhabu yangu duniani. Yale ambayo yanafanyika sasa hivi ni kionjo tu cha yale yajayo. Ndio maana ninaendelea kuwaonya kupitia ishara mzionazo na pia kupitia kwa watumishi wangu: vijana kwa wazee wote pamoja. Maonyo yangu yamekuwa wazi na thabiti, kupitia kwa neno langu na maonyo ninayotoa kupitia kwa wengine. Sibadiliki. Mimi ni ukweli udumuo milele. Ukweli wangu haubadiliki. Neno langu halibadiliki.

Wanangu, wakati umetimia. Ni wakati sasa wa kuwaonya wale walio karibu nanyi. Msinyamaze. Waelezeni kuhusu maangamizi yajayo duniani. Wengi wanadhani kitabu change ni hekaya, au hadithi kuu, bali kila neno lililomo ni kweli na litatendeka. Hivi karibuni, kitabu cha ufunuo kitaanza kutendeka kama kilivyopangwa. Mtayaona yote yakitukia machoni penu. Tayari yameanza kutendeka ikiwa mtachukua wakati wenu kukisoma na kuangalia dunia inavyoenda. 

Yote yanayotendeka yalitabiriwa kitambo sana. Yawekeni mashaka yenu kando. Acheni kuwasikiza wasionijua. Kila mmoja wenu ajisomee kitabu change. Mtafuteni Roho wangu Mtakatifu kuwaangazia ukweli, kuwapa marhamu ya macho—haya ndiyo mnayohitaji ili muone ukweli.

Ufunuo 3:18. Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

Sitaki mpatwe ghafla. Nawataka muwe macho muujue ukweli ili muwe tayari. Nawataka wanangu waje kwa nuru a kuona ukweli upo. Upo. Hamna sababu ya kubaki kwenye giza bila kuwa tayari kwa yale yajayo. Naweza kuwaongoza. Niacheni niwaongoze. Natamani kuwaongoza. Natamani kuwashika na kuwaonyesha kuwa mnaweza kuhepa maafa yajayo duniani. Yote hayajapotea. Bado kuna matumaini. Wanangu, njooni kwa mikono ya kuaminika. Nawajali. Nawapenda. Ni tayari kuwafunza bila kujali yale ambayo mumetenda au bila kujali mtokako. Njooni! Njooni! Huu ndio wakati wa wokovu. Msifuate dunia ambayo inaangamia kwa sababu ya kumkataa Mungu mmoja mwenye ukweli na njia zangu nyoofu.

Wengi watakawia sana na baadaye watajuta kuhusu uamuzi wao. Msiache haya yawatendekee. Ni tayari kuwapa moyo wangu. Kuwa wazi nanyi. Kuwaleta kwangu na kushiriki nanyi kwa undani. Hili ndilo tamanio langu: Kuwainua na kuwakinga kwa wakati mgumu. Nawaomba mniache nishiriki nanyi nyakati zenu ngumu. Nataka mniruhusu niwafariji. Natamani kuwa na uhusiano wa namna hii nanyi. O! Nitamanivyo! Msinisukume mbali, mimi muumba wenu. Yakubali niwaambiayo. Nataka niwe karibu nanyi; karibu sana kuliko vile mtu mwingine ye yote yule awezavyo. Nawapa wanangu uhusiano ambao ulimwengu hauwezi kuwapa. Hakuna binadamu awezaye kuwa na uhusiano kama huu na nanyi. Nataka muwe na uhusiano wa ndani nami muumba wenu awajuaye kuliko ye yote yule. Nawapa uhusiano huu wa karibu. Nawapa moyo wangu. Ni wangu kuwapa na ninawapa. Ni wenu ikiwa mtauliza. Ni wachache sana wanaoniuliza, bali upo. Wanangu, nafungua moyo wangu na kuwaalika mje ndani, mnifurahie. Njooni mnijue sana kwa undani, kiliko kuniona kama Mungu aliye mbali nanyi. Mnaweza kunijia. Naweza kuwaambia mawazo yangu niliyonayo juu yenu. Naweza kuwafariji, niwaongoze katika nyakati za matatizo na kuwahimiza wakati munapitia mashaka. Mimi ni Mungu wa upendo. Ni tayari kuwa karibu nanyi. Tutembee pamoja katika maisha haya. Hamtawahi kutembea pekee yenu tena. Ni kando yenu. Kuwaliwaza, kuwashikilia na kuwahimiza. Njooni mnijue katika uhusiano huu ambao nimetamani kushiriki nanyi siku zote.

Niliuumba kwa ajili hii, muwe na uhusiano wa ndani nami. Ndio azma yako maishani. Hata msiponiamini, mimi ndiye muumba wako na hivyo ndivyo ilivyo. Natamani kuwa nanyi wakati mu chini na wakati mu juu. Wakati wa huzuni na wakati wa furaha. Tushiriki maisha pamoja, tutembee katika njia nyoofu pamoja. Haya ndiyo maisha niliyowapangia. Mpango wangu kmamilifu, na mapenzi yangu kwa maisha yenu.

Zaburi 139:3. Umepepeta kwenda kwanguna kulala kwangu. Umeelewa na njia zangu zote.

Kwa hivyo, njooni kwangu. Nitoleeni maisha yenu. Niacheni kwa unyenyekevu, nami nitayachukua, niyasafishena kuyatayarisha kwa ufalme wangu ili mshiriki kwa karamu ya ndoa yangu kama bi arusi wangu. Mkiniuliza nitawapa haya yote. Natamani kuwaweka duniani mwangu. Mimi Mungu ni tayari na ninawasubiri. Acheni kuishi maisha yenu mbali na muumba wenu.

 

 

SURA YA 13: WANANGU, MUDA UNAYOYOMA

 Sasa, hebu tuanze. Wanangu. Nazungumza na wanangu: Muda unayoyoma. Naja kwa kasi kwa mabawa ya njiwa weupe, kwa farasi wa kifahari, nikiwa nimezungukwa na mamilioni ya malaika. Siku hii inakaribia. Mnahitaji kuwa tayari, mkingoja na kukesha, mkinitazamia.

2 Wathesalonike 3:5. Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na saburi ya Kristo.

Huwa sichelewi. Mimi huja kwa wakati. Neno langu ni njema. Natenda ninavyosema na kwa wakati. Wakati wa kufunga umewadia. Kwa hivyo wale ambao mnanisubiri, msife moyo. Mimi ni Mungu anayetimiza neno lake. Neno langu ni njema na thabiti. Mimi ni Mwamba! Hakuna awekaye imani yake kwangu atakosa kuridhika. Hakuna! Sibadiliki. Mimi ni yule yule jana, leo na hata milele. Mimi ni Alfa na Omega! Wanangu, jitayarisheni! Wekeni kando mambo yote ya kidunia na mjitayarishe. Mtajitayarishaje?

Nataka mnyenyekee kwa utiivu.

Nataka toba ya kweli mkinyenyekea na kukiri dhambi zenu mbele ya Mungu Mtakatifu, mnayewajibika kwake.

Nataka mjitolee kikamilifu bila kusita.

Nataka muiweke imani yenu yote kwangu.

Nataka mjazwe na Roho wangu Mtakatifu. Njooni mpokee taa iliyojaa mafuta.

Nataka mjioshe kwenye neno langu na mjisafishe na damu yangu— damu niliyotoa kama fidia.

Nataka mnitafute kwa njia zenu zote na mnijue katika mahali pa siri.

Nataka mtembee nami kila siku na kunitegemea kila wakati.

Nataka muombe kwangu na kuzungumza nami siku yote.

Huyu ni Bwana wenu anayenena nanyi. Wanangu, nawataka muwe macho, mkinitazamia. Nataka mzione dalili, mzitambue siku na kukisoma kitabu changu. Msikose kuujua ukweli. Huu ni wakati mbaya na hautakuwa mwema. Hakuna wema unaokuja duniani, ni mambo ya kutisha tu. Nisikizeni vyema: Ukweli wangu kila wakati ni wa kuaminika. Mnaweza kuutegemea. Nilinena hapo awali kuhusu matukio yajayo na sasa yamewadia. Wana, huu si wakati wakuwa walegevu na kupenda kulala. Amkeni! Njooni kwa ukweli wangu. Jirekebisheni! Nawasubiri. Achilieni dunia! Hii dunia ambayo mnaiamini kwa moyo wote. Msikwamilie dunia ambayo inasambaratika. Haitawapa majibu. Acheni kubwata kati yangu na dunia. Siwezi kukubali kujitolea nusu nusu. Sitakubali kamwe. Ni lazima mje kwangu kikamilifu. Bila hivyo haiwezekani. Wanangu, niliwafia kifo kikamilifu na cha aibu. Nilijitolea kufa bila kuzuia chochote kutendeka kwangu. Sikukimbia ili nizuie kifo changu kwa ajili ya dhambi zenu. Nilipata wakati mgumu. Kila dakika ilikuwa ya mateso. Nilikuwa kama mwana kondoo kwa mbwa. Nililipa deni lote.

Zaburi 22:16. Kwa maana mbwa wamenizunguka; kusanyiko la waovu wamenisonga; wamenizua mikono na miguu.

Msikane deni hili kubwa nililolipa kwa ajili ya adhabu zenu. Mkikataa niwapayo, hamtapata tena msamaha mwingine wa dhambi zenu. Hakuna msamaha mwingine tena wa dhambi. Ingawa watu wanautafuta, haupo. Mimi ndiye malipo ya hilo deni: Damu yangu iliyomwagika. Mateso yangu msalabani. Mwili wangu uliovunjika. Moyo wangu uliovunjika. Nililipa deni lenu. Nanilifanya hivyo kwa hiari yangu ili mpate kuwa na uhusiano bora nami, Baba yangu, na Roho Mtakatifu. Haya ndiyo niliyoyapitia na hiyo ndiyo sababu ya kuyapitia.

Waebrania 13:12. Kwa ajili hii, Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe aliteswa nje ya lango.

Hii ni zawadi yenye tunu. Wanangu, thamana haiwezi kuwekwa kwenye zawadi hii. Hakuna thamana inayotosha. Msiifanyie mzaha na kuiona bila maana. Ipeni heshima zawadi hii. Hakuna zawadi nyingine kutoka kwaMungu zaidi ya hii.

Sasa wana, sitaki malipo ya zawadi hii. Hakuna malipo yanayoweza kutosheleza kulipia zawadi hii. Nawapa bure. Muichukue bila malipo. Msikatae zawadi kuu kama hii kutoka kwa Mungu aliye mnyenyekevu na mkarimu. Kuikataa zawadi kuu kama hii kutasababisha adhabu ya milele. Kukataa zawadi kuu kama hii kutafanya uende jehanamu. Je wanangu, hamunielewi? Msiifanyie zawadi hii mzaha. Muilinde vyema kwa maana ni tunu kubwa kutoka kwa Mungu kwa ajili ya wokovu wenu na uhuru wa milele kuwatoa jehanamu.

Waebrania 10:29. Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyokubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema.

Hii ni zawadi isiyo na kifani. Ni wachache sana hapa duniani wanaoithamini. Ni wachache sana watakaotembea kwenye barabara za dhahabu, kwa ajili ya dharau walionayo juu ya zawadi yangu kubwa kwa wanadamu. Msidanganywe. Kuikejeli zawadi kubwa kama hii ni balaa. Ishikilieni, ithaminini, na kuiheshimu zawadi yangu na kuifurahia kwa maana ni kupitia kwa zawadi hii ndio mtapokea wokovu wa milele, tumaini, na uzima wa milele katika ufalme mkuu wa Mungu. Zawadi yangu kwa wanadamu ambayo ni mimi tu ningeweza kuilipia na mimi tu ningeweza kutimiza yale ambayo mwingine hangeweza. Nawapa pendo langu bure. Pendo langu lililo kuu kuliko pendo lingine lolote lile. Njooni mle nami kwenye meza ya upendo na mpate upendo usiolinganishwa na mwingine. Nawapa bure. Hakutakuwa na wakati mwingine. Utwaeni --- twaeni bure bila malipo. Ni upendo ulioko kila wakati. Huu ni upendo wangu ninaotoa kama dhabihu kwa wote.Ye yote yule awezaye na aje ...

BWANA YAHUSHUA, MFALME MKUU,

MWANA-KONDOO MNYENYEKEVU, DHABIHU ILIYOMWAGIKA

 

SURA YA 14: DUNIA IMENIGEUKA

Natuanze, mwanangu. Wanangu ninataka kuizungumzia dunia ambayo imenigeuka. Dunia hii imenigeuka mimi pamoja na yote yale ninasimamia. Imekua mbovu na isiyokalika.

Yakobo 4:4. Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adhi mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.

Wanangu, dunia imejawa na dhambi. Hakuna unapoweza kupata ukweli na utakatifu. Hata makanisa yangu ya mbali nami. Hata wale wanaodai kunijua wa mbali nami. Wananiweka mbali. Hata viongozi wangu hawapati ushauri kutoka kwangu. Hawanitafuti. Hawanijui. Makanisa yamekuwa maficho ya uasi kwa maana wanahubiri maubiri ya uongo. Hawanijui wala kutaka kunijua. Mimi ni Mungu asiyefahamika kwao.

Dunia haina wakati na Mungu wao. Inamtafuta tu kwa maneno wala sio kwa ukweli. Dunia imejaa waongo na wezi, watu wenye majivuno na waabudu sanamu wanaofuata dunia na mambo ya kidunia, wala sio mimi Mungu wake.

Ni huzuni ulioje kwa wale wasionifahamu bali wanasema na kudhani wananifahamu. Mimi ni Mungu anayeweza kufahamika. Sijajificha kwa wale wanaonifuata. Mimi siye Mungu asiyefahamika kwa wale wanaonikaribia kwa unyenyekevu. Nafahamika. Nikaribie nami nitakukaribia.

Zaburi 73:28. Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu; nimefanya kimbilio kwa Bwana Mungu, niyahubiri matendo yako yote.

Wanangu kila uendako, uovu upo. Hakuna cho chote duniani ambacho adui hajatengeneza kwa minajili ya kuwafanya mkose kuwa karibu nami MUNGU. Mfumo wote wa dunia niwakuhakikisha kuwa wanangu wa mbali nami. Ikiwa adui yangu atawafanya mfuate miungu mingine basi hamtaweza kunitafuta na kuipata njia ya ukweli ili mpokee wokovu wangu, utakatifu wangu, na uhuru wangu.

Huu ni mpango wa adui wakuwafanya mkose kufahamu na mpoteze mahali penu katika ufalme wangu. Mfumo huu wa dunia umewekwa pamoja na mipango ya adui wangu. Kila kitu ni cha ubinafsi wala sio kwa mpango au mapenzi ya Mungu, wala kutafuta Mungu. Adui hataki mje kunitafuta. Anataka mfungwe kwenye mfumo wa ubinafsi unaowafunza kujifikiria tu wenyewe bila kuwajali wenzenu. Anataka ujifikirie tu, ujitegemee, na kujipangia siku zako za usoni mwenyewe bila kumtegemea Mungu.

Hii siyo njia yangu wanangu. Mapenzi yangu yanasema unitafute na kunifuata mimi, unitegemee, ufuate njia zangu. Unapojitafutia mapenzi yako na hiari yako u nje ya mapenzi yangu na hiyo ni dhambi. Unaishi dhambini ikiwa u nje ya mapenzi yangu. Utajuaje mapenzi yangu juu ya maisha yako ikiwa hunitafuti wala kujitolea kwangu kikamilifu? Ni sharti uiweke kando mipango yako, njia zako na uniruhusu kukuelekeza maishani mwako. Ni katika tu kutembea ndani ya mapenzi yangu maishani mwako ndipo utapata uhuru na amani, amani nikupayo. Kufuata njia zako mbali nami itakuangamiza. Hautaweza kushinda dhambi. Mapenzi yangu ni wingi wa Roho Mtakatifu na kuwa na taa iliyojaa mafuta. Hivi ndivyo utakavyo kuwa tayari kwa kurudi kwangu, uokolewe na kupelekwa mahali salama.

Wanangu, amkeni! Huu ndio ukweli! Hakuna ukweli mwingine!

Mathayo Mtakatifu 25:4. Bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao na taa zao.

 

 

SURA YA 15: VIONGOZI HAWANIFUATI

Natuanze tena. Wanangu, ninasononeka juu ya dunia hii ambayo hainijali. Siheshimiwi hata kidogo. Watu wangu hawanitafuti -- wale ambao nimewaita ili kuwaongoza kondoo wangu. Wana mipango yao wenyewe na hawatafuti ushauri kutoka kwangu. Siwezi kuwategemea. Hawawambii watu ukweli, ila tu yale wanayoamini kuwa watu wanataka kusikia.

Watu wangu hawana mahali pa kwenda ili waelezewe ukweli. Ni sharti wanijie! Watapotoshwa makanisani mwao! Watakanganywa na yale yaonekayo kuwa ya ukweli na mwishowe wajipate kwenye mitego ya adui. Adui wangu anataka waamini kuwa wanaweza kuamini maneno ya viongozi wao na kwamba si lazima wanitafute mimi Mungu wao. Ukweli unapatikana tu kupitia kuoshwa kwa neno langu kila wakati. Hii inahitaji nidhamu. Enyi wanangu ni wafuasi wangu na ufuasi unahitaji nidhamu. Ikiwa mtashikwa kwenye mambo ya dunia, mtawezaje kuwa kwenye mapenzi yangu? Haiwezekani. Mimi sio Mungu wakutoheshimiwa na kukanwa.

Dunia imeanza kuona athari za kumkana Mungu wake. Kuna matokeo unapoamua kumkana Mungu. Kuna matokeo magumu. Sifurahishwi na wale ambao wanasonga karibu nami kisha tena wanaukimbilia ulimwengu kwa sababu wanaamini kuwa ulimwengu ni chaguo nzuri kuniliko mimi. Hili si jambo la busara hata kidogo. Ilhali hivi ndivyo walimwengu wanafanya: kuacha matumaini na kukimbilia dunia ambayo inawafanya wajitegemee, wajisimamie, wawe na ubinafsi, na kutafuta njia zao wenyewe. Wakati wangu wa kurudi umewadia. Je wanangu, mu wapi? Mu nami an na ulimwengu? Dunia haina matumaini yote. Ni dunia ambayo inaaguka, dunia iliyopotea. Imepotea kwa maana haitafuti Mungu ili awape majibu kuhusu maisha.

Mapepo sasa yanatawala ulimwengu kupitia njia nyingi: kupitia ujumbe mnaoupata, kupitia mfumo wa dunia ambao umewekwa sasa hivi na kupitia makanisa ambayo yamepotea. Neno langu tu ndilo la kweli na la kutegemewa. Halibadiliki. Kuweni na wakati nami. Muombeni Roho wangu awafunulie ukweli. Atawafunulia ikiwa mtamuuliza katika haki. Anatamani kuwaonyesha ukweli. Hii ndio tamaa yake kuu. Awaonyeshe ukweli ili mweze kuoshwa na neno langu.

1 Wakorintho 2:13. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.

Wanangu, msiruhusu dunia iwazibe macho yenu. Msiruhusu adui awapoteze kama alivyowapoteza wengi. Muwe macho. Njooni kwenye nuru yangu. Mlishwe kwa ukweli wangu na kwa mkono wangu mtakatifu. Natamani kuwalisha ukweli, kuwastawisha na mafunzo yangu kutoka kwa neno langu. Acheni niwalete katika nuru yangu. Niwaonyeshe yale ambayo hamjayaelewe hapo awali. Nina mengi ya kuwambia. Nataka kuwavuta kutoka gizani. Huu ndio wakati wa ukweli kujulikana. Siyo ukweli ulio hafifu, uliokamilika. Msichezee wokovu wenu.

Kwa hivyo njooni kwangu. Ulilieni ukweli. Nitawapa ukweli; ukweli usiobadilika.

Sasa wana, sasa ndio wakati.

Mimi ni YAHUSHUA, MUUMBA VYOTE.

 

SURA YA 16: SAA YA KURUDI KWANGU INAKARIBIA

Tuanze, binti. Saa ya kurudi kwangu wanangu yaja. Saa hii inakaribia kama vile mchana hugeuka kuwa usiku. Naja na hakuna lolote litakalo weza kusimamisha tukio hili.

Yafaa mzingatie sana umuhimu waa tukio hili. Tukio hili litaathiri kila mtu. Hakuna ye yote ambaye hataathiriwa ulimwenguni kote. Kutakuwa na wale watakaoepuka na kwenda nami kwa raha na kuna wale ambao watabaki na kuangamia.

Jinsi utakavyo patikana wakati wa tukio hili ni chaguo lako. Jinsi utakavyoathiriwa na tukio hili ni chaguo lako. Utaenda nami nirudipo kuchukua bi arusi wangu kumpeleka mahali pa salama ama utabaki na kuangamia nimwagapo gadhabu yangu kwa adui wangu?

Chaguo hili linaonekana rahisi ila kuna wachache tu ambao wanachagua kwenda nami. Ni wachache sana wanaonitazamia au wanao amini kuwa kurudi kwangu ku karibu. Mbona hivi wanangu? Ni kwa sababu dhambi imewabana. Wameuzoea na kuukubali ulimwengu huu uliojaa dhambi. Wanazipenda njia za dunia na wazikumbatia haraka na kwa upesi. Hawasomi neno langu, wala kuliamini. Hawanitazami ili niwape majibu wanayohitaji. Dunia na binadamu ndio washauri wao.

Wana, siwezi kuwaokoa wale wasionirudia kwa unyenyekevu, kwa imani kama ya moto. Bila kujitolea kwangu kikamilifu, sitaweza kuwaokoa nitakaporudi ili kumchukua bi arusi wangu. Bi arusi atachukuliwa nanyi mtaachwa. Wale wanangu watakaoachwa watakabiliana na adui. Utakuwa wakati mgumu sana. Hakutakuwa na usaidizi kutoka kwangu.

Marko Mtakatifu 10:15. Amini, nawaambieni, yeyote asiyekubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa. 

Mngali mna nafasi ya kurudi kwangu katika siku hizi za mwisho kabla ya kurudi kwangu. Mkijitolea kwangu, mnipe hiari zenu nitawafanya watu wapya na kuwatayarisha kuingia kwa ufalme wangu.

Ninaona ni wachache sana wanotaka kufanya hivyo. Ni idadi ndogo sana ya watu wanaonifuata jinsi ninavyotaka. Ni wachache sana wanaonipa maisha yao. Wengi wanaamini dunia na fikira za binadamu.

Wanangu, nawataka mjirudi na kuacha upumbavu. Mimi tu ndiye niwezaye kuwasaidia. Hakuna mahali pengine popote pa kwenda. Ndiyo, mnaweza kurudia dunia lakini dunia inaisha na inazorota kila siku.

Nawataka muwe uzimani. Msidanganywe na yale mnayodhani ni ya kawaida. Myaonayo kwa macho yaweza kuwahadaa. Dunia haiwezi kuendelea bila mimi. Mimi ndiye dira ya uadilifu. Bila mimi, dunia itakosa uadilifu.

Wanangu, hivi karibuni, na ni karibu sana, nitarudi. Sitaki muachwe au mpotee. Nawataka mje nami. Huu ndio mualiko wangu kwenu. Nawataka mje nami. Mtembee kwenye njia nyembamba nami. Niacheni niwaongoze. Ushikeni mkono wangu.

Msikose nafasi hii kubwa ya kuwa bi arusi. Ni mrembo na amejitayarisha. Nampenda mno. Ni kanisa langu linipendalo kuliko vyote. Ananishuhudia. Mimi ni wake wote. Naja kumuokoa kutokana na tisho lijalo. Hataathiriwa na yote yatakayotokea. Nitamtwaa mikononi mwangu.

 

 

SURA YA 17: KUHUSU MPINGA KRISTO

Tuanze. Wanangu, ningependa kuzungumzia kitu kipya leo: Nataka kuzungumzia juu ya mpinga Kristo na utawala na mamlaka yake ulimwenguni.

Hivi karibuni, atakuja ulimwenguni ili kuutawala na kutamalaki. Kila kitu kitageuka. Utakuwa wakati usio na matumaini kwa wengi.

1 Yohaha 2:22. Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana.

Wale watakao litaja jina langu watapatikana na makosa. Jina langu litamaamisha kifo. Wengi wanaodai kunijua wataogopa kulitaja jina langu. Hii itatendeka duniani kote. Maangamizo yatakuwa kote duniani. Yatakuwa maangamizi ya kina.

Ufunuo 20:4. Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu, nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.

Mpinga Kristo atakuja wakati ambapo dunia itakuwa inatafuta majibu na suluhisho kwa ajili ya uharibifu utakaokuwa baada ya bi arusi kunyakuliwa. Hili tukio litatendeka hivi karibuni. Dunia itaona shida isiyolinganishwa na nyingine yote.

1 Yohana 4:3. Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.  

Mpinga Kristo atajaribu kuwaangamiza wote wanaoshika njia zangu na ushuhuda wangu. Mpinga Kristo ataleta ile chapa ya mnyama kama njia yake ya kwanza ya kuwadhibiti watu.

Wale watakao kataa kuwekwa chapa ya mnyama wataangamizwa kama wapinzani wa mfumo wake. Wale watakaopewa chapa watawakejeli wale ambao wataikataa. Wale watakaokubali chapa watapotea milele. Hiyo ni miliki ya mfumo wa mpinga Kristo.

Ufunuo 14:11. Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wasujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.

Wanangu, yafaa mzingatie sana maonyo haya bila kuyapuuza. Haya yatatimia hivi karibuni.

Wakati wangu wakumchukua bi arusi yangu umefika. Kanisa langu lililo kweli. Wakati huu umewadia kwa maana mfumo wa mpinga Kristo u karibu kuanza.

Mpinga Kristo anakuwa mkatili na mwenye hamu ya kumwaga damu. Hatakubali cho chote kiwe mbele yake. Ni mwingi wa hasira na tamaa ya uongozi. Hawajali watu. Hana huruma. Anaishi tu ile aweze kutawala na kutamalaki ulimwenguni kote.

Atafanya uharibifu ili awape nguvu watu wake. Hakuna kitakacho mzuia hadi nirudi kumsimamisha. Hakuna mwanadamu yeyote awezaye kumsimamisha ila mimi.

2 Wathesolonike 2:8. Hapo ndipo atakapofurushwa Yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake.

Nyakati za uovu zaja. Mipango ya mfumo huu kuanza inafanywa kisirisiri.

Watakao baki baada ya kanisa kunyakuliwa watatambua kuwa wanatawaliwa na mfumo wa mpinga Kristo ambao ni wa kuangamiza.

Wakristo walio vuguvugu ambao wataachwa watatambua kile ambacho kitakuwa kimetukia. Majuto yatakuwa makuu. Wengi watamfuata mpinga Kristo kwa sababu njia ya kumfuata Mpinga Kristo itakuwa rahisi kuliko ya kutomfuata. Utakuwa wakati wa uchaguzi mgumu. Wengi watajua mioyoni mwao kile ambacho wanahitaji kufanya na kwa ajili ya ujasiri wao na tama ya kuona ufalme wangu, watafanya uchaguzi huo mgumu. Imani yao itawasaidia. Imani ya kumkataa mpinga Kristo na kunichagua mimi. Wengi hawatakuwa na imani hii pamoja na ujasiri huo.

Ufunuo 19:20. Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hali katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti.

Kweli wanangu, jitayarisheni ili muweze kuokolewa. Wakati umefika. Jitayarisheni. Mkingoja na kunitazamia. Macho yenu yanitazame mimi. Mimi ndio mlango….mlango wa kutoka…. Mlango wa kuepukia. Hivi karibuni nitaufunga mlango huu. Huu tu ndio utakaokuwa mlango wa kuepukia. Wakati umewadia.

Kanisa langu lafaa kujitayarisha.

Mathayo 25:10. Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.

Mpinga Kristo yu pembeni. Anafanya matayarisho ya kushika usukani. Anatafuta kutawala duniani. Hakuna litakalomzuia. Ukatili ndio alama yake. Atatawala kwa hofu na ukatili. Hakuna anayeweza kumzuia duniani. Nguvu zake zinakuja kupitia kwa adui yangu. Yeye ndiye mwenye ukatili huo.

Msiyapuuze mambo haya. Muonayo ni udanganyifu. Mnadanganywa kuwa kila kitu ki shwari. Adui wangu ndiye anayewadanganya. Anataka kuwapoteza. Hawataki mtembee kwenye njia nyembamba ili mnijie na kuokoka.

Wanangu wamedanganyika kuwa kila kitu ki sawa. Yote si sawa wanangu! Yote si sawa! Dunia inatawanyika. Yafungueni macho yenu. Myakubali yanakuja kutukia. Amkeni! Tazameni! Someni neno langu na kulinganisha na yale yatendekayo kwa sasa.

Dunia inamkataa Mungu katika pande zote nne. Siwezi kuvumilia tena. Nauondoa mkono wangu wa ulinzi juu ya dunia, na kuiacha ifanye itakalo, bila mimi Mungu, Muumba wake.

Mimi ni Mungu anayeelewa bali dunia ikinitaka niondoke na kusimama kando, hivyo ndivyo nitakavyofanya. Ndipo mtakapogundua kuwa bila mkono wangu wa ulinzi, mambo ni tofauti. Ni mvumilivu, lakini sasa uvumilivu wangu umefika kikomo. Wanangu, nawasihi… tafadhali njooni kwangu. Jitoleeni kwangu kikamilifu.

Nipeni maisha yenu. Nitayakubali. Nitawafunika na damu yangu. Nitawaosha kwa neno langu. Wakati umefika. Mnahitaji kusafishwa ili muweze kuja nami nitakapokuja kumchukua bi arusi. Mngali mna nafasi. Jitayarisheni. Muda umekwisha. Hakuna kitakachonizuia.

NI mimi YAHUSHUA….. MFALME MKUU… MUNGU MNYENYEKEVU.

Yohana Mtakatifu 15:3. Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.

 

 

SURA YA 18: MUDA WA KUSHUKA KWANGU UMEFIKA

Natuanze tena. Sasa ni wakati wangu kuzungumzia juu ya mada mpya: Wana, muda wangu wakushuka chini umefika.Wengi hwajajitayarisha na wengi wana anguka. Wengi hawajeiwahi kukitayarisha. Kuna mabadiliko mengi ambayo hivi karibuni yatatendeka duniani. Nataka mwamini ukweli huu.

Wana, saa yangu ya kurudi imefika. Naona kuwa wengi hawajajitayarisha. Wengi wanamini wa tayari ila siyo hivyo. Wengi bado wanacheza na dunia. Hii haiwezekani. Wanangu, vunjeni uhusiano na dunia. Dunia hii ni meli inayozama na itazama nanyi.

Wanangu, sifurahiswi na jinsi mnavyo fukuza vitu vya dunia badala ya kunifuata. Mwatafuta majibu kutoka kwa dunia. Haiwezekani wanangu.

Mwatazama tumaini lilo bure… Ahadi za bure … ukweli ulio bure. Majuta ikiwa mtaendelea kuifuata hii njia isiyo na matumaini yo yote. Mbona mnaendelea kuamini kuwa dunia itawapa majibu hali mimi ndiye ukweli.

1 Yohana 2:15. Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

Wana, sikizeni kwa makini, wakati wenu unakwisha. Mna muda mdogo sana wa kujitayarisha. Wakati wa kujitayarisha ni huu. Ikiwa mnataka kuja nami, ni sharti mzingatie kurudi kwangu. Adui wangu anajitayaisha kutenda mambo yake hivi karibuni. Mipango yake itaharibiwa tu na kurudi kwangu.

Wanangu, hamuoni kuwa ni sharti muwe macho na tayari kwa matukio ambayo ya karibu kutendeka? Hivi karibuni kila mtu ataathiriwa na mabadiliko yajayo duniani. Aidha mnakuja nami pahali pa salama au mnabaki ili mpambane na adui wangu na ghadhabu yangu ijayo.  

Siku hii yaja, wanangu. Yaja na hakuna awezaye kuizuia. Mwafaa mjitayarishe maana wakati u karibu. Waja kwa upesi.

Njooni mnijue. Hamna njia nyingine. Msipotenga wakati wakunijua, basi hamtaweza kuja nami mahali pa usalama.

Lazima mjitolee na kuniachia kila kitu kilicho chenu. Nawasubiri wanangu. Nani atakaye nijia kwa kujitolea kikamilifu? Nani atakaye kuja ili anijue, anijue kweli. Hivyo ndivyo ninavyohitaji.

Niliwatengenezea njia. Nimewatengenezea njia. Nimelipa gharama kubwa sana kwa ajili yenu ili muwe huru ili muweze kuwa nami nitakapokuja kumchukua bi arusi wangu. Bi arusi wangu yu tayari nami namjia.

Gharama niliyolipa ilikuwa kubwa sana. Hakuna ye yote ambaye angefanya nilivyofanya. Ni mimi tu ndiye nigeweza kutimiza yale niliyotenda. Ni mimi tu ningeweza kulipa gharama kubwa kiasi hicho – Mungu ambaye alijiweka kua kiwango cha binadamu na kupondwa kwa ajili ya binadamu. Gharama hi haiwezi kuhesabika. Hakuna thamani inayoweza kuwekwa kwa kitendo hiki. Hakuna kiasi cha fedha kinachoweza kulipa gharama iliyolipwa.

Isaya 52:14. Kama vile wengi walivyostajabia uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu yeyote, na umbo lake zaidi ya wanadamu.

Wana, msiikatae zawadi kama hii. Njooni, nawapa zawadi hii bure. Naomba muichukue zawadi inawangoja muichukue ili muwe huru, huru kuja kwangu na kwenda nami nitakapokuja kuwavuta wanangu ili wapate uhuru.

Hii zawadi ni yenu. Njooni kwangu na mjitolee kwangu. Nipeni yenu yote yanayowahusu. Ninachotaka tu ni ninyi muniachie maisha yenu yote niyatawale. Msipokuja kwangu na kuwa wana wangu, mtakuwa mngali wana wa adui wangu. Hamna lenu. Aidha ninyi ni wangu au ni wa adui wangu. Nichagueni. Nangoja jibu lenu.

Huyu ni BWANA na MWOKOZI, YAHUSHUA, MASIYA MKUU.

 

 

SURA YA 19: JITAYARISHENI

Natuanze (Februari 19, 2012). Wana, nina maneno: Wakati wa kurudi kwangu unakaribia. Mnahitaji kujitayarisha. Nataka niwachukue nimkujiapo bi arusi wangu, mrembo, bali ikiwa hamtakuwa tayari, sitawachukua.

Ni sharti mjitayarishe. Mnionyeshe kuwa mu tayari. Nawataka muwe mkinitazamia. Nataka macho yenu yawe kwangu. Ikiwa haunitazami, basi hauko tayari. Wale wanaonitazamia tu ndio walio tayari.

Waebrania 9:28 kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.

Wengine wanasema hawahitaji kunitazamia ili wawe tayari. Huu ni uongo kutoka kwa adui. Ni mjanja na mwingi wa udanganyifu. Anataka kuwaongoza wanangu mbali na kuwatoa kwenye njia nyembamba. Ni lazima muwe tayari kila wakati. Ni sharti mnitazamie na kujitayarisha kwa maana hamjui saa nitakayo rudi. Nitakuja kama mwizi usiku. Je, neno langu halisemi hivyo? Neno langu li wazi kuhusu jambo hili. Wengi watapigwa na bumbuazi. Hawatakuwa tayari kwa maana walikataa kunitazamia na kusimama imara.

Msiwe kwenye kundi hili ambalo linakataa kutii maonyo yangu na yakunitazamia na kuwa tayari. Kundi hili litahuzunika sana na kufadhaika likigundua kuwa wameachwa ili wapambane maafa ya dunia na misukusuko ya binadamu.

Msiwe wanyamavu nawasiotenda lolote kwa ajili ya maonyo mengi niwapayo. Kuweni tayari! Amkeni!

2 Timotheo 4:8. Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake. 

Wanangu, hata mnaruhusu kazi zenu za huduma ziwafanye msijitayarishe na tukio hili kuu. Makanisa mengi na viongozi wangu wengi wataachwa. Msipatikane mtegoni humu. Muwe macho. Muwe tayari. Mjihadhari.

Usiache nyumba yako invunjwe na mwizi. Usisimame tu kando ukiangalia nyumba yako ikivunjwa na mwizi. Mlinzi asiyejitayarisha atashtuka mwizi akija bila matarajio. Jilindeni. Jitayarisheni kwa maana hamjui saa ile nitakayorudi. Wakati mnapodhani kuwa siji ndipo nitakapo kuja.

Nikishamchukua bi arusi wangu, kanisa langu, sitarudia na hii njia tena. Mlango utafungwa na hakuna binadamu atakaye weza kuufungua.

Luka 13:24-25 Wakati mwenye nyumba atakapo simama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema Ee, Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia Siwajui mtokako.

Kurudi kwangu ni kwa haki na upesi. Sitachelewesha tukio hili kwa ajili ya mtu yeyote au kitu chochote. Laja, hakika laja. Kesho huenda ikawa umechelewa. Hivyo ndivyo kurudi kwangu kulivyo karibu. Msichelewe kwa uamuzi wenu na kujitayarisha kwa kurudi kwangu. Mkingoja sana mtanikosa. Huu si wakati wa kuchelewa na kurandaranda kwa njia za dunia.

Wana, msingojee kufanya uamuzi. Sitalisubiri milele ili kanisa langu vuguvugu liamke. Nawaomba myaweke maanani maneno haya. Sitaendelea kulisubiri kanisa ambalo linakataa kunifuata na kunitafuta. Haiwezekani.

Nitaendelea na mipango yangu na kuwachukua walio tayari. Wanaonitafuta kwa bidii, na kunisubiri kwa matarajio makuu. Hawa ndio nitakaowachukua… wengine wote wataachwa.

Nawaomba msamaha ikiwa maneno yangu ni magumu. Maonyo yangu yamekuwa wazi na bila kusita. Mbona watu hawaamini neno langu? Je, mimi MUNGU sijakuwa hivyo? Mimi sibadiliki.

Waebrania 13:8 Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.

Jitayarisheni, kwa maana ni tayari kumchukua mpendwa wangu. Ni tayari kumchukua. Ikiwa unataka kuwa mmoja wa bi arusi wangu, basi jitayarishe. Wakati ni huu “sasa”. Jitayarishe.

Muda unakwisha. Tazama na kujitayarisha. Haya ni maneno yangu. Nami hutimiza maneno yangu.

BWANA WENU YAHUSHUA.

 

SURA YA 20: WAKATI WENU U KARIBU KWISHA.

Natuanze (Februari 20, 2012). Ni tayari kukupa maneno: Wana, Ni mimi, BWANA wenu na ni hapa kuwapa muelekeo mpya.

Dunia inakwisha upesi. Wakati waja wa dunia kuipata gadhabu yangu. Saa hii yaja upesi, wana, kwa kasi mno. Kuna wakati kidogo sana umebaki, kila mmoja ataweza kuelewa. Ni hivi karibuni.

Ufunuo 14:10: Yeye naye atakunywa katika mvinyo wa gadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana- Kondoo.

Wana, kaeni chonjo na kuwa macho. Msitupilie mbali maonyo haya muhimu.Tieni bidii kwa kujitayarisha. Kurudi kwangu ku karibu sana. Hakuna wakati wa kupoteza. Amkeni!. Sitawasubiri milele. Siwezi. Ni sharti nimuondoe bi arusi wangu natuondoke. Yu tayari. Amejitayarisha. Nawataka ninyi muwe tayari pia. Wanangu, njooni kwangu kwa unyenyekevu. Hii ndio saa yangu ya kurudi.

Msingonjee milele. Hamna “milele”. Wakati wenu u karibu kwisha. Najua haya yanawajia kwa mshangao nakutoamini, ila ukweli ni kuwa wakati umefika wangu mimi kumuondoa bi arusi. Yu tayari, ni tayari, na dunia imenipa kisogo.

Hivi karibuni, bi arusi wangu aningojeaye hataningojea tena. Sitamruhusu abaki nyuma na kukumbana na yale yajayo kwa walio duniani ambao wamenigeuka. Amejitayarisha na wakati wake wa kuondolewa na kupelekwa mahali pa usalama umefika.

Ufunuo 19:7. Natufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

Hili litakuwa tukio kuu lisilolinganishwa na linguine lote katika historia ya binadamu.  

Wana, jitayarisheni ili mje nami. Tukutane hewani. Nataka niwachukue mwende nami pahali pa usalama. Hivi karibuni itatendeka.

Msidanganywe na dunia. Wengi wanakwamilia kwa dunia wakidhani kuwa itawapa majibu. Dunia ina simanzi na hofu. Msihangaishwe na maonyo haya. Yakubali maana ni ukweli.

Kiangalieni kitabu changu. Kisomeni. Fungueni kurasa zake. Acheni ukweli wangu ufunuliwe mbele yenu, ukweli wangu.

Nitafuteni mimi. Fuateni Roho wangu. Acheni Roho wangu awaonyeshe ukweli. Mruhusuni aje maishani mwenu na awape kuelewa kupya kwa neno langu. Binadamu hawawezi kuwaonyesha ukweli. Roho wangu tu.

1 Wakorintho 2:11-14. Maana ni nani katika binadamu ajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukupokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.

Wana, saa hii inakaribia. Niacheni nizitendee kazi roho zenu. Niacheni niwaoshe kwa damu yangu ya ukombozi. Niacheni nizifunike dhambi zenu na damu yangu iliyolipa fidia msalabani. Huo msalaba wa aibu ambako nilivuja damu hadi kufa kwa ajili ya dhambi zenu. Nilifanya haya yote kwa ajili yenu wanangu. Ninyi wote..nilivuja damu kwa ajili yenu….wale wote watakao ikubali zawadi hii ya bure.

Wafilipi 2:8. Tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.

Naam, ulikuwa upendo wangu na matakwa yangu kuwaokoa wanadamu kutoka kwa makosa kwa ajili ya laana za dunia hii. Hii zawadi ni yenu pia ikiwa mtakubali kuichagua na kuichukua na kupata msamaha wa njia zenu mbovu.

Ni sharti mu ihitaji. Ni sharti mje kwangu kwa kujitolea kikamilifu. Nataka kuwaona mkiachana na upendo wa dunia na mambo yote yanayohusu dunia. Hamwezi kuwa kwenye ufalme wangu ikiwa mngali na mapenzi kwa dunia.

Kwa hivyo mna uchaguzi wa kufanya! Njia zangu ama mnachagua kwenda kwa njia zenu wenyewe pamoja na adui wangu? Hakuna kuwa katikati. Ni upande mmoja au mwingine. Hiari yenu au hiari yangu. Lazima mchague.

Ikiwa mtachagua mapenzi na hiari yangu, ni sharti mje kwa unyenyekevu na kutubu dhambi zenu. Nitawafunika kwa damu yangu na kutoa dhambi zenu zote. Kumbukumbu zote zitaharibiwa na maisha yenu yatakuwa mapya.

Waebrania 13:12. Kwa ajili hii, Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe aliteswa nje ya lango.

Haya ndiyo yawangojayo ikiwa mtakuja kwangu kwa kunyenyekea na kutubu dhambi zenu. Huu ndio wakati wa uamuzi huu. Msingojee. Wakati wa kurudi kwangu umewadia. Hakuna binadamu awezaye kuisimamisha saa hii.

Mwafaa mjitayarishe. Jitayarisheni. Nasubiri jibu lenu.

Huyu ni wenu Mstahamilivu, Mungu mpendwa, YAHUSHUA.

 

SURA YA 21: MBALI NA MAPENZI YANGU, MWANIPINGA

Natuanze, Binti yangu. Wanangu, Nataka kuwazungumzia kuhusu mada mpya.

Hivi karibuni, wanangu, nitafika na kuliondoa kanisa langu. Ni wachache sana ambao wa tayari… waningojea… wananitazamia.

Hili ni jambo zito, kweli. Ni wanangu wachache sana wanaonisikiza. Ni wachache sana wanaoyatilia maneno yangu maanani. Wengi hawasomi kitabu changu wala kuyatenda maneno yangu yaliyomo kitabuni humu. Hawazifuati sheria ambazo nimewapa. Wengi wanatenda wapendalo, bila kujali ninavyofikiria.

Wako nje ya mapenzi yangu kabisa, na wanatenda kulingana na hiari na mapenzi yao wenyewe.Mnapoenda mbali na mapenzi yangu, mnanipinga. Hili ni jambo la kuhuzunisha na wengi hawaamini neno langu na wameamua kuifuata dunia, badala ya kunifuata.

Wana, dunia ina uadui nami. Hamwezi kuwa nami, na dunia pamoja.

Yakobo 4:4. Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.

Inamaanisha nini kuwa mmoja wa dunia? Ina maanisha kugeukia dunia ili dunia ikupe majibu yote uyatakayo: kufuata dunia kwa usalama wako, ukidhani kuwa dunia ina majibu yote. Huu ni usalama wa uongo – kutazamia majibu kutoka kwa binadamu. Binadamu asiyejua cho chote kuhusu yajayo. Ni mimi tu MUNGU nijuaye yajayo. Dunia inatafuta majibu kutoka kwa binadamu na mapepo mabaya. Mfumo wa dunia ni mfumo wa adui wangu. Anawataka wanangu wapotezwe na kila aina ya vitu ili wasinitafute niwape majibu. Kwa hivyo hawanitafuti ili kunijua kwa undani na kuwa na uhusiano wa karibu nami. Hii ni hatari sana wanangu.  

Zaburi 20:7. Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu.

Anawataka muwe mbali nami ili awanase na kuwaangamiza. Atatumia mbinu zote ili awanase. Atatumia huduma zenu, familia zenu, pesa na mali, burudani, na cho chote kile awezacho ili awapoteze. Hii ndiyo mbinu yake ya kuwafanya mniache na kuwa mbali nami.

Hii ndiyo mipango yake yakuwaangamiza na amefaulu kwa wengi wenu. Ni wachache sana wanaonifuata kwa karibu. Hili ndilo kanisa langu kamili. Hawa ndio wafuasi wangu kamili ambao wamejitolea kunifuata kikamilifu.

Mbona mnasisitiza kufuata dunia hali mimi ndiye nuru ya ukweli? Mimi ni uzima wa milele. Nawapa uhai, nawalinda. Mimi ndimi niyalindayo maisha yenu. Mimi ndiye niwapao uhai na kuuchukua tena ….hakuna mwingine.

Ayubu 12:10. Ambaye nafsi ya kila kilicho hai i mkononi mwake, na pumzi zao wanadamu wote.

Mbona mnashikilia kutonijali na kuwafuata wapenzi wengine? Wapenzi wasio na cho chote? Mwajichimbia shimo ninyi wenyewe….shimo ambalo hamtaweza kutoka ndani yalo.

Njooni kwangu. Tubuni na kuniachia maisha yenu. Ni mimi tu niliye na majibu. Ni mimi tu niwezaye kuwatendea yaliyo haki. Ni mimi niliye na ufunguo wa ufalme. Dunia hii haina cho chote cha kuwapa. Ni mateso, masumbuko kisha kifo hivi karibuni na uharibifu ujao duniani.

Acheni kuyaweka matumaini yenu kwa dunia ambayo imekufa… imekufa kwa maana hainitambui kama BWANA na MKUU wao. Hakuna Serikali ambayo inanitambua duniani.

Viongozi wote duniani wanafuata imani zingine, badala ya kunifuata mimi ambaye ni BWANA na MUUMBA. Hii ni makuruhi na sitakubali yawe hivyo. Dunia hainiogopi na kwa hivyo, nitawafunza tena ili wanitambue kuwa MIMI ni nani. Nitawachukua wachache waniaminio mahali pa usalama ndipo dunia itanitambua kuwa mimi sio MUNGU wa kuwekwa pembeni. Hivi karibuni nitauondoa mkono wangu wa kinga na adui wangu ataanza kutenda kazi yake duniani ... yeye na Jeshi lake la mashetani. Utakuwa wakati wa huzuni kwa wakaazi wa ulimwengu huu.

Zaburi 111:10. Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima, wote wafanyao hayo wana akili njema, sifa zake zakaa milele.

Nifanye nini ili niweze kuwaelezea ukweli huu? Mniamini? Yote yameandikwa kitabuni mwangu, bali ni wachache sana wanaotaka kuujua ukweli. Mnakimbia huko na huko mkitafuta maarifa na busara, bali hamji kwa UKWELI.

Danieli 12:4. Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukatie muhuri kitabu hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka. Ni saa ya huzuni kwa wanadamu: watu wanaokimbiza dunia bali hawatamani kuwa na maarifa yatokayo kwa MUUMBA, wao. Huu ni wakati wa huzuni kwa binadamu. Matokeo ya kutonijali mimi MUNGU, ni wazi kabisa: uovu, magonjwa, uhalifu, kifo, uharibifu wa uchumi, vita na matetesi ya vita. Hii ndiyo shida binadamu wanayojiletea wakati wanamuacha MUNGU wao na kufuata dunia.

Wana, nirudieni. Hamjachelewa. Nitawatwaeni. Nawasubiri. Kimbieni mikononi mwangu. Njooni mnifuate.Tunaweza kuwa pamoja milele. Naweza kuwafanya muwe wangu. Na muishi maisha ya milele nami huko. Ndiyo wana, nifuateni, Muumba wenu au muifuate dunia bila mimi. Chaguo ni lenu. Nawajia watakaonichagua hivi karibuni. Wanipendao na wala sio wapenzi wa dunia. Chagueni kati yangu na dunia, kwa sababu ni sharti nije niwaokoe walio wangu. Wanaonichagua mimi badala ya kuchagua dunia. Mtafanyani?

Nasubiri kwa makini, bali si kwa muda mrefu. Hivi karibuni, ni sharti nimuondoe bi arusi nimpeleke mahali pa usalama. Huyu ni BWANA, NA MUUMBA WA dunia, YAHUSHUA.

 

 

SURA YA 22: UOVU WAJA KUINGAMIZA DUNIA

 Natuanze tena. Wana, huyu ni BABA yenu anayezungumza. Nina maneno mengi yakuwapa leo.

Kuna dhoruba kuu ijayo ulimwenguni mwote. Inaitwa “uovu”. Yaja kuangamiza dunia na wakaazi wote.

Itakuja baada ya kumuondoa bi arusi wangu kwenda mahali pa usalama. Ataondoka kwanza. Hatashuhudia vitisho vijavyo. Baa lijalo nchini litawafanya wengi kuwa wazimu. Vitisho visivyo semekana vyaja. Utakuwa wakati wa vitisho tupu.

Waja watashtuka. Hakutakuwa wa kuaminika. Ni wakati wa vitisho ulioje.

Mpinga Kristo atatawala. Atatawala dunia nzima. Hakuna atakayeweza kumkomesha. Viongozi waliokuwapo walionyanyasa watu hawataweza kulinganishwa naye na tamaa yake ya damu. Hakuna wakufananishwa naye. Hakuna atakayeweza kujificha. Hakutakuwa na msaada wowote kwa yule atakayetaka kumuepuka. Kuepuka kutokana naye kutakuwa tu ni kifo. Huu utakuwa wakati mgumu katika historia ya binadamu.

Ufunuo 18:4-5. Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni na Mungu amekumbuka maovu yake.

Wana, amkeni na kuuona ukweli huu. Kisomeni kitabu changu. Yasomeni yatakayotukia. Kaeni chonjo. Jisalimisheni … njooni mikononi mwangu iwasubirio. Ni tayari kuwaokoa. Ni tayari kuwapokea, kuwabariki, na kuwaleta katika ufalme wangu mtukufu, kwenye upendo na uzuri wa milele. Nitawaleta kwenye karamu yangu ya ndoa ambapo tutaungana na kushiriki pendo letu milele na milele.

Hamuhitaji kuogopa siku za usoni. Hamuhitaji kuwaza juu ya mambo ya kesho. Mnachohitaji ni kujitolea kwangu. Jitoleeni kikamilifu. Nipeni yenu yote: maisha yenu, roho zenu, nafsi zenu, mioyo yenu, na mipango yenu yote. Nifanyeni niwe BWANA wenu. Nitawaongoza kwa usalama.

Ni wachache sana wajao. Ni wachache sana wanaotaka kushiriki kwenye wokovu wangu, nitakapo wapeleka wanangu kwa usalama kwenye mbingu zangu. Mtapokea miili mipya mitukufu. Itakuwa miili iliojaa nuru, nuru yangu ya mbinguni. Itanawiri, ya milele, isiobadilika na yenye utukufu. Wanangu, bi arusi wangu atakuwa mrembo sana.

Ndiyo, huku kubadilika kwa kanisa langu ku karibu. Hatakuwa alivyokuwa tena. Atakuwa na utukufu. Mabadiliko haya yatatendeka kwa kufumba na kufumbua macho kwa dakika moja, kanisa litabadilika tayari kwa BWANA ARUSI. Litakuwa tayari katika utakatifu na usafi.

1 Wakorintho 15:51-54. Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho, maana parapanda italia na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, mauti imemezwa kwa kushinda.

Atapendeza kwa mavazi yake yote. Namjia bi arusi wangu. Najua ananitazamia na kunitafuta. Imani yake ni imara. Yeye ndiye niliye mfia. Yeye ndiye aipokeayo zawadi yangu. Zawadi yangu ya wokovu nitoayo bure kwa binadamu. Ni wachache sana wanaoitikia zawadi hii na waifuatayo. Jambo hili lanihuzunisha sana; wana. Nilivuja damu nikafa kifo cha uchungu ili niwaokoe watu wote. Ni wachache sana wanaoutaka wokovu huu. Ni wachache sana wanaokubali wokovu huu na kujitolea kwangu.

Njooni wanangu, msiwe miongoni mwa wale watakaobaki na kupotea. Badilisheni nia zenu. Nitafuteni kwa mikono iliyo wazi. Kimbilieni mikononi mwangu, inayowangoja.

Saa hii inaisha haraka. Mu karibu kuuona mwanzo wa uovu na dhiki kuu. Amkeni. Zijazeni taa zenu na mafuta. Zikiwa bila mafuta hamtaweza kuja nami.

Mtakatifu Mathayo 25:4. Bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.

Njooni mumpokee Roho wangu Mtakatifu kikamilifu. Atawawezesha kuwa na uhusiano wa ndani nami. Kisha nitawaosha katika damu yangu na kuondoa madoa yote kwa nguo zenu na kuwaweka tayari kwa ufalme wangu. Hivi ndivyo mtakavyokuwa bila ila wala kunyanzi lolote. Bi arusi wangu mrembo.

Waefeso 5:25-27. Enyi waume, wapendeni wake zenu, jinsi Kristo alivyolipenda kanisa, akajitolea kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.

Nataka kuwaleta pahali hapa, pahali pa uhuru na uzima wa milele. Njooni tu kwangu na mjitolee nami nitaanza kuwaweka tayari. Wakati unaisha. Amueni. Mwabaki au mwaja nami kwenye uhuru na usalama? Sasa wana, amueni. Nawataka muwe tayari, tayari kweli. Upendo wangu wawasubiri. Ni mimi mfalme wenu YAHUSHUA.

 

SURA YA 23: SAA SITA YA USIKU INAKARIBIA

Natuanze tena. Wana, huyu ni Bwana wenu anayezungumza nanyi. Nina maneno mengi ninayotaka kuwaambia.

Saa imefika, wanangu. Mnachelewa – saa inayoyoma. Saa sita za usiku zi karibu kutimia. Ni dakika mbili tu zimesalia.

Hii inamaanisha muna wakati mfupi sana wa kujitayarisha namaanisha kuitayarisha mioyo yenu na kuwa tayari. Ni saa ambayo kurudi kwangu kunakaribia sana. Kurudi kwangu ni kwa kumvuta bi arusi wangu nimuweke huru kutokana na ukaidi na gadhabu zitakazofuata. Hataathiriwa na yale yajayo. Bi arusi wangu ni mrembo na ametayarishiwa MFALME wake, na Bwana arusi wa Kifalme. Macho yangu ya kwake. Urembo wake unanitia bumbwazi. Ananifurahisha na ung’aavu wake. Ni watu walio tayari kumpokea BWANA ARUSI wao.

Wimbo ulio Bora 4:9. Umenishangaza moyo, umbu langu, Bibi arusi, umenishangaza moyo, kwa mtupo mmoja wa macho yako, kwa mkufu mmoja wa shingo yako.

Wamejitayarisha, wameoshwa kwa damu yangu. Wameoshwa na neno langu. Wananitazamia kwa hamu. Kila siku wananitazamia.Wananitarajia na kuniangalia pekee. Tuna ushirikiano wa ndani nao. Tunafahamiana. Watu wangu wamejitolea maishani mwao na wameachana na tamaa za dunia. Wananitumainia mimi tu. Wanautafuta uso wangu na sauti yangu. Wanaifahamu sauti yangu. Nizungumzapo hao hunifuata. Wanikimbilia.

Yohana 15:19. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi niliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. 

Nawathamini. Nawaongoza nao wanifuata. Maisha yao yanaangaza nuru yangu duniani. Hao ni mfano wangu kwa ulimwengu, ulimwengu unaoisha.

Hivi karibuni nuru hii itaondolewa duniani, na giza tu ndilo litakalosalia. Vivuli vitaingia na kutawala. Giza litatanda ulimwenguni mwote… pembe zote nne za ulimwengu. Itakuwa siku ya huzuni kweli.

Hamfai kuwa hapa wakati huu wa huzuni. Mwaweza kunifuata kwa kujitolea. Nitawaleta kwangu, niwakinge na kuwaongoza mahali pa usalama, nitakapokuja kulitwaa kanisa langu, kanisa langu bora. Yu tayari na nitamkinga kutokana na wakati huo wa giza kuu lijalo duniani. Wana, wakati wangu wa kurudi umewadia. Wakati uliosalia ni mchache sana. Ni sharti mjitayarishe. Kuna wakati kidogo uliobaki. Msiuharibu, kwa kufuata vitu visivyo na maana duniani. Utumieni wakati huu kujitayarisha.

Nifuateni kwa moyo wote. Tubuni dhambi zenu. Ninataka kusikia toba itokayo kwa moyo uliyojaa simanzi. Moyo wa mtu humdanganya. Ni miye pekee nionayo yaliyo moyoni mwa mwanadamu. Naweza kuona katika pembe zote za moyo na dhambi iliyofichwa humo isiyoonekana na mtu mwingine yeyote.

Jeremiah 17:9. Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nami awezaye kuujua?

Niacheni niisafishe miyo yenu, iwe safi. Niacheni nizitakase nafsi zenu. Niacheni niwaweke tayari kusimama mbele yangu. Ni mimi tu niwezaye kutenda haya.

Ni mimi tu niwezaye kuwakamilisha kupitia damu yangu niliyotoa kugharamia dhambi zenu. Natamani kuwapa damu hii ili iwatakate na kuwafanya kuwa wasatafi.

Matendo ya Mitume 22:16. Basi sasa, unakawilia nani? Simama, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako ukiliita jina lake.

 Wana, wanangu, nawasuburi mje kwangu kwa toba, toba ya moyoni. Njooni kwa mwanga wangu: pokeeni wokovu wangu, wokovu nilioununua kwa damu yangu. Ni mimi tu pekee niwezaye kuwatendea haya. Niachieni maisha yenu yote. Msiogope. Dunia inaporomoka. Haina majibu yote, ukweli wowote haina. Siyo ya kutegemewa. Miye ndiye mwamba. Ni mimi tu niwezaye kuaminiwa na maisha yenu. Nipeni maisha yenu. Hata msipoelewa maana yake, niachieni maisha yenu.

Niachieni maisha yenu nami nitayachukua na kuwajali. Nitawafanya tunu yangu na kuwajaza na upendo wangu, Roho wangu, na amani yangu. Inayopita vyote. Amani msioyoweza kuelewa. Amani ya mungu. Itokayo kwa Mungu, Mungu Mtakatifu. Mnastahili amani kama hii ya milele. Ni mimi pekee ninayeweza kuwapa amani hii.

Hii ndio saa ya kunena imani yenu kwangu. Mnichague. Msiponichagua, mtakuwa mumemchagua adui wangu. Kuna mawili tu -- mawili tu. Aidha u nami, au unanipinga. Hakuna nafasi ya tatu. Msidanganywe. Hata mkiwa ukingoni, ninyi si wangu. Nataka mjitolee kikamilifu.

Njooni kwangu kwa toba iliyo kamilifu, na nitaziondoa dhambi zenu, jinsi mashariki ilivyo mbali na magharibi. Sitaziangalia tena. Nitawafanya wasafi. Tutashiriki katika uhusiano wa karibu na mtanijua na kunifahamu vyema. Natamani tujuane hivi.

Zaburi 103:12. Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.

Kwa hivyo njooni mpate kunijua. Ninastahili kuwa na uhusiano nanyi. Nitawaleta pahali pa amani na uelewano. Roho wangu atawaongoza na kuyafungua macho yenu ili mwone ukweli; ukweli unaoyakoa maisha yenu. Atawaonyesha wakati mlio ndani. Atawaonyesha ukweli kwa njia msioweza kuelewa, na mtaokolewa na kuwa na pahali katika ufalme wangu. Haya ndio matamanio yangu. Njooni muweze kumjua huyu Mungu wenu. Tetembee pamaja mkono kwa mkono. Nitawapeleka nje ya dunia hii. Wakati unakwisha. Nichagueni.

Ni mimi BWANA wenu na MWOKOZI wenu MKUU MASIYA Mfalme Mkarimu YAHUSHUA.

 

SURA YA 24: ACHENI KUPIGANA WENYEWE KWA WENYEWE

 Natuanze. Wanangu, leo nina maneno ya kuwapa. Yote si muonavyo. Mambo yatabadilika hivi karibuni. Wanangu, kuna kuwa giza. Kila kitu ni giza. Maisha myajuavyo yanabadilika sana. Hivi karibuni hakutakuwa na kurudi nyuma.

Hili ndili onyo langu. Nawapa maonyo makali ila ni wachache tu wanao yatilia maanami. Ni wachache sana wanaonisikiza. Mbona wanangu hawasikizi? Wako kwenye dunia yao-sio dunia yangu, sio mawazo yangu, sio maonyo yangu. Yasikitisha mno, wanangu. Siwapi maonyo kwa manufaa yangu bali ni kwa manufaa yenu. Ninafahamu yatakayo tendeka na niwataka mfahamu vile vile.

Mathayo Mtakatifu 6:24. Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili. Kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.

Wana, sitaki muwe gizani. Nawatakeni mjue ukweli. Nawataka muwe kwenye ukweli wa yale ambayo ya karibu kutukia. Nawaomba mwamke! Nuseni uovu…u kwenye hisia zenu. Kila kiti ni kiovu. Hakuna atakaye utakatifu. Kila mtu amepotea.

Isaya 53:6. Sisi sote kama kondoo tumepotea, kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe. Na BWANA ameweka juu yake maovu yetu sisi sote.

Bi arusi wangu pekee ndiye mwaminifu. Yeye pekee ananitazamia. Pekee ndiye anitakaye nirudi. Anitafuta kwa kila jambo na kwa kila pembe. Huyu ndiye bi arusi wangu, kanisa langu, kanisa langu la kweli.

Wana, acheni kuzozana. Mnaangamizana Acheni kubishana kuhusu maneno yangu. Huu sio wakati wa kuwa na hasira kwa ndugu au dada yako. Adui ameingia kati yenu na kuwadanganya. Anataka kuwaweka kiwango sawa naye. Naomba mwache ubishi usio na maana kati yenu na mpendane.

Yohana 13:34 Amri mpya nawapa, mpendane kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.

Hii siyo njia. Siyo njia yangu. Tubuni wanangu. Kisha muwaende wenzenu na kusuluhisha mambo. Sameheaneni. Muda unaisha. Msiache mambo madogo madogo yaliyo kati yenu. Yawaweke mbali na wokovu wangu wa milele.

Mathayo 6:14-15. Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.

Ninataka kuwaweka huru kutoka kwa dhambi hii. Hakuna dhambi duniani ambayo ni ya thamani kuu kukufanya uupoteze wokovu wako wa milele. Tafadhali likumbukeni jambo hili. Wana, upendo wangu ni mkuu, lakini siwezi kutozingatia dhambi. Kwa hivyo, tubuni leo na msameheane. Likimbilieni jambo hili msiache cho chote kibakie. Wasameheni wote, ndipo baba yenu aliye mbinguni, awasamehe. Hili ni jambo rahisi sana la kusamehe na kuacha machungu yaliyo mioyoni mwenu.

Niacheni niwaponye. Ziwekeni simanzi zenu mabegani mwangu na muniache niwaletee uponyaji. Ni mimi tu niwezaye kuyatenda haya. Njooni kwangu nami nitaichukua mizigo yenu. Nitafanya hiyo kwa hiari yangu.

Niacheni niyajenge maisha yenu na kuondoa uchungu wenu. Nileteeni uchungu wenu. Wasamehe walowakosea na mje kwangu kupata afueni kutoka kwa mizigo yenu. Ningependa kuwapa mioyo mikamilifu.

Lisomeni neno langu. Mimi ni Mungu wa urejesho. Niacheni niwarejeshe kwa ukamilifu na raha. Mimi ndimi nirejeshaye na kuweka kuwa kamilifu. Hakuna mwingine. Niacheni niwaonyeshe mapenzi ya dhati.

Yoeli 2:25 Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa. Nilituma kati yenu.

Ndiyo, hii saa inawadia ya kurudi kwangu. Niacheni niwasafishe na kuwarudishia uzima mpya ndani yangu. Niacheni niwatayarishe kwa kurudi kwangu. Nitayari. Mimi ndimi tumaini lenu, tumaini la pekee. Njooni kwangu. Huu ndio wakati. Msingojee sana. Mimi tu ndiye ninayestahili. Mwana Kondoo ndiye anayestahili. Njooni mikononi mwangu haraka.

Huyu ni BWANA wenu, YAHUSHUA.

 

SURA YA 25: SITAWACHUKUA IKIWA MNGALI MNA DHAMBI AMBAYO HUMJATUBU

Tuanze. Ni tayari kukupa maneno mengine mengi. wana, saa ya kurudi kwangu inakaribia. Itakuja kwa wakati uliopangwa.

Wengi wanadhani kuwa sitawahi kuja. Wengi wanadhani sitakuja hivi karibuni. Wanadhani kungali na miaka mingi sana inayosalia ndipo nije. Wanangu, naja hivi karibuni. Kurudi kwangu ku karibu. Hata mlangoni. Wengi watapatwa bila kutarajia. Wengi watakuwa wamelala, wamelala kiroho.

1 Wathesalonike 5:6. Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.

Hivi karibuni, wakati utafika. Wale wanaonitazamia na kuningojea watakuwa tayari. Wale wasio macho wataachwa ili wakabiliane na yajayo. Wakati u karibu sana.

Wana, mnafaa kuwa tayari. Msipatikane bila kujua. Sitaki kumuacha yeyote nyuma, ila ina huzunisha sana maana wengi wataachwa. Ni wakati wa kuhuzunisha sana. Nataka muamke. Mkaamini kuwa wakati huu kweli waja. Naja na hata ni mlangoni. Hivi karibuni, hakuna atakayeshangazwa na yajayo kwa maana ukweli utajulikana wakati watagundua kuwa yote ambayo niliwaambia ni ya kweli. Dunia itatambua kuwa mabadiliko makuu yametendeka. Hivi karibuni, dunia haitakuwa vile imekuwa. Itabadilika.

Wanangu, msikize kwa makini. Sitachukua yeyote ambaye angali na dhambi ambayo hajatubu. Siwezi kuwachukua. Haiwezakani. Kwa hivyo, njooni mbele zangu na mtubu.

Luka Mtakatifu 13:5 Nawaambia, sivyo lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.

Njooni msuluhishe mambo kati yenu nami. Natamani kuwaleta ufalmeni mwangu. Nataka kuwaokoa kutokana na maafa yajayo.  

Siwezi kuwachukua wasio wangu. Ikiwa hujaja mbele zangu na kunipa maisha yako basi wewe si wangu. Hili ni jambo la muhimu sana wanangu. Munahitaji kunipa maisha yenu. Niyaweke chini ya miguu yangu bila kusita. Huu ndio wakati wenu wakuja kwangu kwa unyenyekevu na toba. Nileteeni mahangaiko yenu yote. Nayataka maisha yenu. Nitayabadilisha maisha yenu ya mahangaiko na maisha ya upendo, furaha na ukamilifu. Karibuni, hivi karibuni, naja na ningewapenda muwe tayari. Wakati huu umewadia. Niruhusuni niwape ukamilifu wamaisha. Upendo wangu utazifunika dhambi zenu zote. Njooni kwangu. Nawangojea kwa mikono wazi. Mikono inayotamani kuwakumbatia na kuwapenda.

Mtakatifu Luka 5:31 Yesu akajibu akawambia, Wenya afya hawana haja na tabibu, isipokuwa walio hawawezi.

Msichelewe. Huu ni wakati muhimu sana. Sitachelewa kumtoa bi arusi wangu. Ni tayari kumpeleka nyumbani kwa majumba niliyo mtengenezea. Hapa ndipo atakapoenda ili awe salama. Kwa hivyo wanangu, jitayarisheni, maana kurudi kwangu ku karibu. Nazungumza nanyi kama BABA awapendaye na kuwajali. Nataka kuwaokoa niwaondoe kwenye dunia ambayo hivi karibuni itakua kama kichaa. Niacheni niwaonyeshe mlango wa kuwapeleka mahali salama. Huo mlango utafunguka hivi karibuni. Kisha utafunga. Kwa hivyo jitayarisheni. Ni tayari kuwapokea. Huyu ni BWANA MUNGU wenu kutoka mbinguni YAHUSHUA.

 

 

SURA YA 26: NITAZAMENI

Luka Mtakatifu 13:24-25. Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawambia ya kwamba wengi watataka kuingia wasiweze. Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako.

Natuanze tena. Wana, huyu ni BWANA wenu anayezungumza nanyi. Nawataka mnitazame mimi. Huu siyo wakati wa kukimbia hapa na pale na kutazama dunia. Huu ni wakati wa ustadi. Huu ni wakati wa kunitazamia mimi na kuwa macho kuhusu kurudi kwangu. Kila siku, wakati unakaribia.

Msiyapuuze maonyo yangu. Maonyo haya yanatokea pande zote. Natuma ujumbe kutoka pande zote. Ujumbe wangu unakuja kupitia mikasa, vita na uvumi kuhusu vita, kupitia kwa manabii wangu na wajumbe wangu, kupitia ishara kwenye mbingu na kupitia midomo ya watoto wachanga. Hamtakuwa na sababu yo yote mkiachwa. Hamtamlaumu ye yote ila ninyi wenyewe mkiachwa kuyakabili yajayo.

Kitabu changu kimeonyesha wazi nyakati hizi mnazoishi kwa sasa, na yale ambayo yanawadia kutendeka. Wana, mnahitaji kuamka na kufuata huu ukweli ambao ninawaambia. Msisimame kama watu ambao sijawapa chochote cha kuwaelekeza kwa uzima wa milele. Nimewapa pia maonyo. Nimewapa kitabu changu lakini ikiwa mtakataa kukifuata na kuyapuuza maneno yangu na maonyo ninayowapa, sitaweza kuwasaidia. Nimekuwa wazi sana na ujumbe wangu ninaowapa. Hamtakuwa na udhuru yoyote mtakaposimama mbele yangu ikiwa mtakataa kufuata niwaambiayo. Ninaweza kuwaomba ili myatilie maanani lakini mkikataa kunisikiza sitawalazimisha. Ni kwa hiari yenu kuamua. Uamuzi ni wenu.

2 Petero 3:3-4. Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao  tamaa zao wenyewe na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali hiyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.

Ni wachache sana watakaofanya uamuzi wa kweli au hata kufanya uamuzi wowote. Kutofanya uamuzi ni sawa na kumchagua adui wangu. La kuhuzunisha ni kuwa kuna wale ambao hawatafanya uamuzi wowote na wataendelea kuwa katika mamlaka na nguvu za adui wangu. Jambo hili linanihuzunisha mno kwa maana nililipa gharama kuu kwenye kilima cha Kalivari, ili wanangu wapate kuwa huru, huru kutoka kwa mitego ya Shetani na mitego yao wenyewe. Si vyema wanangu kuteseka bila sababu katika maisha haya na maisha yajayo bila matumaini na upendo wa milele.

Mathayo Mtakatifu 24:37-39. Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya gharika watu walivyokuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

Kwa hivyo wana, amkeni! Itwaeni zawadi hii yenye thamani, ambayo nawapa na mniruhusu nigharamie uhuru wenu. Ninaweza. Ninataka. Ni yangu kuwapa na ninawapa bure. Ni raha yangu kuwafanya muwe wazima, wenye amani na fahamu nzuri. Haya yote ni yenu ikiwa mtanijia na kujitolea kikamilifu. Mnipe uzima wenu. Niacheni niwe Bwana wenu. Niacheni niwajaze na Roho wangu na niwanifunike na damu yangu ndipo nifute orodha ya dhambi zenu.

Luka Mtakatifu 17:16. Akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.

Niacheni niwaonyeshe njia mtakayoitembelea ili muachilie njia za adui. Njooni kwangu na mpokee mioyo iliyotakaswa na kuoshwa kwa moto na maji ya neno langu. Ni yenu kutwaa.  

Yohana Mtakatifu 15:3. Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.

Achaneni na mipango yenu yote na mnipe maisha yenu, na mipango yenu yote. Nipeni maisha yenu. Nitayabadili maisha yenu na mipango yenu na mipango ambayo nilipanga tangu hapo awali kuhusu maisha yenu, nilipowaumba. Tembeeni katika mapenzi yangu. Msitende dhambi kwa kutembea kwenye njia na hiari zenu. Njooni kwenye mapenzi yangu ili muwe wakamilifu mbele zangu. Hii ndiyo hamu yangu kuhusu maisha yenu.

Mimi ni muumba wenu. Najua yaliyo bora kwenu. Njooni mpokee zawadi hii kuu—amani kwa muumba wenu. Wana, saa inayoyoma. Msipoteze wakati kufanya uamuzi wa kunifuata. Wakati huu ni muhimu. Sitaki mkumbane na wakati mgumu ujao duniani. Nifuateni na nitawaonyesha ukweli na kuyafungua macho yenu. Nitayafungua macho yenu kwa kuyatoa magamba machoni na kuwapa uhuru, na kuwaandaa ili mje nyumbani ili muwe salama nami.

Matendo ya mitume 9:17-18. Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani, akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu. Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa.

Nataka kuwaamsha. Hii ni hamu yangu. Mje mikononi mwangu. Msisite. Kusitasita ni hatari na kunaweza kuwafanya mpoteze wokovu wenu.

Maneno haya yanatoka kwa BABA ambaye anawajali na kuawapenda, YAHUSHUA.

 

 

SURA YA 27: HAMNA BUDI KUJITAYARISHA IKIWA MNATAKA KUJA NAMI

Natuanze. Wana, huyu ni BWANA wenu na nina maneno ya kuwanenea. Wakati unaisha. Hivi karibuni nitamjia bi arusi wangu ili nimlete mahali palipo salama. Atainuka kutoka duniani kwa ushindi na utukufu. Yeye ni mshindi wangu. Nitamleta kwangu na kumuinua ili tukutane hewani. Tukio hili linaitwa ‘Unyakuo’ au cho chote kile utakachoamua kuliita tukio hili. Hili tukio litatendeka hivi karibuni. Nitamvuta bi arusi wangu kutoka kwa minyororo ya dunia ambayo inaenda kombo – bila muelekeo; dunia ambayo inaishi mbali na MUNGU.

1 Wakorintho 15:51-52. Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.

Mimi ni MUNGU anayezuia matukioa mabaya duniani, na sasa dunia itaanza kuona maisha yatakavyokuwa bila mkono wangu mkuu wa ulinzi. Hivi karibuni yatatendeka. Wengi watashuhudia tukio hili kama wale walioachwa. Wachache watalishuhudia kama wale watakaochukuliwa kutoka duniani. Nataka muwe kati ya wale watakaochukuliwa kutoka duniani, ila ni sharti mjitayarishe ikiwa mnataka kutoka nami. Ni wale tu ambao wamejiosha na kuwa weupe kwa damu yangu ndio watakao kuja nami, nitakapo mwita bi arusi wangu juu. Ni wachache sana wanaokuja. Hii ni hatari, wanangu. Wengine wote watawachwa nyuma.

1 Yohana 1:7. Basi tukienda nuruni kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, mwana wake, yatusafisha dhambi yote.

Ni huzuni ulioje uwangojeao watakaoachwa nyuma! Usiwe mmoja wao. Si lazima uwe mmoja wao. Niwatengenezea njia. Nimewatengenezea mahali pa kupitia. Ni kupitia kwa damu yangu. 

Njia yako ni wazi na huru kupitia kwangu. Hakuna njia nyingine. Hakuna mwingine atakayewaokoa. Hakuna majibu kwingine. Ni hili tu: Njooni kwangu, na mjitolee kwangu. Msisite. Fanyeni hima kwa maana kurudi kwangu ku karibu. Kuweni na wakati wa kunijua mimi. Ni tayari na ninawasubiri. Upendo wangu wawangojea. Njooni kwangu kwa toba na unyenyekevu. Nitawatayarisha kupitia kuwafunika kwa damu yangu, na neno langu—kuoshwa kwa neno langu.

Waefeso 5:25-27. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyazi wala lo lote ka hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.

Njooni kwangu. Msipoteze wakati. Hii ndiyo saa ya kumchukua Mungu bila utani. Msingojee sana. Ni mimi BWANA MUNGU YAHUSHUA

 

SURA YA 28: UZIMA WENU WA MILELE U MASHAKANI

 Natuanze tena. Wakati wa u karibu wa kurudi kwangu. Unatimia. Kuna mengi mnayohitaji kufanya ili mjiandae. Nina mengi ninayotaka mfanye. Nawataka mjitolee kwangu na myatoe maisha yenu kwangu kikamilifu. Nataka mniachie kila kitu. Kujitolea nusu ni kama kukosa kujitolea. Myatafakari haya sana. Uzima wenu wa milele u mashakani. Bila kujitolea kikamilifu, ninyi si wangu. Haijalishi mnayoyasema au kufikiria. Ni kwa kujitolea kikamilifu ndiko kutakako dhihirisha kuwa mu wangu. Mkiangalia kushoto na kulia, mtapotoshwa. Msiwe hivyo. Muda unayoyoma. Wanangu, ni sharti muamke! Muwe macho!

Mathayo Mtakatifu 7:14. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.

Wakati waja wa kumuondoa bi arusi wangu, kumleta nyumbani, kumsindikiza nyumbani kwake kupya ambako ataishi nami milele, BWANA ARUSI WAKE. Natamani kumkumbatia, kumshika kwa karibu, kumpa mapenzi yangu, kumuhusudu na kumuonyesha mapenzi yangu. Hivi karibuni haya yatatendeka. Ni tayari na bi arusi wangu pia yu tayari. Ananisubiri kwa ustahamilivu. Bi arusi wangu ndiye nuru ya dunia. Anang’aa katika dunia yenye giza, na isiyopendeza. Yeye ndiye nuru ya mwisho. Nuru yake ni kuu na inaonyesha nuru yangu. Nuru ni ukweli—ukweli wangu unaodumu milele. Mengine yote ni uongo kutoka kwa adui wangu. Ameukanganya ulimwengu na uongo wake. Ulimwengu umedanganyika na watu hawauoni ukweli.

Yeremia 17:5-6. BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu Yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake, na moyoni mwake amemwacha Bwana. Maana atakuwa kama fukara nyikani, hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.

Wakati umewadia wa wanangu kuamka na kuukabili ukweli. Dunia inaisha. Kipindi kipya chaja: kipindi cha Mpinga Kristo na mabadiliko magumu yatafuata. Hakuna yeyote atakayekua salama, ila tu wafuasi wangu wa kweli ambao nitawapeleka nyumbani na kuwaweka mahali pa usalama. Hawa pekee ndio walio na ruhusa ya kutoshiriki kwa matukio yajayo—yale ambayo dunia itakumbana nayo pindi tu adui wangu ashikapo usukani na kuruhusiwa kutawala na kutamalaki. Ni siku ya huzuni tele.

Ufunuo 17:16-17. Na zile pembe kumi ulizoziona na huyo mnayama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto. Maana Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao hata maneno ya Mungu yatimizwe.

Huu utakuwa wakati mgumu sana kwa wanadamu. Shida kubwa yaja duniani. Saa hii yaja na yaja kwa kasi. Hivi karibuni, mambo yatabadilika. Nawataka ninyi wana mjitayarishe ili mwende juu nami. Nawataka mje nami. Mwaweza kuyaepuka haya yote ikiwa mtayafungua macho na kuja kwangu kwa unyenyekevu, toba na kujitolea. Natamani kuwachukua mikononi mwangu na kuwaokoa kutokana na simanzi ijayo. Hamu yangu kuu ni kuwaokoa kutoka kwa matatizo yajayo. Nawapa maneno mengi na ishara nyingi za kuwaleta kwa ukweli huu. Ni wachache sana wanaonisikiza. Wengi wangali wameolewa na dunia hii ya uovu ambayo ni kahaba. Ndiyo, wana. Ikiwa mngali mumeshikilia dunia na njia zake, mnafanya usherati kwangu na sitawaleta katika ufalme wangu. Kwa hivyo, ondokeni kwa dunia na njia za dunia. Dunia ni chafu bila maadili na yampinga Mungu, na siwezi kustahamili tena.

Ezekieli 16:35. Kwa sababu hiyo, Ewe kahaba, lisikie neno la BWANA; Bwana MUNGU asema hivi: Kwa sababu uchafu wako umemwagwa, na uchi wako umefunuliwa, kwa njia ya uzinzi wako pamoja na wapenzi wako; na kwa sababu ya vinyago vyote vya machukizo yako; na kwa sababu ya damu ya watoto wako, uliyowapa.

Wakati unaisha. Rudini kwa fikira zenu. Yafungueni macho yenu. Ziangalieni nyakati muishimo. Msidanganywe na yale myaonayo na kudhani kuwa kila kitu ki sawa. Nitawaleta ufalmeni mwangu na kwa uzima wangu wa milele. Jitoleeni kwangu. Nifanyeni niwe BWANA na MUNGU wenu. Wakati wa kuamua ni sasa. Msichelewe! Huyu ni BWANA wenu, YAHUSHUA.

Luka Mtakatifu 21:31-32. Nanyi kadhalika mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu. Amin, nawaambieni, kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie.

 

SURA YA 29: NI SHARTI MNIKIMBILIE SASA WALA SIO KUTEMBEA

Ndiyo binti, natuanze. Wanangu, huyu ni BWANA wenu anayezungumza nanyi. Nataka mjue ya kuwa naja hivi karibuni. Saa i mlangoni. Hivi karibuni, nitakuja kumchukua bi arusi wangu. Apendeza, uzuri wake wang’aa. Namwangalia kwa hamu na ninataka kumleta nyumbani kwa makao yake yaliyorembeka ambayo nimemwandalia. Saa hii inakimbia wanangu. Yafaa mjitayarishe. Yafaa mjiandae kwa upesi. Siku ya huzuni yaja. Hivi karibuni nitambeba bi arusi wangu. Nitampeleka kwa usalama. Ni dakika chache tu zilizosalia. Kurudi kwangu kwakaribia mlangoni. Kwa hivyo njooni mikononi mwangu. Ni karibu sana. Ni sharti mnikimbilie wala sio kutembea mkinijia. Msiwe walegevu wana. Myatilie maonyo yangu maanani. Nawalete mahali hapa. Wanangu, nawataka muamke, muutazame ukweli. Hivi karibuni saa hii itakuwa mlangoni. Nisikizeni wana, nawataka muamke. Kuna matatizo ambayo yaja, duniani. Yaja kama gari la moshi. Yateremka kwa kasi. Hakuna liwezalo kuyakomesha. Hakuna mwanamume, mwanamke, mtoto awezaye kukomesha yajayo. Kutakuwa na matokeo makali, kwa watakaokataa kuyasikiza maonyo yangu. Nimewaonya kwa njia ya ishara nyingi. Hakuna atakayekuwa na hudhuru ya kusema kwamba hakujua. Kila mmoja atawajibikia dhambi zake—jinsi nilivyosema katika kitabu changu.

Warumi 14: 12. Basi ni hiyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.

Mnaamua kucheza na dunia ila mjue kuwa sio kila kinga’acho ni dhahabu, wanangu. Dunia inang’aa na kuonekana mpya ila ni sumu tupu na yawapa kifo. Iwekeni dunia kando na kumtazama MUNGU wenu. Je, sistahili kufuatwa miye?

Yohana 12:25. Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalamisha hata uzima wa milele. 

Ndiyo. Niliwafilia kifo cha uchungu kwa msalaba muovu. Ulikuwa uchungu kweli. Ndiyo, nilimpa BABA yangu maisha yangu baada ya masaa mengi ya mateso katika mikono ya watu waovu, wapotovu, wenye chuki ambao walikuwa wanafanya mapenzi ya baba yao, adui yangu. Hii ndiyo gharama niliyolipia uhai na maisha yenu. Je, sistahili muda wenu, mapenzi yenu na kushughulikiwa miye?

Zaburi 22:12-16. Mafahali wengi wamenizunguka, walio hodari wa Bashani waminisonga; Wananifumbulia vinywa vyao, kama simba apapuraye na kunguruma. Nimemwagika kama maji, mifupa yangu yote imeteguka, Moyo wangu umekuwa kama nta, na kuyeyuka ndani ya mtima wangu. Nguvu zangu zimekauka kama gae, ulimi wangu waambatana na taya zangu. Unaniweka katika mavumbi ya mauti. Kwa maana mbwa wamenizunguka; kusanyiko la waovu wamenisonga; wamenizua mikono na miguu. Naweza kuihesabu mifupa yangu yote; wao wananitazama na kunikondolea macho. Wanagawanya nguo zangu na vazi langu wanalipigia kura.

Njooni kwangu. Nawaambia mje kwangu. Niacheni niwachukue mikononi mwangu, niwashike, niwapapase, kama wanangu. Mimi ni BABA yenu awapendaye. Hakuna upendo mkuu kuliko wangu. Hakuna huba kuu kuliko yangu. Msininyime upendo wenu. Njooni kwangu mkinyenyekea katika toba. Niacheni niwasafishe, muwe wasafi mbele yangu. Niacheni niijaze mioyo yenu na furaha na raha. Naweza. Nataka. Wakati ni huu. Msingojee wala kusita. Huu ndio wakati wa kurudi kwangu. Naja kuwaondoa. Niacheni niwajaze na ROHO wangu. Niwafanye wakamilifu ndani yangu. Wakati unaisha wana. Hivi karibuni hakutakuwa na wakati tena uliosalia. Kwa hivyo, msidharau toleo hili la wokovu wangu pamoja na damu niliyoimwaga ili mpate ukombozi na kuwa wakamilifu milele.

Mathayo Mtakatifu 25:46. Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.

Natamani kuwa na uhusiano wa karibu na wa ndani nanyi. Ni wenu mkiniuliza. Nitawapa. Natamani kuwa na uhusiano wa karibu nanyi. Hamu yangu ni kuwa nanyi wakati wote kwa undani. Mkija kwangu kwa njia hii, hata nami pia nitakuja kwenu. Neno langu linaonyesha kuwa nataka kuwa na uhusiano wa ndani nanyi. Nawataka mnitafute mahali patulivu ambapo tunaweza kushiriki pamoja. Wanangu, mahali hapa ndipo ninapoweza kuwapa mafunzo namna ninavyotaka muishi maisha yenu. Mkinijia na kuwa na uhusiano wa ndani nami nitawaonyesha mipango yangu niliyo nayo juu yenu, na jinsi ninavyotaka muishi maisha yenu. Ila kwanza, lazima muwe kwenye mapenzi yangu, na kuwa kwa mapenzi yangu, ni sharti myatoe maisha yenu kwangu. Maisha yenu yote. Msiache cho chote. Myafanye maisha yenu yawe yangu. Myatoe kote kote. Muache mambo mengine yote pamoja na dunia. Nawataka muache mambo yote ya dunia na muwe tayari kunifuata po pote niwapelekapo. Watu wengi hawataki kufanya hivi. Wengi wamekwamilia vitu wasivyotaka kuviachilia. Wanangu, ni vitu gani vinawatenganisha nami? Ni kazi zenu? Ni mali? Ni huduma? Ni wana wenu? Ni nini hasa kinachowatenganisha nami? Ni kitu gani kinachowachangamsha kuniliko?

Mathayo Mtakatifu 10:37-39. Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi hanistahili. Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.

Wana, msiponiweka wa kwanza, mtapoteza vyote vile vinavyowachangamsha na mimi pia mtanipoteza. Haya ni maneno yenye uzito lakini sina budi kuyasema. Nataka myasikie na kuangalia mliko ndani yangu. Mimi ni wa kwanza au wa mwisho maishani mwenu? Wanangu, pimeni nafasi zenu kwangu. Ni nafasi gani ninayoshikilia maishani mwenu? Wana, simameni karibu nami – natamani kuwaweka karibu moyoni mwangu. Saa ya kurudi kwangu yaja. Sitaki mbaki nyuma kwa mateso. Njooni na mtanipata. Kila wakati ni karibu nikiwasubiria mnifuate. Upendo wangu nu mkuu! Msikose kuufurahia upendo huu milele.

Huyu ni BWANA ARUSI WENU WA KIFAHARI YAHUSHUA

 

SURA YA 30: BI ARUSI WANGU APENDEZA KWA NJIA ZAKE ZOTE

Ndiyo binti, tuanze tena. Wanangu, ni mimi BWANA wenu. Nawasalimu katika jina la BABA YANGU ambaye ni BABA YENU pia. Wana, saa yangu ya kushuka chini ili kumtwaa bi arusi imefika. Apendeza kwa njia zake zote. Nafurahia kumwita wangu. Mpendwa wangu. Nitamchukua mikononi mwangu hivi karibuni. Atakuwa nami milele. Tutakuwa kama nyota, mimi naye. Upendo wetu hautakuwa na kikomo. Amani nimleteayo itadumu milele. Yeye ni bi arusi wangu mwema. Ananitii na anazipenda njia zangu. Ni mpendwa wangu naye hunifuata. Anatembea kwenye njia nyembamba. Anitazamia. Njia zake zapendeza. Yeye ndiye nuru ya mwisho iliosalia duniani. Anaonyesha dunia njia zangu. Dunia inaniona kupitia kwake. Anaonyesha yangu kwa ulimwengu. Njia zake ni za unyenyekevu na ana imani kama ya mtoto. Hii ni jinsi ya watu walio mbinguni. Saa ya kumtoa duniani ina karibia. Namchukua awe wangu. Namweka mahali pa usalama. Hivi karibuni atakuja nami mahali palipo salama ili asikumbane na mambo yajayo. Saa hii yaja, msiwe na tashwishi.

Mathayo Mtakatifu 18:3. Akasema, Amin nawaambia, msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Nawataka mjiandae na kuwa tayari jinsi bi arusi wangu alivyojiandaa. Amejitayarisha kwa kujisafisha katika damu yangu. Amejisafisha na hana doa wala kunyazi lolote. Yu tayari kuja katika mbingu zangu, kuwa pamoja nami na kufuarahia kuwepo kwangu.

Waefeso 5:26-27. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake ili maksudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.

Ni tayari anijie mawinguni, aje juu. Hii ni siri. Siri kubwa mno, kwa maana atabadilika. Atafanywa awe nilivyo na mwili mpya mtukufu. 

Mwili wake utabadiliki: usio na dosari, usioangamia, ulio na nuru ya milele, NURU YANGU. Atang’aa mbinguni. Atakuwa na utukufu na kung’aa kwa sababu atakuwa jinsi nilivyo. Mwili huu hautokufa wala kujua kifo. Ni chemichemi ya ujana wa milele. Ni mwili usio na mipaka. Wanangu wataifurahia miili yao mipya. Hawatakuwa na uchungu tena. Miili hii itakuwa ikibadilika kulingana na mazingira. Watasafiri mbinguni bila shida. Miili hii itaweza kutembea au kupaa. Watafanya ifanyayo miili ya binadamu na mengine mengi zaidi. Ni miili ya nuru. Miili hii haitakuwa na kizuizi cho chote kama miili ya binadamu ilivyo. Wanangu watakula na kufurahia chakula kama wafanyavyo sasa. Yote kuhusu miili hii mitukufu itawabumbwaza wanaoipokea. Yote yatabadilika kwa pumzi, kwa dakika moja. Wanangu watabadilika kwa dakika. Itawafanyikia haraka sana. Watashangazwa sana, haya ni badiliko ya milele. Jicho halijaona wala sikio kusikia kile ambacho nimewaandalia wanangu. Wanangu waaminifu.

1 Wakorintho 15:51-54. Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. Maana sharti huu uharibikao uvae kutoharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. Basi huu uharibikao utakapovaa kutoharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapa ndipo litakapokuwa lile neno liloandikwa, mauti imemezwa kwa kushinda.

Geukeni na kunitazama mimi. Msikose tukio hili na utukufu huu, nirudipo kumchukua bi arusi wangu. Tukio hili laja wana, jiandaeni – fanyeni maandalizi muwe macho, mnifuate. Ni wachache sana wanaonitazamia. Wengi wamenaswa na dunia. Dunia inaonekana tulivu na sawa lakini ni uongo. Dunia inahadaa. Ina uovu tele na mnaukumbatia. Inakwama kwenye uongo na kuufanya kama ukweli —hakuna ukweli duniani. Dunia inakuhadaa kuwa mambo ni shwari na hali si hivyo. Hivi karibuni mtayaelewa haya yote. Jitayarisheni. Sitasubiri muda mrefu. Kuja kwangu ku mlangoni. Nasimama mlangoni nikibisha. Niacheni niingie mioyoni mwenu. Saa inapita. Muda unakwisha. Ondokeni kwa ulegevu na mpige magoti. Tubuni dhambi zenu. Nipeni maisha yenu nami nitawasafisha na kuwafanya muwe tayari. Natamani kufanya hivi. Jitengeni na dunia. Jitengeni na dunia, ondokeni. Dunia ni kifo. Haitaendelea bila mimi. Maangamizi yake yametokana na kunipa mimi kisogo na kuendea mambo maovu.

1 Wathesalonike 5:23. Mungu wa amani Mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe muwe kamili bila lawama wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.

La wana, ni sharti muamue. Mtaenda na dunia au mtakuja nami? Ni uamuzi wenu. Siwezi kuwaamulia. Niwezalo ni kuwaomba tu mje kwangu. Nawataka muwe upande wangu milele. Natamani muwe nami mbinguni. Ila ni uamuzi wenu. Mjitolee kwangu ama mbaki nyuma. Naungojea uamuzi wenu. Upendo wangu ni mtulivu. Mimi ni MUNGU asiyedanganya. Nijieni kabla ya muda kwisha.

Ni MIMI MKUU YAHUSHUA.

 

 

SURA YA 31: NI WACHACHE SANA WANAONIABUDU NA KUTUBU KWANGU

Haya, natuanze (Februari 28, 2012). Wanangu niwahusuduo, saa ya kurudi kwangu inawadia. Ni sharti mjiandae. Ni sharti mjitayarishe. Jifunikeni kwa damu yangu. Dunia inaisha. Inafikia kikomo. Inabadilika. Ina uozo wa maadili. Inanuka kwa uovu mtupu. Inanigeuka mimi MUNGU wake. Ni wachache sana wanifuatao kwa kiwango nihitajicho kutoka kwao. Ni wachache sana wajitupao miguuni pangu kuniabudu na kutubu kwangu. Ni wachache sana watakao kunifuata ko kote kule nitakako waende bila kusita.

Marko Mtakatifu 8:34. Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.

Wengi wameshikwa duniani wakifuata vitu vya duniani. Hamjui kuwa dunia hii ina uadui nami? Sitaistahamili dunia hii tena. Sitairuhusu dunia iendelee inavyoendelea. Hivi karibuni nitamwondoa bi arusi wangu na kuwavuta wanangu niwapeleke kwa usalama. Bi arusi wangu apendeza na ni tayari kumpokea kwa nyumba niliyomwandalia juu mbinguni. Hakika tukio hili li karibu kutendeka. Wanangu mwahitaji kuelewa mambo haya. Yafaa mwelewe ukweli huu. Wengi wanasinzia, wamelala fofofo. Wanaenda mbali nami. Wanaanguka mikononi mwa adui na hivi karibuni kama ndege ambaye anashikwa mtegoni mwa wawindaji watashikwa.

Zaburi 124:7. Nafsi yetu imeokoka kama ndege katika mtego wa wawindaji.

Amkeni wanangu, muone ukweli. Amkeni na mtizame, naja! Amkeni kabla hamjapatwa na kuniacha kabisa. Sasa yangu ya kurudi imefika na wengi wangali wanalala –wamelala fofofo. Huu si wakati wa kupatikana mkiwa hamjajitayarisha! Amkeni! Hivi karibuni adui atawaweka mahali awatakapo ninyi nyote muwe, msiponijia na kujitolea kwangu kabisa. Huu ni wakati wakumtii MUNGUwenu kabisa. Mimi ni MUNGU mvumilivu, ila uvumilivu wangu karibuni utakwisha. Sitastahamili dunia hii ambayo yafa. Yafa kwa sababu inamkataa MUNGU aliyeiumba. Kila pembe ya dunia imenikataa. Nimekataliwa kote. Dunia sasa inakumbatia uovu. Inakumbatia uovu, inalala na uovu, inaamka kutenda uovu na kulala na uovu. Bi arusi wangu pekee ndiye anifuataye. Yeye tu ndiye mwaminifu. Yeye tu ndiye aliye na mikono misafi. Yeye tu pekee ndiye anayenifuata na amejitenga na dunia. Ni yeye tu pekee ambaye hajachafua nguo zake kwa kushiriki kwa mambo ya dunia. Yeye ni nuru yangu katika dunia iliyojaa giza. Anang’aa gizani. Nuru yake inaweka kimulimuli kwa dunia iliyojaa giza tele, dunia ambayo inajaa giza kila siku. Hivi karibuni nuru hii itazimika kwa maana ni sharti nimuondoe nimpeleke mahali palipo salama. Kisha dunia itaendelea kuwa na giza bila matumaini yo yote. Huu ni wakati mgumu wanangu. Ni sharti mje kwa nuru yangu wakati mungali na nafasi. Wakati uliobaki ni mdogo mno. Saa i karibu kwisha. Mshale wa dakika unakaribia sa sita za usiku. Msiyapuuze maneno haya ninayowaambia. Ni kwa manufaa yenu: Kuwaepusha na madhara. Kuwaepusha na yajao.

Yohana Mtakatifu 8:12. Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.

Wanangu, nawapenda jinsi baba mpendwa anavyowapenda wanawe. Nawataka mje mikononi mwangu ambamo mtakuwa salama. Ni kupitia kwangu tu ndipo mtapata usalama. Kuwa ndani yangu na kupitia kwangu ndiko kutawaokoa. Hakuna njia nyingine. Mkigeukia dunia kuwapa majibu, mtapotoshwa na uongozi wa watu wasionijua wala kuujua ukweli wangu. Hii saa inakaribia. Jitengeni na dunia. Isafisheni mikono yenu kuondoa uchafu dunia inayowapa. Dunia inawatoa kwangu. Njooni karibu nami. Nitazameni mimi. Mimi ndiye mwokozi wa mwisho kabla dunia kuisha. Msikose wokovu huu ambao ndio wa kipekee na utakao wapeleka kwa usalama.

 Waraka wa Yakobo 4:8. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.

Jitayarisheni kuwa mmoja wa bi arusi wangu. Njooni kwangu kwa kujitolea kikamilifu. Maisha yenu yote yatoeni kwangu. Nipeni kila kitu chenu na utii wenu. Nitawaongoza kwa usalama. Hii ndiyo ahadi yangu kwenu: usalama na uhuru kutokana na yale yatakayo kuja duniani hivi karibuni. Msikatae. Msiishi ili kujuta uamuzi wenu siku moja. Mimi hulitimiza neno langu. Naweza kuwapeleka kwenye usalama. Mimi ni MUNGU mwenye nguvu. Ni mwaminifu. Msifadhaike mioyoni mwenu. Ikimbilieni mikono yangu ya wokovu.

MUNGU wenu mwaminifu, YAHUSHUA.

 

SURA YA 32: NI KARIBU KUMUONDOA BI ARUSI NA KUMPELEKA MAHALI PA USALAMA

Binti yangu, hebu tuanze (Februari 28, 2012). Wana, mimi ni MUNGU wenu. Mimi ni MUNGU anayewajali sana. Nawatakia tu mema. Sasa wanangu, nataka myasikie maneno yangu. Nisikizeni kwa makini. Dunia i karibu kuangamia. Hivi karibuni dunia itageuka. Ni mengi sana yatatendeka ndani na pande zote na ni machache tu yatakayokuwa mema. Nauondoa mkono wangu wa kinga kutoka duniani, kwa maana dunia imeniasi. Inatembea kinyume na moyo wangu, njia zangu, ukweli wangu. Ni makuruhi kwangu. Ni karibu kuwaruhusu mbwa na shetani, kurithi dunia.

Zaburi 22:16. Kwa maana mbwa wamenizunguka, kusanyiko la waovu wamenisonga; wanizua mikono na miguu.

Tukio li karibu. Wanangu, siku zijazo zitakuwa siku za giza. Sistahamili uovu tena duniani. Ni karibu kumuondoa bi arusi wangu na kumpeleka mahali pa usalama. Hivi karibuni nitamuondoa. Sitavumilia yanayotendeka duniani tena. Ni karibu kuitema dunia. Uovu ambao umetanda duniani ni uvundo usoni mwangu. Siwezi kuutazama. Sitawaruhusu wapendwa wangu waendelee kustahamili dunia. Kanisa langu li karibu kuondolewa ili lipelekwe kwa usalama. Saa hii inakaribia kwa upesi sana. Enyi wana, mbona mna tashwishi? Muamini musiamini, tukio hili litatendeka. Ni lazima litendeke kama ilivyo kwenye kitabu changu. Nimewambia ukweli. Nimewaeleza kuhusu siku za mwisho kitabuni mwangu. Yasomeni maneno yangu. Jizoezeni na kitabu changu. Myasome maneno kwa makini. Mtaona kuwa hizi ni siku za mwisho na kurudi kwangu ku karibu. Enyi wana, acheni kujadiliana. Njooni mnitafute. Njooni kwangu na mioyo mikunjufu nami nitawaonyesha ukweli. Natamani kuwafichulia ukweli. Mimi siwapotoshi wanangu. Wakiamua kutonifuata basi siwezi kuwafichulia ukweli. Wataendelea kwenda kwenye uchochoro usotoka, na njia za kuangamiza. Njooni nami ili mpate njia. Nitawaongoza kwa njia yangu nyembamba. Ni wachache wanaoipata. Wanangu, wachache wanaitafuta njia hii. Msiwe miongoni mwa wale wengi wasioipata njia hii. Kuna wengi sana ambao wamepotea njia. Wengi sana walio kwa njia pana ambayo itawaangamiza.

Mathayo Mtakatifu 7:13. Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.

Jirudini wanangu. Changamkeni. Nitafuteni kwa bidii. Hakuna njia zingine ziendazo kwa uhuru na uzima wa milele. Saa ni hii. Kimbilieni mikononi mwangu. Msisite. Kusita kutasababisha mwisho wenu. Nataka kuwaokoa. Jitoleeni kwangu kwa kila njia. Nipeeni maisha yenu yote. Kutojitolea kikamilifu hakutoshi. Njooni kwangu na kuyatoa maisha yenu. Nitayapokea na kuwatukuza kwa ajili ya mipango yangu ya ninyi kunitumikia kisha mje kufurahia mbinguni milele.

Yeremia 30:19. Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge.

Saa hii inakwisha. Adui wangu ameanza kujitokeza. Hivi karibuni nyote mtajua kuwa mnaishi kwa wakati gani; ila huenda ikawa mumechelewa sana kuokolewa na mtakuwa mumepoteza nafasi ya kuokolewa. Wanangu, najaribu kuwaamsha na kuwaletea ukweli. Nitafanya nini ili mnisikize? Mkingoja sana kunijia mtaachwa nyuma. Itanibidi niwaache nyuma. Msiache jambo hili litendeke. Kutubu, kujitolea na kunisongea: Haya matatu ndiyo ninayotamani kwenu. Haya ndiyo mnayohitaji ili muingie katika ufalme wangu. Kitabu changu si kinanena hivi? Njooni upesi bila kuchelewa. Njooni na nitawasafisha na damu yangu na mtakuwa tayari kusimama mbele yangu na kupokelewa ufalmeni mwangu, ufalme wangu wa milele.

Ufunuo wa Yohana 1:5. Tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake.

Wakati unakwisha. Msipoteze hata dakika nyingine moja duniani humu. Huyu ni BWANA na MFALME wenu anayenena nanyi. Aliye juu na mwenye nguvu, aliye na mamlaka ya milele BWANA YAHUSHUA.

 

SURA YA 33: AIDHA MNIPE NAFASI YA KWANZA AU MSINIPE NAFASI YO YOTE ILE

Hebu tuanze (Machi 1, 2012). Wana, huyu ni Bwana wenu. Nina maneno mapya ambayo nataka kuwaelezea: Wanangu, kuna kipindi kipya ambacho kinataka kuanza duniani. Kipindi cha uovu. Watu waovu, nyakati mbovu. Ni sharti mjitayarishe kuondoka nami. Nawataka muwe tayari. Nitahitajika kumkuta bi arusi nimuondoe katika dunia hii mbovu na kumpeleka kwa usalama. Siwezi kumueka hapa duniani tena, kwa sababu hivi karibuni dunia hii itakuwa mbovu na isiyopendeza. Bi arusi ni sharti afichwe kwa usalama. Kisha dunia itaanza uovu wake kwa watakaobaki. Hivi karibuni, tukio hili litatendeka. Hata sasa tufani zote zajaa ili kuanzisha tufani kuu ya uharibifu, uoga mkuu ambao utawashinda wanadamu ambao watachagua kwenda kinyume nami. Ni sharti nipewe nafasi ya kwanza maishani mwenu ili mzuie tisho hili lijalo.

Mimi si Mungu anayetamani kuwaona wanawe wakiteseka, ila mkikataa kuniweka juu ya miungu mnayoiweka mioyoni mwenu, basi hivi karibuni mtajifunza maana ya kumkataa MUNGU wenu, MUUMBA wenu. Mimi si Mungu wa kufanyiwa mzaha. Nataka nipewe nafasi ya kwanza au nisipewe nafasi yo yote ile. Sitaki kupewa nafasi ya pili au ya tatu kwa orodha zenu. Niliwaumba kwa manufaa yangu. Mniabudu, mnitukuze na kunijua. Natamani kuwa na uhusiano wa karibu sana nanyi. Mkiamua kutonijua kwa njia hii, basi mtapata njia zenu na tutaachania hapa. Nendeni mhusiane na adui wangu mahali pake pa milele. Mimi ni MUNGU aliye na wivu. Sikuwaumba ili nishiriki nanyi na adui wangu.

Kumbukumbu La Torati 32:16. Wakamtia wivu kwa miungu migeni. Wakamkasirisha kwa machukizo.

Aidha mnataka kuwa wangu tu au mwaweza kuifuata ile njia pana itakayo wapeleka upotevuni ambako wengine tayari wameshaenda huko. Ni wachache sana wanaotaka kunijua kuliko kufuata mambo ya dunia. Je, ni wapi maishani mwenu? Sistahili kupewa nafasi ya kwanza maishani mwenu? Niliwafia wanangu kifo kiovu cha uchungu mwingi! Niliwaumba na nikawapa uhai. Nawahimili kila siku. Wanangu, hivi karibuni itabidi muamue. Mnataka amani, utulivu, na upendo wangu? Mnataka hakikisho langu la kuwapeleka kwa usalama kutoka kwa dunia ambayo inakwisha? Basi hii ndio saa ambayo mtaamua mtakalofanya. Mtamkubali vipi Mungu wenu? Kwa upendo na utiifu au kwa uvuguvugu?

Wafilipi 2:8. Tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.

Nawataka muamue. Mtajitolea kufa kwa ajili ya miili yenu na kunitolea yote? Nawangojea mje kwangu, mtubu ili niwafunike kwa damu yangu. Ni kwa kupitia damu yangu tu ndipo mtaokoka. Kwa dhabihu niliyotoa msalabani. Mkikubali zawadi hii ya gharama ya damu yangu, mtubu dhambi zenu kwa mioyo mikunjufu, myatoe maisha yenu kwangu na kunifuata bila kusita, nitayabadilisha maisha yenu, niwasafishe na kuwaandaa kuingia kwa ufalme wangu. Niwaweke kuwa tayari kuja nami. Zingatieni sana haya. Wana, msingojee sana. Kungojea ili kuona litakalotokea na kutoamua haraka kwaweza kusababisha kutoona niliyowaandalia kwa uzima ujao. Msiwe wajinga. Jirudini. Kuweni tayari. Nataka muokoke kutoka kwa tisho lijalo. Nawaombeeni. Nawaombeeni kwa baba yangu kwa ajili yenu. Wana, wakati huu unadidimia. Nawataka mfanya uamuzi. NITAMJIA BI ARUSI WANGU! Msikose kushiriki. Msikose yote niliyowaandalia. Sidanganyi. Nitashinda na kanisa langu pia litashinda! Kwa hivyo, ni sharti myatilie maanani ninayowambia. Ni mimi NIKO ambaye NIKO. NI BWANA YAHUSHUA ambaye ni mwaminifu kwa ukombozi.

 

SURA YA 34: KUNA DHIKI YAJA—DHIKI KUU.

 Natuanze (Machi 2, 2012). Wanangu, ni mimi BWANA wenu. Nina maneno mapya ya kuwapa. Wana, huu ni wakati wa kutilia maanani. Kuna simanzi kuu yaja duniani. Kutakuwa na hatari kubwa na huzuni. Shida hizi tayari zimeanza. Dhambi imeenea miongoni mwa wanadamu wote. Msifadhaike, nimeshinda dunia. Naja kumuondoa bi arusi nimpeleke mahali pa usalama. Ni mrembo na mzuri ajabu. Anatazamia kurudi kwangu. Kurudi kwangu hivi karibuni. Ananitazama mimi pekee. Nampenda kwa moyo wangu wote. Namkumbatia kwa macho yangu. Namtazama po pote aendapo. Hatoki machoni pangu. Hivi karibuni atakuwa nami mbinguni kwa usalama huku dunia atakayoiacha ikiwa inapasuka.

Yohana 16:33. Hayo nimewambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwengu unayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.

Tukio hili limeanza kujitokeza wanangu. Kuna dhiki yaja – dhiki kuu. Dunia haijawahi kuona tukio kama hili. Ninyi nyote hamtilii maanani maonyo yangu, ishara zangu, kitabu changu. Je mnaelewa kuwa mashaka yaja duniani? Yaja na hakuna binadamu yeyote awezaye kukomesha. Chanzo ni ulimwengu huu ambao umemkataa MUNGU wake. Dunia haijali kunihusu au kuhusu njia zangu. Kwa hivyo ni sharti niuondoe mkono wangu wa kinga na kumuondoa bi arusi wangu. Hivi karibuni, dunia itaelewa maana ya hofu kuu.

1 Yohana 4:1-8. Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. Katika hili mwamjua Roho Wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mugu. Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya Mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani. Ninyi watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni Mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. Hao ni wa dunia; kwa hivyo wanena ya dunia na dunia huwasikia. Sisi twatokana na Mungu. Yeye amjuaye Mungu atusikia, yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Katika hili twamjua Roho wa kweli, na roho ya upotevu. Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye amjua Mungu. Yeye asiyependa hakumjua Mungu, kwa maana Mungi ni upendo.

Sitawadanganya enyi wana. Mimi ni MUNGU. Dunia hii haitakuwa mahali ambapo mtatamani kubakia kuona yatayotokea baada ya tukio hilo. Hamtaweza kustahamili yajayo ikiwa mnataka kuwa ndani yangu. Wote watakao nikiri baada ya bi arusi wangu kuondolewa watakufa kwa ajili ya imani yao. Utakuwa wakati mgumu kwa wanangu. Msiwe wapumbavu kufikiria visivyo.

2 Timotheo 3:12. Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.

Sitadhihakiwa. Dunia haiwezi kuendelea jinsi ilivyo ikiamini kuwa hakutakuwa na matokeo. Nimechoka kukinga na kujali juu ya dunia ambayo inanidhihaki na kunichukia. Enzi hii i karibu kwisha. Hivi karibuni nitaiacha dunia ifanye itakavyo. Itakuwa dunia bila Mungu wao ambaye anaweza kuzuia maovu ambayo yatendeka kutotendeka. Dunia hainidhamini mimi kama Mungu wake. Kwa hivyo nitaiacha ili ipate kile ambacho inatamani. Ijiendeshe bila mimi Mungu Mtakatifu. Dira yake. Ndipo dunia itagundua umuhimu wa kuzishika njia zangu, sheria zangu, na kuzifuata njia zangu za milele. Wanangu watakaoachwa watashuhudia dunia isiyo na kizuizi. Utakuwa wakati mbaya kwa wanadamu. Msiachwe nyuma. Njooni kwangu. Msingojee. Jiosheni kwa damu yangu na kwa neno langu. Lisomeni neno langu. Tubuni na kuyatoa maisha yenu kwangu. Niacheni niwaokoe kutoka kwa yajayo. Ninataka. Muda ni mfupi. Fanyeni hima. Hii ndiyo saa ya kukimbilia mikononi mwangu. Upendo wangu wawangojea. Niacheni niwaokoe kutokana na maovu yajayo. Njooni niwafunike na damu yangu ili muwe salama. Nina haja ya kuwaokoa. Maneno haya ni ya kweli na halisi. Huyu ni BWANA wenu, YAHUSHUA, MKUU WA KUOKOA.

 

SURA YA 35: HAKUNA MANUFAA YOYOTE KUIKIMBIZA DUNIA INAYOKUFA

Natuanze tena. Wana, huyu ni BWANA wenu anayezungumza nanyi. Wanangu, naja hivi karibuni kwa hivyo msifadhaishwe. Dunia hii haina wakati wa kuyarekebisha mambo. Hivi karibuni, watakaokataa kurekebisha mambo kupitia kwa njia ya kutubu na kujitolea kwangu kikamilifu watateseka. Adui wangu ana kiu ya damu na hana huruma. Dunia itaona uovu ambao haijawahi kuona tangu awali. Wakati huu unakaribia kwa upesi. Sistahamili tena dunia hii mbovu na sugu. Nimesikia na kuona ya kutosha. Ni dunia inayomkataa Mungu wake na kuzipa kisogo njia zake na ukweli wake.

Yakubu 4:4. Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu?

Wana, mnaongozwa na vipofu ikiwa mtaendelea kukimbia ovyo ovyo mkitafuta mambo ya dunia. Hakuna manufaa yo yote kwa kuikimbiza dunia ambayo yafa. Haina mwelekeo wa kiadili. Ni sharti muwe mnayaona haya sasa. Ukubalini ukweli. Hakuna matumaini kwa dunia hii ambayo yafa kwa kumkataa Muumba wake. Kuweni macho. Yafungueni macho yenu. Mnaongozwa mbali na njia yangu nyembamba. Wana, ni wachache sana wanaoipitia njia hii nyembamba. Amkeni! Safisheni macho yenu na kuyatoa magamba ambayo yanawafanya msione. Njooni kwangu niwape macho ya kiroho. Niacheni niwaonyeshe ukweli. Acheni kucheza na adui mkidhani ni mchezo mwema. Ni muuaji. Atawashambulia wakati ambao hamtarajii. Hamwezi kumshinda bila mimi. Ni lazima mnisongelee ili niwakinge. Mtakuwa salama tu mnaponisongelea. Mtanusurika tu ikiwa mtakisoma kitabu changu na kuwa na uhusiano nami. Je, mnayaelewa haya? Msijidanganye. Msiwe wapumbavu. Moyo wa mwanadamu ni mdanganyifu. Adui wangu ni mjanja sana. Ninyi hamwezi kukabiliana na ujanja wake. Ni uhusiano kati yangu nanyi ndio unaoweza kuwapa ushindi ikiwa mu karibu nami, karibu sana, adui hatawakaribia kwa maana giza haliwezi kustahamili nuru. Kwa hivyo, nipeni maisha yenu na mipango yenu. Nipeni ili niyageuze majivu kuwa uzuri. Niacheni niwaonyeshe mapenzi yangu kwa maisha yenu. Ninaweza kuwatendea. Ni tayari kuwatendea. Ni hamu yangu ninyi muwe kwa mapenzi yangu. Hamu yangu ni kuwaosha kwa damu yangu na kuwaleta karibu nami jinsi mama ampendavyo mwanawe, hivyo ndivyo natamani kuwashughulikia.

Isaya 66:13. Mfano wa mtu ambaye mama yake amfariji, ndivyo nitakavyowafariji ninyi; nanyi mtafarijiwa katika Yerusalemu.

Mathayo Mtakatifu 23:37. Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!

Wana, saa hii ya kurudi kwangu inakaribia. Hamtazami. Mtaachwa. Nawajia tu wanangu ambao wanatazamia kurudi kwangu, wanaotamani kunitafuta kwa uhusiano wa ndani. Hawa ndio wajao nami. Wengine wote, watabaki. Wengi kati yao watapotea kwa maangamizi ya ghafula. Huu ni wakati wa kutilia maanani maonyo haya. Someni kitabu changu. Zifungueni kurasa zake. Ombeni Roho wangu Mtakatifu awaongoze katika ukweli. Wakati unaisha. Msipoteze hata dakika moja mkikimbiza dunia ambayo inanichukia, Mungu wenu. Mnaelekea kwa upande wa mauti. Jirudini. Nitafuteni. Mtafuteni Roho wangu; mtafuteni baba yangu, tutafuteni. Sisi ni kitu kimoja na sote tunataka kuwaokoa. Wakati wa kurudi kwangu umewadia. Msikose wokovu wangu. Huyu ni BWANA WENU YAHUSHUA, awapendaye kwa dhati.  

 

SURA YA 36: WENGI WADHANIAO KUWA WA TAYARI WAJIDANGANYA

Natuanze binti yangu (Machi 4, 2012). Sikiza kwa makini ninapokupa maneno haya mwanagu, huyu ni BWANA. Tafadhali yaandike maneno haya: wakati wa kurudi kwangu unakaribia. Wengi wangali hawatazamii. Wengi wana pazia za macho na wanakataa kusikiliza niwaambiayo. Saa ya kurudi kwangu yaja haraka. Ni sharti mjitayarishe wanangu. Ni sharti mjiandae. Kuweni macho mkitazama. Ni muhimu kufanya maandalizi. Wale wanaotazamia ndio tu watakaochukuliwa. Wale walio na haja ya kujua kurudi kwangu ndio watakaochukuliwa pekee yao. Wale wasiojali na wasio kaa kwenye roho wangu watabaki na kukabiliana na uovu. Wengi watashangaa kuwa wameachwa. Wengi watashtuka kuona kuwa wameachwa. Wengi wanaofikiria kuwa wa tayari watashangaa kuona wameachwa. Wengi wadhaniao kuwa wa tayari wajidanganya. Hawako tayari hata kidogo. Wamefungwa na vitu vya dunia. Fikira zao zi kwenye mambo ya dunia. Hawajali kutazamia kurudi kwangu. Wanajishughulisha na mambo ya dunia. Hawana wakati nami. Hawanitazamii.

Wanakejeli na kuwatesa wanitazamiao. Watashikwa na bumbwazi watakapoachwa nyuma wakidhani kuwa wananijua. Hawanijui hata kidogo. Wanadhani tu wananijua. Mioyo yao i mbali nami. Hawaji kwangu mahali pa siri. Wanayakimbilia mambo ya dunia. Macho yao hayanitazamii. Wanapenda kushika na kushiriki na mambo ya dunia. Wanapangia mambo yajao. Wanafanya mipango ambayo haitatendeka. Hawaniulizi kuhusu mipango hii. Wangeniuliza ningewaambia wanitazame mimi, waje karibu nami, na kuniachia mipango yao. Hili ndilo ninalohitaji. Mjitolee kwangu kikamilifu. Iwekeni mipango yenu miguuni pangu. Nipeni maisha yenu na mipango yenu ya siku zijazo. Mimi tu ndiye ninayeelewa mambo yajayo. Mipango yote mliyonayo yaweza kuvunjika wakati wowote. Mbona msiniache niwapangie mipango yangu niliyonayo kuhusu maisha yenu? Najua yaliyomema kwenu. Najua mwanzo na mwisho. Mimi ni ALFA na OMEGA. 

Ufunuo wa Yohana 22:13. Mimi ni ALFA na OMEGA, Mwanzo na Mwisho, wa Kwanza na wa Mwisho.

Mimi ni muumba wa jua, mwezi, na nyota. Mnadhani siwezi kujali kuhusu maisha yenu ya baadaye? Ninaweza kuwaleta ufalmeni mwangu ikiwa mtanipa maisha yenu. Nitawapa amani na usalama, nitawabeba hadi mahali pa usalama. Mtaishi kwa amani mkijua kuwa mipango yangu kwenu ni miema na nitaitimiza. Mtakuwa na usalama huu ikiwa mtakaa ndani ya mapenzi yangu, maishani mwenu. Hamtakuwa na wasiwasi tena mkiwa ndani ya mapenzi yangu. Achilieni mipango yenu na maisha yenu. Itawaongoza tu kwa uteketezi. Nitoleeni kila kitu na mwingie kwa mapenzi yangu. Mapenzi yangu kamili. Muachieni ajuaye mwanzo na mwisho ayaongoze maisha yenu. Mimi ni MUNGU wenu aishiye milele. Nitawaleta kwa ufalme wangu wa milele. Ni wenu mkiuliza.

Ufunuo wa Yohana 21:6. Ananiambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, chemichemi ya maji ya uzima bure.

Jitoleeni, tubuni, na mnifanye kuwa wenu. Mnijue. Nitaufungua moyo wangu kwenu. Natamani kutembea nanyi. Hamtakuwa pekee yenu. Kwa hivyo, wakati wa kunipa yote ni sasa. Hii ndiyo saa. Chagueni kwa hekima. Kuna nia nyingi. Njia moja tu ndiyo ya kweli, njia moja tu ndiyo nyoofu. Mnijue na nitawaongoza kwa njia nyoofu. Hii ni tamaa yangu. Kuwaongoza.

Waebrania 12:13. Mkaifanyie miguu yenu njia za kunyooka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.

Hivi karibuni saa itagonga saa sita za usiku. Ikimbilieni mikono yangu. Mikono salama. Niacheni niwaokoe. Chagueni haraka. Yanihuzunisha kumwacha ye yote ila chaguo ni lenu. Msisite kuupokea upendo wangu.

YAHUSHUA, MUNGU wa upendo mkuu.

1 Yohana 4:16. Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.

 

SURA YA 37: MNA WAKATI MDOGO SANA ULIOBAKI

Natuanze. Nitakupa maneno mengine: Wana, ni mimi BWANA wenu na nina maneno ya kuwapa.

Saa inachelewa. Nuru iliyobaki kwa siku ni ndogo sana. Ni sharti mjitayarishe. Jitayarisheni kwa maana wakati wa kurudi kwangu u karibu sana. Unatimia. Ni wachache sana walio tayari na wangojao. Ni wachache sana wanaojali kujitayarisha. Wengi wamechagua kutosikiza maonyo yangu. Wengi hawajali kuhusu yajao. Saa inakaribia. Nawataka muwe macho na kuwa tayari. Msipofanya hivyo, mtapatwa bila kujihadhari. Ikiwa hamtazami, hamtayaona yajayo. Wale wanaotazamia ndio watakao kuwa macho. Hao pekee ndio watakaokuwa wamejiandaa. Utajiandaa kivipi ikiwa hautazamii? Wale tu ambao wamejiandaa na kujitayarisha ndio watakaoenda pekee yao. Wengine wote watakuja na taa zisizo jaa mafuta.

Mathayo Mtakatifu 25:7-10. Mara wakaondoka wanawali wale wote wakitengeneza taa zao. Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, sivyo; hayatutoshi sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie. Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.

Huu si wakati wa kusinzia wanangu. Hii siyo saa ya kulala. Siji kuwachukua wale ambao hawawezi hata kukesha wakinitazamia. Wale walalao wataamka na kukumbana na tisho wasiloweza kulikabili. Ni wakati wa huzuni sana kwa kanisa langu linalo lala.

Waebrania 9:28. Kadhalika Kristo naye, akishakutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi, atatokea mara ya pili pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.  

Wanangu wamelala fofofo na wasipoamua haraka, watajipata kwa mikono ya adui wangu. Hana huruma na yeyote. Ni fedhuli. Ana kitu kimoja tu akilini mwake: Nguvu na mamlaka ya kuongoza. Atatawala kwa nguvu. Siwezi nikawafanya muelewe kwa undani atakayofanya. Huu ni wakati mgumu sana na kuna mambo mazito yajayo duniani. Sifurahii kuwaelezea mambo haya. Ninawaonya tu kuhusu yajayo kwa sababu sitaki mteseke kwa mikono ya adui wangu kwa ajili ya yale ambayo hivi karibuni yataikumba dunia. Jirudini wanangu. Amkeni kutoka usingizini. Ondoeni pazia machoni penu. Njooni kwangu haraka. Wakati uliobaki ni kidogo sana. Nikimbilieni kwa upesi. Nataka niwaokoe kutoka kwa maafa yajayo. Msipatwe na dhoruba inayokuja. Ni wachache sana watakaokuja nami nirudipo kumchukua bi arusi wangu. Ni wachache sana ambao wamechagua kunitazamia na kujiandaa kupitia kuoshwa na neno na damu yangu. Hakuna majibu. Hakuna njia nyingine.

Waefeso 5:25-27. Enyi waume wapendeni wake zenu, kama Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.

Jitoleeni kwangu sasa. Ni tayari kuwapokea. Nawataka mje kwangu ili muwe salama. Nitawafunika na kuwakinga na vitisho vijavyo duniani hivi karibuni. Jiokoeni wenywe na mje kwangu. Mimi pekee ndiye niwezaye kuwaepusha na haya. Nipeni mioyo na maisha yenu yote. Mtatayarishwa na Roho wangu Mtakatifu. Mwacheni awajaze na mtauona ukweli, ukweli wangu. Ni tayari kuwaleta ufalmeni mwangu. Je mwaja?

Huyu ni BWANA wenu YAHUSHUA. Ni mvumilivu nikiwasubiri muamue. Nichagueni ili mwokolewe!

 

 

SURA YA 38: WAFUASI WANGU KAMILI WANANITAZAMIA — WAMEJIHADHARI.

Binti, natuanze. Binti yangu, ni tayari kukupa maneno mapya: Wana, huyu ni BWANA anayezungumza nanyi. Saa imewadia ya kurudi kwangu na wanangu wamelala fofofo. Hawajijui wala hawajui yanayoendelea kando yao. Hata hawanitazamii. Ni wazi kuwa ni vipofu na macho yao hayako kwangu. Nitakuja kama mwizi usiku. Wengi watapatwa bila kujihadhari. Je, neno langu halisemi hivi? Ikiwa ni hivyo, mbona wengi wenu mnalipuuza? Mbona mnakataa kukesha na kuomba? Nawapa yaliyo mema nanyi mnanifanya wa mwisho maishani mwenu. Kama wanangu wangalikuwa wananifuata kwa karibu, wangalijua kuwa huu ni wakati wa kunitazamia, kunitafuta na kunisubiria. Wangeutambua ulimwengu ambao umewazunguka, na jinsi dunia inavyoendelea kunikataa katika pembe zote nne. Wafuasi wangu kamili wananitazamia. Wamejihadhari. Wametega masikio wanasikiza sauti ya hatua zangu. Wanatazama mienendo yangu yote na kusikia sauti yangu. Naja na hili sio jambo geni kwa wale wanaonitazamia. Hawa wana ni wavumilivu na wananingojea kwa hamu. Hili ndilo kanisa langu, bi arusi wangu. Yuapendeza na shauku yake juu ya kurudi kwangu inanipendeza. Napenda jinsi alivyo na hamu akiningojea. Huyu ndiye niliyemfia. Wafuasi wangu waminifu wanaoua ubinafsi wao na tamaa zao ili kuniishia mimi.

Luka Mtakatifu 12:37. Heri watumwa wale ambao Bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amini nawambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.

Wanayaweka maisha yao miguuni pangu na kuyaacha mambo ya dunia na kufuata Mungu wao. Nawashukuru sana kwa haya yote na zawadi zao hazitakwisha. Hili ndilo kanisa langu. Mwaweza kuwa mmoja wa kanisa hili, bi arusi wangu. Mwaweza kujitayarisha ili nikija niwachukue niwapeleke kwenye makao yenu huko mbinguni ambayo nimewaandalia. Wakati ulioko ni mfupi sana kwa hivyo muweke bidii ya kunifuata. Nataka mjitolee kote kote. Nataka mnipe  maisha yenu na kila kitu chenu. Msiache chochote. Nayataka maisha yenu yote. Nitawabadilisha na kuwapa maisha mapya ndani yangu. Nitawaosha na damu yangu muwe wasafi na niwajenge katika ufalme wangu; niwape nafasi kati ya wanangu ambao watanitumikia milele; wataishi na kutawala nami milele, kando yangu. Huyu ndiye bi arusi wangu. Ni mrembo. Watu waliojiandaa na kujitayarisha, wakikesha na kungojea MFALME wao. Naja kuwaokoa hawa wana, niwapeleke katika uhuru na usalama mbali na uovu ambao utaikumba dunia. Hawa ndio washindi wangu. Mwaweza kuwa miongoni mwao. Nawasubiri wanangu ili mje mshiriki katika karamu ya harusi yangu, muwe kati ya wale walio kwa ufalme Mungu. Nimewawekea nafasi katika meza yangu ya karamu ya ndoa yangu. Ni mahali ambapo nimewawekea ila ni lazima ninyi wenyewe kupadai. Sitaufungua mlango milele. Hivi karibuni, wanangu watapita kwenye mlango huu kisha nitaunfunga na kuwaacha wale waliokataa mwaliko wangu nje, wakabiliane na maovu yajayo. Itakuwa siku ya huzuni ilioje kwa wale wanaokataa kukubali maneno yangu! Watakapogundua kuwa wameachwa watakuwa na mahangaiko makubwa. Ndipo watakapojua kile ambacho wamekosa na yale ambayo wanaenda kukumbana nayo. Kutakuwa na majuto. Kutakuwa na kilio wakati kanisa langu vuguvugu litatambua makosa yake ya kukataa kuyasikiza maonyo yangu. Ndiyo, kutakuwa na simanzi kuu, watakapogundua kuwa wamepoteza nafasi yao katika ufalme wangu. Msiachwe ili mshuhudie giza litakalokuja duniani. Njooni kwangu. Jitoleeni kwangu, tubuni dhambi zenu zote mkijuta dhambi zenu na kuwa na tamaa ya kunifuata kwa mioyo yenu yote. Nitaibadilisha mioyo yenu na kuziosha dhambi zenu muwe wasafi kwa damu yangu. Hivyo mtasimama mbele yangu mkiwa mumejiandaa na kuwa tayari kushiriki kwenye karamu ya ndoa yangu kuu. Hii ndiyo hamu kuu niliyo nayo moyoni mwangu. Mnirudie. Mimi ni BABA yenu, MUUMBA wenu. Natamani mnijie ili niwafanye muwe wanangu wa kiume na kike. Mna nafasi sasa hivi ya kujirekebisha mbele zangu. Njooni ili tuishi wote milele. Naungojea uamuzi wenu.

Ni mimi BWANA wenu, MFALME wenu, MUNGU wenu, JEHOVA.

 

SURA YA 39: USHUHUDA WANGU KUHUSU KITABU HIKI NA KUFUNGA KWANGU

Bwana aliniita na kuniambia niende mahali pa faragha ili niombe na kufunga bila kula bali ninywe maji pekee. Baada ya wiki mbili, nilishiriki katika meza ya Bwana kila siku, kisha baadaye nikunywa maji ya machungwa glasi nne kila siku. Kufunga huku hakukuwa rahisi kwangu. Ni jambo ngumu sana ambalo nilitenda maishani mwangu. BWANA alinileta mahali hapa ili nijikane mwenyewe na tamaa zangu. Pia alinipa maneno ambayo nimeyaandika ili wengine wapate nafasi ya kuyasoma. Maneno niliyoyaandika hapa, Mungu aliyasema kwa sauti huku nikiyaandika. Ilikuwa mnamo mwaka wa 2012 kuanzia Januari 27, 2012 hadi Machi 6, 2012. Kuna barua zingine ambazo sikuweka tarehe kwa maana kwangu maneno haya yalikuwa muhimu kuliko tarehe. Wakati wa kufunga, Mungu aliniambia kuwa nikihisi njaa nimuulize anipe “Mkate wa Mbinguni.” Kwa hivyo kila wakati nilipohisi njaa, niliomba na kumuuliza anipe “Mkate wa Mbinguni” na mara tu maumivu ya njaa yalikwisha. Kweli MUNGU ni mkate utokao mbinguni.

Wakati mmoja nilikuwa nikisoma kitabu ambacho kilinifanya niamke. Kiliandikwa na mwanamke mmoja ambaye Mungu alikuwa amemuonyesha mbinguni na jehanamu. Na alisema kuwa katika jehanamu, watu daima wanahisi njaa na kiu. Nikajiuliza, “Ikiwa watu hawa watakuwa na kiu na njaa milele, mbona naona ugumu wa kufunga siku arobaini tu na angalau ninakunywa maji?” Tangu siku hiyo, niliweka bidii maana sikutaka kwenda jehanamu na kuishi huko milele nikihisi njaa na kiu. Nawataka ninyi pia mfikirie sana juu ya maisha yenu ya milele. Myatilie maanani maneno haya. Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kumaliza mfungo huu wa siku arobaini.

Kuhusu maneno haya, MUNGU alitumia maneno mengi ambayo hata mimi mwenyewe sikujua maana yake lakini wakati nilipoyatizama kwenye kamusi, nikayapata na yalikuwa sawa kabisa na vile alivyotaka niandike. Hakuna hata mabadiliko yo yote niliyofanya katika kitabu hiki. Yote yale MUNGU aliniambia niliyaandika vivyo hivyo.

UTUKUFU KWA NUNGU! ASANTE BWANA kwa uvumilivu wako juu ya chombo hiki kisicho na maana, Susan Davis.

YESU NDIYE MKATE KUTOKA MBINGUNI

Yohana Mtakatifu 6:29-58. 29 Yesu akawajibu, “Kazi anayotaka Mungu muifanye ni hii: mumwamini yeye aliyenituma.” 30 Wakamwambia, “Utafanya ishara gani ya muujiza, tuone ili tukuamini? Utafanya jambo gani? 31 Baba zetu walikula mana jangwani. Kama Maandiko yanavyosema, ‘Aliwapa mikate kutoka mbinguni wakala.”’

32 Yesu akawajibu, “Nawaambia kweli sio Musa aliyewapa mkate kutoka mbinguni. Baba yangu ndiye anayewapa mkate wa kweli kutoka mbinguni. 33 Kwa maana mkate wa Mungu ni yule aliyeshuka kutoka mbinguni na ambaye anatoa uzima kwa ulimwengu.”

34 Wakamwambia, “Bwana, tupatie mkate huo sasa na siku zote.

35 Yesu akawaambia, “Mimi ndiye mkate wa uzima. Ye yote ajaye kwangu hataona njaa kamwe, na ye yote aniaminiye, hataona kiu kamwe. 36 Lakini kama nilivyokwisha waambia, mnaniona lakini bado hamtaki kuamini. 37 Wale wote ambao Baba amenipa watakuja kwangu na ye yote ajaye kwangu, sitamtupa nje kamwe. 38 Kwa maana sikushuka kutoka mbinguni nije kutimiza mapenzi yangu, bali nitimize mapenzi yake yeye aliyenituma. 39 Na mapenzi yake yeye aliyenituma ni haya: kwamba nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa bali niwafufue wote siku ya mwisho. 40 Kwa maana mapenzi ya Baba yangu ni haya: wote wamwonao Mwana na kumwamini wawe na uzima wa milele. Nami nitawafufua siku ya mwisho.”

41 Wayahudi wakaanza kunung’unika kwa kuwa alisema: “Mimi ni mkate ulioshuka kutoka mbinguni.” 42 Wakasema, “Huyu si Yesu mwana wa Yusufu? Na baba yake na mama yake si tunawajua? Anawezaje basi kutuambia kwamba ameshuka kutoka mbinguni?”

43 Lakini Yesu akawaambia, “Acheni kunung’unika. 44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu kama Baba aliyenituma hakumvuta kwangu; nami nitamfufua siku ya mwisho. 45 Kama manabii walivyoandika, ‘Wote watafundishwa na Mungu.’ Ye yote amsikilizaye Baba na kuji funza kutoka kwake, huja kwangu. 46 Hii haina maana kwamba kuna mtu aliyekwisha kumwona Baba. Ni yule aliyetoka kwa Mungu peke yake, ndiye aliyekwisha kumwona Baba. 47 Nawaambieni kweli: anayeamini anao uzima wa milele. 48 Mimi ni mkate wa uzima. 49 Baba zenu walikula mana jangwani, wakafa. 50 Lakini hapa kuna mkate utokao mbinguni ambao mtu ye yote akiula, hatakufa. 51 Mimi ni mkate wa uzima uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu ataishi milele. Na mkate wenyewe ni mwili wangu ambao nitautoa ili watu wote ulimwenguni wapate kuishi milele.”

52 Hapo Wayahudi wakaanza kubishana kwa hasira wakiulizana, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?”

53 Kwa hiyo Yesu akasema, “Ninawaambieni hakika, msipoula mwili wangu mimi Mwana wa Adamu na kuinywa damu yangu, hamtakuwa na uzima ndani yenu. 54 Mtu ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. 55 Kwa maana mwili wangu ni chakula halisi na damu yangu ni kinywaji halisi. 56 Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu anaishi ndani yangu na mimi ninaishi ndani yake. 57 Kama vile Baba wa uzima alivyonituma, na kama nipatavyo uzima kutoka kwake, kadhalika, ye yote anilaye ataishi kwa sababu yangu. 58 Huu ndio mkate uliotoka mbinguni, si kama ule mkate walio kula baba zenu hatimaye wakafa. Alaye mkate huu ataishi milele.” 59 Yesu alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika sinagogi huko Kapernaumu.

 

Impressum

Tag der Veröffentlichung: 03.03.2016

Alle Rechte vorbehalten

Nächste Seite
Seite 1 /